Utajiri wa Mfanyabiashara Elon Musk wazidi kuongezeka

Manyanza

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
16,464
Reaction score
35,629
Mfanyabiashara maarufu wa Marekani, Elon Musk amekuwa Mtu wa kwanza katika historia duniani kufikisha thamani ya juu ya utajiri wa dola bilioni 400 za Kimarekani ( zaidi ya Trilioni 970 za Kitanzania) baada ya kuongezeka kwa utajiri wake kutokana na ushindi wa Rais mteule Donald Trump katika uchaguzi wa Marekani uliofanyika Novemba mwaka huu.

Ripoti zinaeleza kuwa Utajiri wa Musk kwa sasa ni mara mbili ya Mtu tajiri wa pili duniani ambaye ni Jeff Bezos mwenye utajiri unaokadiriwa kufikia dola bilioni 244 za Kimarekani (zaidi ya Trilioni 590 /- za Kitanzania) ambapo kwa mujibu wa Bloomberg utajiri wa Musk umeongezeka kutokana na kupanda kwa hisa za Kampuni yake ya Tesla na SpaceX.

Hisa za Tesla zimeongezeka kwa zaidi ya asilimia 60 tangu wakati wa uchaguzi wa Marekani huku kukiwa na matarajio kwamba Rais mteule, Donald Trump atafutilia mbali kanuni zinazoonekana kurudisha nyuma maslahi ya biashara za Musk na kumfanya aendelee kufanya vizuri zaidi kutokana na nafasi aliyopewa ya kusimamia Ufanisi wa Serikali ya Trump atakapoanza kazi Januari 2025.

Haya yanajiri ikiwa ni wiki chache tu zimepita tangu Serikali ya Tanzania kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kutangaza kupokea maombi kutoka kwa Kampuni ya Starlink Satellite Tanzania Limited inayomilikiwa na Elon Musk kupitia Wanahisa wa Starlink Holdings Netherlands B.V na SpaceX Netherlands B.V kuomba leseni ya kitaifa ya miundombinu na leseni ya kitaifa ya Huduma ya mifumo tumizi kuendesha shughuli zao Nchini Tanzania.
 
Soma zaidi Elon Musk becomes first person with $400 billion net worth; leaves Jeff Bezos and Mark Zuckerberg behind | - Times of India
 
Hizo dola bilioni 400 ni bajeti ya Tanzania kwa miaka mingapi?
 
Halafu kuna mafukara hapa JF yana aminishana kuna utajiri wa kishetani.
Teh teh tehee,kama mimi kuna jamaa alinambia ati kutengeneza ndege na kuruka vile ni uchawi wa wazungu ati!!,,eti timu zao kushinda ni uchawi tu,hizi dhana ndo zatufanya tusipige hatua za kimaendeleo,.
 
Msiaahau pia jumuiya ya nchi za ulaya umepiga marufuku ndege za Tanzania kutua kwenye viwanja vyao.. hazina usalama
Ya lini hii Kiongozi? Duh! Nyang'au kishatia fitna wallahi!
 
Wealth based on speculation.....ukiangalia revenue ya telsa ambayo ndiyo inamlipa zaidi haijashoot for the past 12 months
 
Back
Top Bottom