Shadrack K. Lwila
JF-Expert Member
- Jul 17, 2016
- 4,925
- 14,287
Naweka mark
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hahahahaha upo huku halafu kwenye uzi wa rikiboy sijawahi kukuona ukipita Miss Anne 😂😂😂Ally Mpemba ni noma
Ona ashamroga jamaa, haweki tena hadithi
Sent from my TECNO CG6 using JamiiForums mobile app
Utafanya wengin tushindwe kulala manaka hii linakaribia kabisa kufanana na mayaUmughaka wee ni nyosoView attachment 2479982
Akahamia rasmi kwenye nyuzi za kuponda walimu.UMUGHAKA tangu amejenga ukaribu na mpwayungu village matokeo ndio aya tunayaona,mpwayungu alianzisha story yake ghafla akatokomea kusikojulikana mpaka leo
Nije tulale wote, upate ulinz wa bureee ?Utafanya wengin tushindwe kulala manaka hii linakaribia kabisa kufanana na maya
Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani - 13.
Ile sauti ya mtetemo iliendelea sana kana kwamba hicho kitu kilichokuwa humo chumbani kilikuwa kimekasirishwa,nilisimama taratibu nikatembea kwa kunyata hadi kwenye mlango wa kile chumba,nilipofika kwakuwa muda wa kukifungua ulikuwa bado,nilitegea sikio kwa makini kusikiliza kilikuwa ni kitu gani,nilitulia kimya kabisa lakini ile sauti ya mtetemo ilikoma,niliamua tena kunyata na kurudi sebuleni.
Muda wa kufungua ule mlango ulipowadia nilinyanyuka na kwenda kuufungua,sasa nilipofungua ule mlango kama kawaida niliuacha wazi kisha nikawasha taa za nje nikatoka zangu ndani kuelekea nje.Siku hiyo sikutaka kabisa kutoka kwenda kula kwasababu nilikuwa nimekula muda siyo mrefu hivyo nikawa nimeshiba,kwakuwa bado ilikuwa mapema,niliona nifungue ile gari nikae ndani nitulie hadi nitakapopitiwa na usingizi,nilifungua vioo vya mbele vya ile gari upepo ukaanza kuingia ndani lakini nilipoona mbu wanazidi kuingia kwa kasi nilivifunga kisha nikawasha AC nikaendelea kula upepo.
Ilipofika mida ya saa 3 usiku kukiwa kumetulia,nilianza kusikia sauti ya kitu ambacho sikukielewa kilikuwa ni kitu gani kikiwa kinatafuna kwa sauti na miguno kama ya nguruwe,ile sauti ilikuwa inasikika kwa nguvu sana kiasi kwamba ikabidi nifungue mlango wa gari na kushuka,baada ya kutoka kwenye gari nilisimama kando ili niweze kuisikia ile sauti vizuri.Hali ile hakuna mwanadamu mwenye moyo ambaye asingeiogopa,mimi pamoja na ujasiri wangu wa kikurya lakini ilifika sehemu nikawa naogopa sana lakini niliendelea kuwa mvumilivu na kumdhibitishia Ally Mpemba ya kwamba mimi ni mwanaume na ni mwaminifu,hivyo mategemeo yangu yalikuwa ni ipo siku atanipa fedha au sehemu ya mali zake kutokana na uaminifu wangu kwake.
Ile sauti ilipozidi,nilisogea hadi pale mlangoni kwa kunyata kisha nikawa nasikiliza kilikuwa ni kiumbe wa aina gani aliyekuwa mle ndani,kiukweli ilikuwa ngumu kutambua kama alikuwa mwanadamu au mnyama,kwasababu nilichokuwa najiuliza,kama ni mwanadamu anawezaje kutafuna kwa kasi kiasi kile na miguno kama ya nguruwe?
Kwa watu mliofuga nguruwe au mlioishi na nguruwe nadhani hapa mtakuwa mnanielewa,kile kitu kilichokuwa humo ndani kilikuwa kinatafuna na kuguna kwa utamu kama nguruwe anapokuwa anakula.
Pia kama ni mnyama,Je alikuwa ni mnyama gani?,kiukweli niliendelea kujiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu,niliona nijiondokee zangu nirudi kwenye gari kutulia,nilipitiwa na usingizi nikajikuta naamka saa 12 baada ya kusikia milio ya magari huko nje,niliamka haraka na kwenda kuufungua ule mlango na kuzama ndani,nilipofika ndani niliwasha taa za pale sebuleni na kukuta kile kitambaa kilichokuwa pale juu ya meza kimetupwa chini na nilipoangalia chini nikakuta kuna ute ute mzito kama ambao hutoa ng'ombe akiwa anatafuna nyasi,zile kabeji pamoja na mboga za majani sikuzikuta hata kipande tu,kiukweli niliingiwa na hofu sana na sikutaka kusubiri nilielekea moja kwa moja mpaka kwenye kile chumba na kukifunga.Nilipokifunga kile chumba angalau sasa moyo wangu ulitulia,niliingia jikoni nikachukua dekio (Mop) nikaenda kusafisha ule ute mzito kisha kile kitambaa nikakirudisha jikoni kama kawaida.
Baada ya kumaliza lile zoezi,nilitoka nje nikafunga mlango kisha kuelekea bombani kunawa,nilipomaliza kunawa uso na kusukutua nilirudi kwenye gari kusikilizia hadi mida ya saa 2 ili niondoke niingie Kkoo kufanya kazi yangu ya usajili.Baada ya muda kufika niliondoka nikaelekea Buguruni ofisini ambako vikao vilikuwa vinafanyika kila siku na ilikuwa ni lazima kuhudhuria,baada ya kumaliza kikao nilichukua box la line kisha nikaondoka zangu Kkoo,sasa wakati nipo kariakoo napiga kazi,Ally Mpemba alinipigia simu na kutaka nimpatie taarifa za usiku.
Ally Mpemba "Assalam aleykum"
Mimi "Alekom salam "
Ally Mpemba "Wajionaje na hali?"
Mimi "Niko vema kabisa kaka"
Ally Mpemba "Mambo yalienda vyema?"
Mimi "Ndiyo kaka hakuna kilichoharibika"
Ally Mpemba "Hakukuwa na usumbufu kama wa jana?"
Mimi "Hapana kaka"
Nilitaka nimuulize jamaa ni kitu gani kilikuwa mle ndani lakini nilikuwa nasita sana na niliona ningemuuliza uenda ningeharibu uhusiano wetu ambao tayari ushaanza kuwa mkubwa,niliamua nipige kimya ili mambo mengine mazuri yaliyokuwa mbele yangu nisiyazibe.
Ally Mpemba "Sasa utamwambia Farah akupe elfu 50 na utafanya kama ambavyo ulifanya jana"
Mimi "Sawa kaka"
Baada ya mazungumzo jamaa akawa amekata ile simu.Ilipofika mida ya saa 10 Alasiri,niliamua nifunge nirudishe vifaa vyangu vya kazi mahali ambapo nimekuwa nikivihifadhi,nilirudi hadi dukani pale nikamwambia yule sister Farah anipatie kiasi cha fedha kama ambavyo Ally Mpemba alikuwa ameniambia.
Farah "Mbona sikuhizi wawahi sana kufunga!"
Mimi "Hata muda wa usajili umebaki mchache na kuna mahali inabidi niwahi"
Farah "Ooh ok nambie"
Mimi "Brother Ally aliniambia unipatie elfu 50"
Farah "Ally kaka yangu au Ally yupi!?"
Mimi "Yes,brother Ally"
Farah "Mbona hajaniambia "
Aliendelea "Ngoja nimtafute nithibitishe"
Baada ya kumpigia Ally Mpemba na kumpata hewani walikuwa wakiongea lakini yule demu nikama alikuwa akimuuliza Ally mimi na yeye tunabiashara gani kwasababu jana alitoa elfu 50 akanipa na leo tena anatoa elfu 50 kunipatia,sikujua Ally Mpemba alimjibu kitu gani,alichukua elfu 50 akanipatia kisha mimi nikaondoka kuelekea sokoni kununua bidhaa kama ambazo nilinunua jana,maelekezo yalikuwa ni yale yale.
Kiukweli kwa muda huo nilikuwa napata sana hela kwasababu kununua mahitaji yote yale nilikuwa natumia chini ya elfu 20 na elfu 30 iliyokuwa inabaki ilikuwa yangu na Ally Mpemba hakuwahi kuiulizia kabisa,kila siku nilikuwa napewa elfu 50 kwa ajili ya manunuzi.
Kama kawaida niponunua bidhaa nilirudi hadi nyumbani Kwa Ally Mpemba na kuyaweka kama ambavyo nilikuwa nimeelekezwa.Ilipofika jioni muda wa kufungua kile chumba,niliamua kufungua pazia la pale sebuleni kisha nikawasha taa,lengo langu ilikuwa ni kuhakikisha siku hiyo nakiona kile kiumbe ambacho sikukifahamu kilikuwa kiumbe cha aina gani!;baada ya kufungua pazia na kuwasha taa,nilienda kuufungua ule mlango na kuacha wazi kisha nikatoka nje.
Niliamua kukaa kando ya lile dirisha la pale sebuleni huku nikiwa na shauku kubwa ya kuona ni kitu gani kilikuwa mle ndani,ilipofika mida ya saa 2 usiku,nilitoka nje nikaelekea kununua chips na soda kisha nikawahi kurudi,nilipofika breki ya kwanza ilikuwa ni kwenye dirisha la pale sebuleni,niliangalia kwa umakini na ndipo niliona zile kabeji na mboga za majani uilikuwa hazijaliwa,hivyo nikaa pale pembeni nikaanza kula huku nikisubiri nione ni kitu gani kilikuwa mle ndani.
Nilikaa sana pale chini hadi mida ya saa 5 usiku lakini kila nikichungulia hakukuwa na dalili ya kitu chochote,niliamua kufungua mlango na kisha kuingia ndani ili nikafunge yale mapazia na kuzima taa,nilipomaliza nilitoka nje kisha nikakaa pale mlangoni na kusikiliza,ndipo haukupita muda nikaanza kusikia utafunaji wa ovyo na papara ukiendelea kama kawaida,niliondoka nikaingia kwenye gari kwenda kulala kama kawaida huku kile kiumbe kikiendelea na utafunaji wake wa sauti kama nguruwe.
Asubuhi kama kawaida niliingia ndani nikafunga ule mlango kisha nikaanza kufanya usafi pale sebuleni kama kawaida,nilipomaliza niliondoka kuelekea kazini kama kawaida.
Sasa ilipofika mida ya saa 3 asubuhi nikiwa tu ndo nimeanza kazi,alinipigia simu Ally Mpemba.
Ally Mpemba "Kaka salama?"
Mimi "Salama kabisa,vipi wewe huko?"
Ally Mpemba "Huku naendelea vema ila narudi wiki ijayo"
Mimi "Sawa kaka,nambie"
Ally Mpemba "Kuna mtu nimempa namba yako atakupigia simu ana mzigo wangu utaenda atakupatia"
Mimi "Sawa kaka ni mzigo gani?"
Ally Mpemba "Ni pesa,hakikisha akikupatia utanipelekea Benki Crdb,nitakutumia vielelezo"
Mimi "Sawa kaka hakuna tatizo"
Ally Mpemba "Pia nimemwambia Farah kuna pesa atakupatia,utachukua utanunua mahitaji yale kama kawaida na itakayobaki utatumia "
Mimi "Nashukuru sana Kaka Ally"
Ally Mpemba "wala huna haja ya kunishukuru,mimi ndiye ninapaswa kukushukuru "
Aliendelea "Nitakufanyia mambo makubwa sana kwa uaminifu wako"
Mimi "Sawa kaka nitashukuru sana"
Baada ya mazungumzo yale mafupi Ally Mpemba akawa amekata simu.
Ilipofika mida ya saa 7 mchana,kuna namba ngeni ikawa imenipigia simu,ilikuwa ni sauti ya mwanamke ambaye alijitambulisha kama Warda.
Mimi "Ndiye mimi"
Warda "Ally kaniambia kuna mzigo wake nikupatie,sijui nakupataje?"
Mimi "Wewe uko wapi?"
Warda "Njoo hapa mtaa wa mkunguni ukifika uniambie"
Mimi "Sawa nakuja muda si mrefu"
Mimi "Aunt Farah samahani naomba unitazamie hapo narudi mara moja"
Farah "Kwani ndo unafunga?"
Mimi "Hapana,kuna mahali nafika mara moja ila nawahi kurudi"
Farah "Ooh sawa kuna hela Ally ameniambia nikupatie,hivyo ukitaka kuondoka utaniambia"
Mimi "Sawa nawahi kurudi"
Itaendelea........
Muendelezo soma Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani
We jamaaa mbna una husda ya wazi hivi!? yaani una wish ungekua mke wa mwambaAnd you think that you are already educated? Kiswahili tumekufundisha na bado hata unaandika unakosea. Acha kiingereza its not your mother tongue i cant blame you for that. Hii dunia tenda wema wende. Unajiona tayari nawe ni super star? Umetukuta lakini.
Daaaah.....kweli wanawake mkiamua kupenda mnapenda. Hii text umeandika kwa mahaba. Na unamwona jamaa tayari ni mwamba wako.....🤣 Umenikumbusha mbali sana. Kuna demu alikuwa ananiita hivyo.... Ngoja aje Chizi Maarifa akujibu. Sema nimeona una mapenzi sana kwa mugakaWe jamaaa mbna una husda ya wazi hivi!? yaani una wish ungekua mke wa mwamba
Bado tu haujapata viazi vya kutosha huko Mbeya mkuu?Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani - 17.
Nikiwa njiani naelekea kwake alinipigia simu akinitaka nipitie pale Big Bon nimsubiri atoke msikitini kisha tuandamane nae hadi kwake.Baada ya muda kupita Ally Mpemba alirudi kutoka msikitini na aliniambia nipande gari yake kisha tuondoke.
Ally Mpemba "Swalama master"
Mimi "Mimi niko poa kaka"
Ally Mpemba "Usiogope mdogo wangu haya ni mambo ya kawaida sana hapa mjini!"
Aliendelea "Wewe nakuona utakuwa mtu mkubwa sana "
Mimi "Kweli kaka?"
Ally Mpemba "Wewe tulia tu utajionea"
Tulipofika kwake nilitelemka kwenye gari na kwenda kufungua geti kisha akaingiza gari ndani.
Sasa tulipofika ndani mimi nilikaa pale sebuleni halafu Ally Mpemba yeye akawa amepitiliza moja kwa moja kuingia chumbani kwake,ilipofika mida ya saa 10 Alasiri nikiwa nimekaa pale sebuleni nikisubiri animbie alichoniitia,ndipo nikahisi mkononi nimeanza kubanwa na ile bangiri;Ilibana kwa nguvu huku damu ikaanza kunitoka kwenye mkono ambayo haikuwa nyingi sana,ilipoendelea kubana sana hadi kuihisi maumivu nilichomoa kile kichupa kidogo cha Gliselin kilichokuwa na ule mchanganyiko wa damu na dawa nikaanza kuipaka ile bangiri,baada ya dakika 2 hivi ndipo nikahisi ile hali ya kubana inaachia.Kiukweli baada ya lile tukio nilijisikia mwepesi kupita maelezo,kila jambo mbele yangu niliona halina kizuizi chochote.
Nikiwa naendelea kumsubiri Ally Mpemba pale sebuleni nilisikia ule mlango wake ukifunguliwa na ndipo kutazama nikidhani ningemuona Ally Mpemba haikuwa hivyo,alikuwa ni yule kiumbe wa ajabu akitoka ndani ya kile chumba akirudi kwenye chumba chake,sikuelewa alichokuwa amefata ni nini kwenye kile chumba na alionekana kama kushangaa sana!.
Baada ya muda Ally Mpemba nae alitoka ndani kisha akakifunga kile chumba.Sikujua yule kiumbe alipita muda gani kuingia kwenye chumba cha Ally Mpemba wakati nikiwa pale sebuleni kwasababu ile nyumba namna ilivyokuwa imekaa,ilikuwa rahisi mtu akitoka au kuingia chumbani kuonekana,yawezekana alikuwa chumbani kwa Ally Mpemba muda mrefu na Ally Mpemba alipofungua chumba basi alimwambia aondoke aelekee chumbani kwake kulikokuwa na shimo chini ya kabati.
Lakini kilichonishangaza zaidi ni muda Ally Mpemba aliotumia alipoingia chumbani,tulifika hapo nyumbani kwa Ally mida ya saa 8 mchana baada ya kutoka Kkoo,mimi niliendelea kukaa pale sebuleni hadi mida ya saa 10 alasiri ndipo kubwana na ile bangiri ambayo niliambiwa ni Alfwat anakula;kuna masaa kama mawili Ally Mpemba alikuwa chumbani kwake na yule kiumbe ambaye hadi wakati huo nilikuwa simuogopi baada ya kuzoea yale mazingira na kuhakikishiwa na Ally Mpemba usalama wangu wa Kimwili na Kiroho.
Ally Mpemba "Vipi zoezi lako limekamilika?"
Mimi "Ndiyo kaka "
Ally Mpemba "wewe ni muaminifu sana na ndiyo maana nakupenda sana!"
Aliendelea "Kama nilivyokwambia,wewe utakuwa mtu mkubwa sana kwasababu huogopi kuyatafuta mafanikio"
Aliendelea "wabongo wengi hawafanikiwi kwasababu wanadhani mafanikio hujileta tu kwa kupiga blah blah,mafanikio yanatafutwa kwa nguvu isiyokuwa ya kawaida master"
Aliendelea "Nitakusapoti mwanangu kwakuwa na wewe umenisapoti na umeonyesha uaminifu kwangu tangu nilipokuamini,sikukosea kukuchagua uwe rafiki yangu!"
Aliendelea "Kwasasa hizi ni hatua za awali tu ila nakuona mbali sana,ukiendelea hivi sidhani kama nitakusogelea kwa pesa master"
Kiukweli maneno ya Ally Mpemba yalinichochea sana hadi kuwaza kufanya mambo makubwa ili nipate pesa na mimi niwe mtu maarufu mjini na niendeshe magari ya gharama kama watu wengine.
Baada ya maongezi yale na Ally Mpemba nilimuuliza uenda kulikuwa na ishu yoyote alitaka kuniambia ili niweze kurudi nyumbani mapema.
Ally Mpemba "Hivi unaweza kuendesha gari?"
Mimi "Ndiyo kaka naweza japo sina leseni!"
Ally Mpemba "Ulijifunzia wapi gari master wewe!"
Mimi "Kaka wala sikwenda chuo kujifunza bali kuna mahali nilikuwa napewa kusogeza kidogo tu hadi nikafahamu kimtindo!"
Ally Mpemba "Kwahiyo unaweza kusogeza kimtindo?"
Mimi "Ndiyo kaka!"
Ally Mpemba "Ulikuwa muosha magari nini!"
Mimi "Kwanini kaka?"
Ally Mpemba "Nimeuliza tu maana jamaa wao ndiyo huwa wanaweza kusogeza kimtindo lakini kuendesha kwao ni changamoto!"
Mimi "Hapana kaka,mimi nilijua kusogeza gari miaka fulani nilikuwa mpiga debe"
Ally Mpemba "Duuuu ushawahi kuwa mpiga debe?"
Mimi "Ndiyo kaka!"
Ally Mpemba "Basi kama ndivyo wewe ni faita,kumbe nakuchukulia poa eeeh!"
Mimi "Kawaida tu kaka ni moja ya utafutaji!"
Ally Mpemba "Ok,sasa itabidi nikusajilie ile gari Aud ili uwe unatembelea miradi yangu pamoja na kufanya ishu zako ziwe rahisi!"
Mimi "Kweli kaka?"
Ally Mpemba "Sijawahi kuongopa na ninachoamini wewe unakuja kuwa mkubwa zaidi yangu,jambo la msingi ni kunitunzia siri vinginevyo tusije tukalaumiana!"
Mimi "Kaka kwa hilo tu usijali "
Ally Mpemba "Hapa kwangu umewahi kumuona mtu mwingine zaidi yako kwa muda huu tu ambao nimefahamiana na wewe?"
Mimi "Hapana kaka sijawahi kumuona mtu yeyote!"
Ally Mpemba "Ok,je umewahi kumuona ndugu yangu yeyote hapa kwangu kwa wale unaowafahamu?"
Mimi "Hapana kaka"
Ally Mpemba "Ok uwe unajiuliza kwa nini wewe ninakupa kipaumbele kuliko ndugu zangu!"
Aliendelea "Wewe ni mtu muhimu sana kwangu hivyo usije ukafanya nikakosa uamimifu kwako itakuwa ni mbaya sana katika maisha yako!"
Mimi "Sawa kaka sitokuangusha"
Ally Mpemba "Hivi karibuni nataka kufanya safari ya Oman ila kabla ya kuondoka nitaomba uwe unanisitiri kwa kipindi chote ambacho sitokuwepo!"
Mimi "wala usijali kaka wewe ushakuwa zaidi ya ndugu!"
Sasa baada ya kusikia jamaa anataka kunipatia ile Aud mpya niwe natembelea,kiukweli nilikuwa nina furaha ya ajabu na nilijikuta nawaza mambo mengi sana na jambo ambalo lilikuwa la kwanza kichwani mwangu baada ya kupata ile gari,safari ya kwanza ingekuwa kwa mjomba Nico kule Ununio ili niende nikaonyeshe taizi la nguvu na kuonyesha sikuhizi niko Matawi ya juu,pili nilipanga niwe naingia nalo pale ofisini buguruni kuwalingishia wale mademu waliokuwa na nyodo na kuniona mimi mshamba!.Kiukweli niliona kama jamaa ananicheleweshea ile mashine na ndiyo maana ilifikia wakati kila jambo alilokuwa akiniambia nilikuwa nikimjibu kwa haraka haraka bila kujiuliza mara mbili mbili madhara ya kile kitu alichokuwa ananiambia.
Ally Mpemba "Unajua maana ya kunisitiri lakini master?"
Mimi "Kaka sitoweza kupayuka kwa watu na kama nikifanya hivyo wewe nifanye unavyoweza"
Ally Mpemba "Mimi simaanishi hivyo master,siyo kwamba sikuamini kwamba wewe ni msiri ila nahitaji uwe unanisitiri kwa kipindi chote hicho ambacho sitokuwepo"
Mimi "Kaka kukusitiri kiaje?"
Ally Mpemba "Umefanya vema kuniuliza na mimi nilisubiri swali lako sema ulikuwa unazunguka!"
Aliendelea "Nadhani wewe waweza kuondoka halafu mambo mengine nitayashughulikia mimi"
Mimi "Kaka hujaniambia lakini kuhusu kusitiri "
Ally Mpemba "Nitakujuza tu wala usijali,siku ya kuondoka nadhani gari nayo itakuwa tayari hivyo nitakujuza"
Mimi "Sawa kaka,basi mimi ngoja niwahi usafiri wetu wa kugombania"
Ally Mpemba "Nisubiri kidogo nakuja"
Baada ya kuniambia nimsubiri,aliingia chumbani ambako hakuchukua muda akawa ametoka na kiasi fulani cha pesa na kunikabidhi nikitumie kama nauli.
Mimi "Nashukuru sana kaka!"
Ally Mpemba "Hupaswi kunishukuru,mimi ndiyo napaswa kukushukuru!"
Niliondoka zangu mle ndani kuelekea nje kisha nikaanza kuhesabu zile hela nikakuta ilikuwa laki 2,kiukweli nilifurahi sana kimoyo moyo na kujiona ni mtu mwenye bahati sana kuwa na urafiki na Ally Mpemba mwenye asili ya arabuni.
Nilipanda zangu gari za gongo la mboto zilizokuwa zinatokea maeneo ya Morocco,ingawaje zilikuwa zimejaa lakini hakukuwa na namna,nilichowaza mimi nikufika nyumbani sikuwaza uwingi wa abiria.Baada ya kufika nyumbani mida ya saa 12 jioni nilifungua mlango na kuingia ndani,nilipofika sebuleni kwangu niliwasha taa kisha nikawa naelekea chumbani,kama nilivyosema hapo awali ya kwamba,nikuwa nimepanga kwenye nyumba ya vyumba viwili,hivyo kulikuwa na chumba na sebule,ndani kwangu kulikuwa na kila kitu ambacho kijana wa kisasa angetamani kuwa nacho.
Baada ya kufungua chumba na kuingia ndani niliwasha taa,sasa nilipowasha taa kuna hela ambazo zilikuwa mpya noti za shilingi elfu kumi kumi nilizikuta pale kitandani,kiukweli nilishangaa sana zile hela na sikujua ni nani alikuwa ameziweka hapo kitandani,nilidhani uenda ile asubuhi wakati natoka nilizisahau pale kitandani lakini bado haikuingia hakilini kwasababu sikuwa na hela yeyote hapo ndani kwa wakati huo.Niliamua kusogea na kuzikamata zile hela na kuanza kuzihesabu moja baada ya nyingine,sasa wakati nahesabu zile hela nikawa nasikia kuna mtu anagonga mlango!.
Nilitoka chumbani kwenda kuufungua ule mlango,baada ya kuufungua ule mlango kumbe alikuwa ni yule demu wake na Steve.
Zuu "Shem mambo"
Mimi "poa,mambo vipi?"
Zuu "Safi,niazime simu yako nimpigie Steve maana kwangu sina salio!"
Mimi "Ok ngoja nikuletee"
Niliingia ndani nikachukua simu kisha nikampigia simu Steve baada ya kumpata nikampa aongee na demu wake kisha mimi nikarudi chumbani kwenda kuendelea kuhesabu zile hela,nilipokuwa nikiendelea kuhesabu zile hela,demu wa jamaa aliniita niende nikachukue simu,sasa nilipofika nilikuta bado simu haijakata na ndipo akaniambia Steve anaomba kuongea na mimi.
Mimi "Mwanangu niambie!"
Steve "Mwanangu naomba umuazime shemeji yako gesi yako apikie maana kwangu imeisha,nikirudi nakuja kuchukua kaka"
Mimi "Usijali kaka ngoja nimpatie hela akabadili mtungi halafu wewe utanirudishia!"
Steve "Utakuwa umenisaidia sana mwanangu"
Baada ya kuelewana na Steve,niliingia ndani nikachukua elfu 50 kwenye zile hela ambazo Ally Mpemba alinipatia kama nauli nikawa nimempatia demu wa jamaa ili akabadili mtungi wa gesi,baada ya kumpatia mimi nilirudi ndani kuendelea na zoezi la kuhesabu zile hela,baada ya kumaliza kuzihesabu jumla yake zilikuwa milioni 5,kiukweli nilifurahi sana na nikaona mambo yangu yanazidi kunyooka tu bila kutumia nguvu nyingi.Sasa mpango wangu ulikuwa ni kwamba,nichukue zile hela niongezee na ambazo nilikuwa nimedunduliza benki ili nianze kufanya biashara ya viazi mbatata kutoka Mbeya na niachane na mambo ya kusajili line za simu.
Kwakuwa dhamira yangu ilikuwa kuwa mfanyabiashara mkubwa wa viazi mbatata hivyo nikaona nianze kutengeneza koneksheni ya madalali pale soko la Ilala na Mabibo ili kuweza kulifahamu na kuliteka soko,sasa baada ya kujiridhisha bei ya soko nikaona nichukue kale ka hela kangu nilikokuwa nimedunduliza benki pamoja na ile hela niliyoikuta pale kitandani kisha nikapata milioni 7.
Niliamua kumpigia simu team leader na kumdanganya kwamba naelekea nyumbani kulikuwa na matatizo huku lengo langu ni kuelekea mkoani Mbeya kukusanya viazi mbatata na kuvileta mjini ili nipige pesa,lengo la kumuaga team leader ni asiendelee kuniona mzembe katika kazi ile ya kusajili line ili kuendelea kuweka uaminifu asije kuninyang'anya kodi akampatia mtu mwingine,nilitaka ile kazi niiache mdogo mdogo bila kuondoka kwa dharau maana nilichoamini ni kwamba maisha hubadilika.
Niliianza safari ya kuelekea Mbeya kwenda kukusanya viazi na kuvileta mjini.
Itaendelea .............
Dah nilikuwa mdogo kiasi Ila Yale magazeti yakusumbua Sana mtaa jamani,yaani linazunguka mtaa mzima😂😂,baadae likatoka lingine kinaitwa Tabasamu dah! cover Sasa wanachora wadada wana misambwanda hiyo balaaMi' nashauri, kwa yeyote anayetaka kutuletea hadithi hapa, awe amejiandaa. Hayo mambo ya tutaendelea..... Yabaki kwenye TV na magazeti.
Wakongwe wenzangu watakumbuka enzi zileeeee za gazeti la SANI, lilikuwa halina siku maalumu. Laweza kutoka leo, litalofuata, basi ni baada ya mwezi, au hata baada ya miezi mitatu!
Basi, wasomaji wa hadithi pendwa zile za akina SAID BAWJI, NICCO YE MBAJO pamoja na ile michoro ya PHILIP NDUNGURU, mtasubiriiiiii weeeee, mpaka mnasahau mlipoishia!
Haya mambo ya… TUTAENDELEA… wasimuliaji wetu, tuyapunguze!