Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani

Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani

Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani - 18.



Nilifanikiwa kufika Mbeya na kuanza kuzunguka kukusanya viazi huku nikiendelea kuwatumia madalali ili kufanikisha kwa haraka niweze kurudi mjini kuuza mzigo.

Nilitumia takribani wiki 1 kununua mzigo na kupakia kwenye fuso kisha kuuleta mjini Dar es salaam,nilipofikisha mzigo mjini hali haikuwa kama nilivyodhani mwanzo,wale madalali ambao niliongea nao tangu mwanzo nilipokutana nao walianza kuniambia mzigo kwasasa umekuwa mwingi na umeshuka bei,niliamua mwenyewe kupita na kufanya utafiti kwenye masoko ya Ilala,Buguruni na Mabibo na kugundua ya kwamba wale madalali walikuwa na nia ya kunipiga kwasababu hakukuwa na mzigo mwingi wala nini!,nilichoamua ni kuanza kuuza ule mzigo mwenyewe,ule mzigo kiukweli ulinikata sana na namshukuru Mungu niliambulia kiasi kidogo cha pesa kwasababu kuna magunia mengine ya viazi yalioza kwasababu ya kukaa chini muda mrefu bila kuuzwa,nilichogundua ni kwamba wale madalali mwanzo walikuwa wakinipanga ili nilete mzigo mjini na nikiisha ufikisha wao ndiyo wanipangie bei ya kuuza,wao wajipatie pesa nyingi kupitia mzigo wangu halafu mimi nipate faida kidogo,sasa nilipowakataa wakasambaza maneno kichini chini kwamba mzigo wangu haufai hivyo kila mteja akawa anaupita tu kama anaaga maiti kiukweli ile hali ilinifedhehesha sana hadi kuna watu ambao ni wema walinishauri niuuze wote kwa jamaa mmoja pale Mabibo ambaye alikuwa ni dalali na alinipatia fedha nusu ya mtaji,kiukweli kwasababu ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kuifanya ile biashara sikutaka kabisa kuendelea nayo kwasababu ilikuwa na fitina kubwa mno,na mpaka leo sielewi watu wengine wanawezaje kufanya biashara ya viazi.

Baada ya kuona hiyo biashara imenishinda kwasababu ya fitina ya mswahili,niliamua kurudi zangu kwenye usajili wa laini za simu huku nikiendelea na majukumu mengine ya usimamizi wa miradi ya Brother Ally Mpemba.

Baadae nilichokuja kugundua ni kwamba,hakukuwa na fitina za mswahili wala nini,ile hela ambayo nilikuwa nikiipata kila ijumaa ya mwisho wa mwezi kiukweli kila nilipojaribu kuifungulia biashara iligoma kabisa kwasababu ukiachilia mbali biashara hiyo ya viazi,nilifungua duka la nguo za kike pale Tandika na kuna jamaa mmoja kutoka Iringa nilimuajiri aniuzie,ilikuwa ni siri sana na sikutaka mtu yeyote ajue kuhusu hilo,lile duka halikufikisha hata miezi 6 likawa linaporomoka,mtaji na faida havikujulikana vinapotelea wapi,nikajaribu kumchunguza yule bwana mdogo nikadhani uenda akawa ananipiga kumbe haikuwa hivyo,lile duka nikaamua kuliuza na bidhaa baadhi zilizokuwa zimebaki,kwakuwa mwanzo nilipata ugumu kuelewa ila kadiri siku zilivyosonga ndipo akili na ufahamu vikanijia nikafahamu ya kwamba ile hela ilikuwa na matatizo,sasa nilichoamua ni kwamba ile hela niingize kwenye ujenzi wa nyumba yangu nitakayokaa huko Chanika kwenye uwanja wangu(Nitakuja kueleza kilichotokea maana hali ilikuwa mbaya kuliko nilivyodhani).

Sasa kwakuwa nilikuwa na kiasi cha fedha ambacho nilibaki nacho,niliamua kununua ramani ya nyumba na kwenda kuanza ujenzi kwenye uwanja wangu kule Chanika ili ule uwanja usiendelee kuota nyasi,baada ya kupiga msingi na jamvi niliamua kuachia hapo ili niendelee kuvuta nguvu za kupandisha boma.

Sasa kuna siku Ally Mpemba alinipigia simu akawa amenitaka nionane nae pale kwake ili tupange mipango kadhaa kwasababu yeye alikuwa anahitaji kusafiri kama alivyokuwa ameniambia awali,tulikubaliana tungeonana jumapili ya wiki hiyo pale nyumbani kwake kwasababu pia hata mimi jumapili mara nyingi nilikuwa napumzika.

Niliondoka zangu kuelekea kwa Ally na bahati nzuri nilimkuta akiwa nyumbani.


Ally Mpemba "Salama?"

Mimi "Salama kaka"

Baada ya salamu na mazungumzo mafupi,jamaa aliingia ndani ambako alichukua muda mrefu kidogo ndipo akawa ametoka.

Ally Mpemba "Pika chakula ule master,hapa ni kama kwako wala usione taabu!"

Mimi "Kaka usijali niko vizuri"

Ally Mpemba "Ulikula muda gani?"

Mimi "Nimekula muda si mrefu!"

Ally Mpemba "Sawa kama ndivyo"

Aliendelea "Mimi nimekuita weye kwasababu hapo awali nilikueleza ya kwamba nina safari ya kwenda Oman,hivyo nikakuomba unisitiri master!"

Mimi "Sawa kaka"

Ally Mpemba "Kuna jambo nahitaji nikwambie na nakuomba Union unionyeshe uaminifu wako kama nilivyokuamini"

Mimi "Kaka ina maana huniamini tu!"

Ally Mpemba "Mimi nakuamini tangua siku ya kwanza ila nadhani unakumbuka nilikutahadharisha ya kwamba kuna mambo ukiyapayuka kwa watu wengine utakachokutana nacho basi utajua mwenyewe!"

Aliendelea "Ndugu zangu siwathamini kama ninavyo kuthamini weye,hivyo thamani ninayokupatia ni kubwa mno"

Aliendelea "Hivyo mimi naondoka na itanichukua takribani mwezi mmoja huko,nakuomba usimamie shughuli zangu hasa ile niliyokukabidhi huko kwengine Farah atasimamia!"

Mimi "Sawa kaka nimekuelewa!"

Ally Mpemba "Vipi mambo yako lakini yanakwenda?"

Mimi "Yanakwenda kaka"

Ally Mpemba "Sawa jitahidi ufanye vema kama ulivyoambiwa na nakuhakikishia wewe ukiwa mwaminifu hakika utakuwa mkubwa hapa Bara kote na hata huko pwani hakuna atakaye kugusa kwa utajiri!"


Niliendelea kumsikiliza Ally Mpemba namna alivyonitia moyo kuhusu ile bangiri lakini sikutaka kumwambia kabisa kuhusu biashara zangu zote mbili zilivyonipatia hasara ikabidi nikaushe.

Ally Mpemba "Kuna jambo ambalo kabla ya kuondoka naomba ulifahamu maana nilazima ndipo uweze kufanya maamuzi ya kunisitiri"

Aliendelea "Bila shaka Huyu kiumbe ninayeishi naye hapa kwangu unamfahamu!"

Mimi "Ndiyo kaka namfahamu"

Ally Mpemba "Sasa nadhani unaelewa huwa nisipokuwepo nakuomba unisaidie kumwandalia chakula"

Mimi "Ndiyo kaka"

Ally Mpemba "Naomba leo nikueleze ukweli na usije kujaribu kumueleza mtu,mimi na wewe tumekuwa wamoja na siri yako ni yangu na naomba siri yangu iwe yako,huwezi kufanikiwa kama hutaweza kutunza jambo!"

Aliendelea "Huyo unayemuona hapa she's my blood sister,na ndiye mwanamke ninaye mpenda kuliko wanawake wote duniani,jina lake si Maya kama unavyodhani,jina lake ni Zahra,hakuna mtu yeyote anayejua Zahra yuko hapa ila wewe,hivyo nakuomba uwe makini na siei hii na nakuomba sana!"

Kiukweli Ally Mpemba alionyesha hali fulani ya huruma na upole baada ya kumuongelea Maya,nilikuwa nikimuangalia Ally Mpemba alionyesha usoni ni mtu wa huruma sana lakini kiuhalisia hakuwa kama ulivyomdhania.

Ally Mpemba "Nikitoka Oman nitakuja kukueleza vizuri ila nachotaka ujifunze na unisitiri!"

Aliendelea "Oman sina mke kama nilivyokwambia hapo awali ila kuna jambo kubwa ambalo na wewe utalifanya siku moja,nikirudi nitakujuza ila kwasasa nakuomba unisitiri!"

Kiukweli hali haikuwa rahisi kama nilivyodhani ila kwakuwa nilikuwa tayari nishaingia kwenye mfumo wa Ally Mpemba sikuwa na jinsi ilibidi nitekeleze na kufanya nilichoambiwa ili kuendelea kujipatia pesa.


Ally Mpemba "Nitakapoondoka nakuomba kila ijumaa uwe unalala kwenye chumba changu hicho!"

Mimi " Sawa kaka nimekuelewa"

Ally Mpemba "Naomba usiwe unashituka kwasababu Zahra atakuwa anakuja mnalala naye na atakachokuwa anataka umfanyie naomba umfanyie usiogope!"

Mimi "Hawezi kuniletea fujo kaka?"
Ally Mpemba "Hawezi,yeye akishakula huwa hana shida,hakikisha kila ijumaa haufungi mlango wa chumba changu,yeye atakuwa anaingia na mnalala nae kisha akitaka chochote mpatie"

Aliendelea "Bila shaka master wewe ni rijali na kama huwezi kabisa basi mimi kuna dawa nitakupatia utakuwa unakunywa ili uweze kuwa imara kitandani!"

Mimi "Hapana kaka wala usijali niko Imara sana!"

Ally Mpemba "Sawa nitashukuru sana kama umeamua kunisitiri!"

Mimi "Kaka asije akajua mimi siyo wewe akaniletea vurugu!"

Ally Mpemba "Hapana hawezi kufanya hivyo,akishaingia chumbani atalala kitandani na wewe nakuomba usipoteze muda wala usione huruma,mshughulikie kikweli kweli,ikifika asubuhi ataamka mwenyewe ataondoka chumbani kwake!"

Mimi "Sawa kaka nimekuelewa!"

Ally Mpemba "Japo anayo harufu ila nakuomba usionyeshe hali ya kujuta maana hiyo harufu ndiyo pesa yenyewe!"

Aliendelea "Ukifanya vema utapata zaidi na utakuwa mkubwa sana"

Mimi "Sawa kaka nimekuelewa kabisa na sitokuangusha"

Ally Mpemba "Usije kuruhusu mtu yeyote kuingia humu ndani zaidi yako!"

Mimi "Sawa"


Ally Mpemba "Sasa jiandae kesho twende pale TRA ukachukue TIN,kuna jamaa pale nishampa hela nitamkabidhi kwako akufanyie mchakato wa leseni ya gari!"

Basi baada ya yale mazungumzo Ally Mpemba alinikabidhi laki 5 kisha akaniambia kesho asubuhi mida ya 2 tuonane ili tuelekee TRA kwa ajili ya ishu ya leseni.Kiukweli nilibaki kushangaa namna Ally Mpemba alivyokuwa na ujasiri wa kulala na dada yake kitanda kimoja na kumuingilia kimwili.Haikuwa kazi ndogo ila niliamua kupiga moyo konde kwasababu nilikuwa ninataka pesa na mimi niliamua kuwa na roho ngumu.

Baada ya siku tatu kufatilia masuala ya leseni,namshukuru Mungu nilijipatia leseni yangu ya kwanza kabisa kwa ajili ya uendeshaji wa gari.Nilipopata leseni Ally Mpemba alinipatia ile gari yake iliyokuwa mpya aina ya Aud A4,kiukweli nilipata kiburi sana kwa kujiona mimi ndiye mimi,sasa kabla Ally hajaondoka kuelekea Oman alinipatia maelekezo namna ya kuimiliki ile gari.

Ally Mpemba "Master nakuomba tu kwenye hii gari mpya ninayokukabidhi ukiamua kuwabeba marafiki zako basi wakae viti vya nyuma,hii siti ya mbele asije akaikalia mtu yeyote labda kama akitokea ndugu yangu,tafadhali sana nakuomba!"

Mimi "Ndugu zako siwafahamu kaka zaidi ya mama yako mdogo pamoja na Farah"

Ally Mpemba "Hao ndiyo ninao maanisha,kama Farah akikuona na akihitaji lift usiache kumbeba na asikae nyuma bali akae kiti cha mbele,wengine wote usithubutu kuwabeba mbele"

Mimi "Nimekuelewa kaka nitakuwa muangalifu!"

Ally Mpemba "Sawa mimi nadhani Alhamisi ijayo naondoka,hakikisha jumatano utakuja kulala hapa ili nikiwa naondoka kuna pesa nikukabidhi pia nikukabidhi na funguo"

Mimi "Utachukua muda mrefu huko?"

Ally Mpemba "Haitapungua mwezi!"

Mimi "Sawa kaka"

Baada ya kuniambia niwe muangalifu na ile siti ya mbele nilivuta picha lakini sikupata majibu,lakini nikakumbuka mara zote nimekuwa nikimuona na ile range akiwa amebeba mtu basi uishia kukaa nyuma na siti ya mbele hukaa bila mtu na mimi pia mara zote nimekuwa nikipanda ile Range ndivyo ilivyokuwa!.

Kweli,baada ya siku kufika Ally Mpemba aliondoka akawa amenikabidhi funguo za nyumba yake pamoja na kiasi cha shilingi milioni 3 na akawa ameniambia amempatia Farah maelekezo endapo zikiisha nimuone atanipatia nyingine,pesa aliyonipatia ilikuwa ya matumizi ya kawaida ya kununulia vyakula vya Maya pamoja na matumizi yangu.Nilifurahi sana maana niliona kila kitu sasa kipo mikononi mwangu na nilipanga kiukweli marafiki na ndugu wanitambue mimi ni nani kupitia lile Audi A4.

Baada ya Ally Mpemba Kuondoka hiyo Alhamisi,ilipofika ijumaa kama kawaida nilienda zangu kazini pale Kkoo kusajili line za simu,ilipofika mida ya saa 10 jioni nilimuaga Farah nikamwambia nitawahi kufunga kuna mahali nawahi.

Farah "Mbona mapema leo!"

Mimi "Kuna mahali nawahi Aunt!"

Farah "Sawa,siunarudi lakini au ndiyo hadi kesho!"

Mimi "Hiyo hadi kesho dada"

Niliondoka zangu nikaenda kununua vyakula vya maya kama kawaida kisha nikaelekea nyumbani kwa Ally Mpemba,nilipofika kama kawaida nilichukua kitambaa kile cheupe nikatandika pale mezani kisha nikaweka vile vyakula,baada ya kuweka vile vyakula nilifunga mlango kisha nikawasha mchuma nikatoka zangu kuelekea kupata chakula ili niwahi kurudi kufungua kile chumba cha Maya.

Nilipomaliza nilirudi mdogo mdogo na ile gari huku nikiendesha kwa madaha kama yangu vile,ilipofika mida ya saa 1 usiku niliwasha taa kisha nikawa nimetoka zangu nje,kiukweli sikutaka kabisa kumuangalia Maya,nilichoamua ni kwenda kuzurura na ikifika mida ya 3 usiku nirudi kulala.Kweli,niliporudi nyumbani kwa Ally Mpemba kama kawaida niliingia chumbani kwake nikawasha taa na sikufunga mlango,kile chumba kilikuwa ni kizuri na kisafi kupita mfano,sikutaka kabisa kuzima taa,niliingia bafuni kuoga kisha nikarudi kujitupa kitandani kulala huku nikiendelea kumsubiri Zahra(Maya)niliyeambiwa na Ally ya kwamba nikiacha chumba wazi ataingia mwenyewe.

Kweli,haikupita hata nusu saa nilimuona Zahra akiingia chumbani akiwa uchi kama ambavyo siku zote huwa.



Itaendelea................
Makubwa haya jamani, hii hadithi au watu wanayafanya haya? Kama ni hivi basi mwengine tupo kwenye giza nene ila kwa YESU nuru ipo [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
 
Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani - 17.





Nikiwa njiani naelekea kwake alinipigia simu akinitaka nipitie pale Big Bon nimsubiri atoke msikitini kisha tuandamane nae hadi kwake.Baada ya muda kupita Ally Mpemba alirudi kutoka msikitini na aliniambia nipande gari yake kisha tuondoke.

Ally Mpemba "Swalama master"

Mimi "Mimi niko poa kaka"

Ally Mpemba "Usiogope mdogo wangu haya ni mambo ya kawaida sana hapa mjini!"

Aliendelea "Wewe nakuona utakuwa mtu mkubwa sana "

Mimi "Kweli kaka?"

Ally Mpemba "Wewe tulia tu utajionea"

Tulipofika kwake nilitelemka kwenye gari na kwenda kufungua geti kisha akaingiza gari ndani.

Sasa tulipofika ndani mimi nilikaa pale sebuleni halafu Ally Mpemba yeye akawa amepitiliza moja kwa moja kuingia chumbani kwake,ilipofika mida ya saa 10 Alasiri nikiwa nimekaa pale sebuleni nikisubiri animbie alichoniitia,ndipo nikahisi mkononi nimeanza kubanwa na ile bangiri;Ilibana kwa nguvu huku damu ikaanza kunitoka kwenye mkono ambayo haikuwa nyingi sana,ilipoendelea kubana sana hadi kuihisi maumivu nilichomoa kile kichupa kidogo cha Gliselin kilichokuwa na ule mchanganyiko wa damu na dawa nikaanza kuipaka ile bangiri,baada ya dakika 2 hivi ndipo nikahisi ile hali ya kubana inaachia.Kiukweli baada ya lile tukio nilijisikia mwepesi kupita maelezo,kila jambo mbele yangu niliona halina kizuizi chochote.

Nikiwa naendelea kumsubiri Ally Mpemba pale sebuleni nilisikia ule mlango wake ukifunguliwa na ndipo kutazama nikidhani ningemuona Ally Mpemba haikuwa hivyo,alikuwa ni yule kiumbe wa ajabu akitoka ndani ya kile chumba akirudi kwenye chumba chake,sikuelewa alichokuwa amefata ni nini kwenye kile chumba na alionekana kama kushangaa sana!.

Baada ya muda Ally Mpemba nae alitoka ndani kisha akakifunga kile chumba.Sikujua yule kiumbe alipita muda gani kuingia kwenye chumba cha Ally Mpemba wakati nikiwa pale sebuleni kwasababu ile nyumba namna ilivyokuwa imekaa,ilikuwa rahisi mtu akitoka au kuingia chumbani kuonekana,yawezekana alikuwa chumbani kwa Ally Mpemba muda mrefu na Ally Mpemba alipofungua chumba basi alimwambia aondoke aelekee chumbani kwake kulikokuwa na shimo chini ya kabati.

Lakini kilichonishangaza zaidi ni muda Ally Mpemba aliotumia alipoingia chumbani,tulifika hapo nyumbani kwa Ally mida ya saa 8 mchana baada ya kutoka Kkoo,mimi niliendelea kukaa pale sebuleni hadi mida ya saa 10 alasiri ndipo kubwana na ile bangiri ambayo niliambiwa ni Alfwat anakula;kuna masaa kama mawili Ally Mpemba alikuwa chumbani kwake na yule kiumbe ambaye hadi wakati huo nilikuwa simuogopi baada ya kuzoea yale mazingira na kuhakikishiwa na Ally Mpemba usalama wangu wa Kimwili na Kiroho.


Ally Mpemba "Vipi zoezi lako limekamilika?"

Mimi "Ndiyo kaka "

Ally Mpemba "wewe ni muaminifu sana na ndiyo maana nakupenda sana!"

Aliendelea "Kama nilivyokwambia,wewe utakuwa mtu mkubwa sana kwasababu huogopi kuyatafuta mafanikio"

Aliendelea "wabongo wengi hawafanikiwi kwasababu wanadhani mafanikio hujileta tu kwa kupiga blah blah,mafanikio yanatafutwa kwa nguvu isiyokuwa ya kawaida master"

Aliendelea "Nitakusapoti mwanangu kwakuwa na wewe umenisapoti na umeonyesha uaminifu kwangu tangu nilipokuamini,sikukosea kukuchagua uwe rafiki yangu!"

Aliendelea "Kwasasa hizi ni hatua za awali tu ila nakuona mbali sana,ukiendelea hivi sidhani kama nitakusogelea kwa pesa master"


Kiukweli maneno ya Ally Mpemba yalinichochea sana hadi kuwaza kufanya mambo makubwa ili nipate pesa na mimi niwe mtu maarufu mjini na niendeshe magari ya gharama kama watu wengine.

Baada ya maongezi yale na Ally Mpemba nilimuuliza uenda kulikuwa na ishu yoyote alitaka kuniambia ili niweze kurudi nyumbani mapema.

Ally Mpemba "Hivi unaweza kuendesha gari?"

Mimi "Ndiyo kaka naweza japo sina leseni!"

Ally Mpemba "Ulijifunzia wapi gari master wewe!"

Mimi "Kaka wala sikwenda chuo kujifunza bali kuna mahali nilikuwa napewa kusogeza kidogo tu hadi nikafahamu kimtindo!"

Ally Mpemba "Kwahiyo unaweza kusogeza kimtindo?"

Mimi "Ndiyo kaka!"

Ally Mpemba "Ulikuwa muosha magari nini!"

Mimi "Kwanini kaka?"

Ally Mpemba "Nimeuliza tu maana jamaa wao ndiyo huwa wanaweza kusogeza kimtindo lakini kuendesha kwao ni changamoto!"

Mimi "Hapana kaka,mimi nilijua kusogeza gari miaka fulani nilikuwa mpiga debe"

Ally Mpemba "Duuuu ushawahi kuwa mpiga debe?"

Mimi "Ndiyo kaka!"

Ally Mpemba "Basi kama ndivyo wewe ni faita,kumbe nakuchukulia poa eeeh!"

Mimi "Kawaida tu kaka ni moja ya utafutaji!"

Ally Mpemba "Ok,sasa itabidi nikusajilie ile gari Aud ili uwe unatembelea miradi yangu pamoja na kufanya ishu zako ziwe rahisi!"

Mimi "Kweli kaka?"

Ally Mpemba "Sijawahi kuongopa na ninachoamini wewe unakuja kuwa mkubwa zaidi yangu,jambo la msingi ni kunitunzia siri vinginevyo tusije tukalaumiana!"

Mimi "Kaka kwa hilo tu usijali "

Ally Mpemba "Hapa kwangu umewahi kumuona mtu mwingine zaidi yako kwa muda huu tu ambao nimefahamiana na wewe?"

Mimi "Hapana kaka sijawahi kumuona mtu yeyote!"

Ally Mpemba "Ok,je umewahi kumuona ndugu yangu yeyote hapa kwangu kwa wale unaowafahamu?"

Mimi "Hapana kaka"

Ally Mpemba "Ok uwe unajiuliza kwa nini wewe ninakupa kipaumbele kuliko ndugu zangu!"

Aliendelea "Wewe ni mtu muhimu sana kwangu hivyo usije ukafanya nikakosa uamimifu kwako itakuwa ni mbaya sana katika maisha yako!"

Mimi "Sawa kaka sitokuangusha"

Ally Mpemba "Hivi karibuni nataka kufanya safari ya Oman ila kabla ya kuondoka nitaomba uwe unanisitiri kwa kipindi chote ambacho sitokuwepo!"

Mimi "wala usijali kaka wewe ushakuwa zaidi ya ndugu!"


Sasa baada ya kusikia jamaa anataka kunipatia ile Aud mpya niwe natembelea,kiukweli nilikuwa nina furaha ya ajabu na nilijikuta nawaza mambo mengi sana na jambo ambalo lilikuwa la kwanza kichwani mwangu baada ya kupata ile gari,safari ya kwanza ingekuwa kwa mjomba Nico kule Ununio ili niende nikaonyeshe taizi la nguvu na kuonyesha sikuhizi niko Matawi ya juu,pili nilipanga niwe naingia nalo pale ofisini buguruni kuwalingishia wale mademu waliokuwa na nyodo na kuniona mimi mshamba!.Kiukweli niliona kama jamaa ananicheleweshea ile mashine na ndiyo maana ilifikia wakati kila jambo alilokuwa akiniambia nilikuwa nikimjibu kwa haraka haraka bila kujiuliza mara mbili mbili madhara ya kile kitu alichokuwa ananiambia.

Ally Mpemba "Unajua maana ya kunisitiri lakini master?"

Mimi "Kaka sitoweza kupayuka kwa watu na kama nikifanya hivyo wewe nifanye unavyoweza"

Ally Mpemba "Mimi simaanishi hivyo master,siyo kwamba sikuamini kwamba wewe ni msiri ila nahitaji uwe unanisitiri kwa kipindi chote hicho ambacho sitokuwepo"

Mimi "Kaka kukusitiri kiaje?"

Ally Mpemba "Umefanya vema kuniuliza na mimi nilisubiri swali lako sema ulikuwa unazunguka!"

Aliendelea "Nadhani wewe waweza kuondoka halafu mambo mengine nitayashughulikia mimi"

Mimi "Kaka hujaniambia lakini kuhusu kusitiri "

Ally Mpemba "Nitakujuza tu wala usijali,siku ya kuondoka nadhani gari nayo itakuwa tayari hivyo nitakujuza"


Mimi "Sawa kaka,basi mimi ngoja niwahi usafiri wetu wa kugombania"

Ally Mpemba "Nisubiri kidogo nakuja"


Baada ya kuniambia nimsubiri,aliingia chumbani ambako hakuchukua muda akawa ametoka na kiasi fulani cha pesa na kunikabidhi nikitumie kama nauli.

Mimi "Nashukuru sana kaka!"

Ally Mpemba "Hupaswi kunishukuru,mimi ndiyo napaswa kukushukuru!"

Niliondoka zangu mle ndani kuelekea nje kisha nikaanza kuhesabu zile hela nikakuta ilikuwa laki 2,kiukweli nilifurahi sana kimoyo moyo na kujiona ni mtu mwenye bahati sana kuwa na urafiki na Ally Mpemba mwenye asili ya arabuni.

Nilipanda zangu gari za gongo la mboto zilizokuwa zinatokea maeneo ya Morocco,ingawaje zilikuwa zimejaa lakini hakukuwa na namna,nilichowaza mimi nikufika nyumbani sikuwaza uwingi wa abiria.Baada ya kufika nyumbani mida ya saa 12 jioni nilifungua mlango na kuingia ndani,nilipofika sebuleni kwangu niliwasha taa kisha nikawa naelekea chumbani,kama nilivyosema hapo awali ya kwamba,nikuwa nimepanga kwenye nyumba ya vyumba viwili,hivyo kulikuwa na chumba na sebule,ndani kwangu kulikuwa na kila kitu ambacho kijana wa kisasa angetamani kuwa nacho.

Baada ya kufungua chumba na kuingia ndani niliwasha taa,sasa nilipowasha taa kuna hela ambazo zilikuwa mpya noti za shilingi elfu kumi kumi nilizikuta pale kitandani,kiukweli nilishangaa sana zile hela na sikujua ni nani alikuwa ameziweka hapo kitandani,nilidhani uenda ile asubuhi wakati natoka nilizisahau pale kitandani lakini bado haikuingia hakilini kwasababu sikuwa na hela yeyote hapo ndani kwa wakati huo.Niliamua kusogea na kuzikamata zile hela na kuanza kuzihesabu moja baada ya nyingine,sasa wakati nahesabu zile hela nikawa nasikia kuna mtu anagonga mlango!.

Nilitoka chumbani kwenda kuufungua ule mlango,baada ya kuufungua ule mlango kumbe alikuwa ni yule demu wake na Steve.

Zuu "Shem mambo"

Mimi "poa,mambo vipi?"

Zuu "Safi,niazime simu yako nimpigie Steve maana kwangu sina salio!"

Mimi "Ok ngoja nikuletee"

Niliingia ndani nikachukua simu kisha nikampigia simu Steve baada ya kumpata nikampa aongee na demu wake kisha mimi nikarudi chumbani kwenda kuendelea kuhesabu zile hela,nilipokuwa nikiendelea kuhesabu zile hela,demu wa jamaa aliniita niende nikachukue simu,sasa nilipofika nilikuta bado simu haijakata na ndipo akaniambia Steve anaomba kuongea na mimi.

Mimi "Mwanangu niambie!"

Steve "Mwanangu naomba umuazime shemeji yako gesi yako apikie maana kwangu imeisha,nikirudi nakuja kuchukua kaka"

Mimi "Usijali kaka ngoja nimpatie hela akabadili mtungi halafu wewe utanirudishia!"

Steve "Utakuwa umenisaidia sana mwanangu"

Baada ya kuelewana na Steve,niliingia ndani nikachukua elfu 50 kwenye zile hela ambazo Ally Mpemba alinipatia kama nauli nikawa nimempatia demu wa jamaa ili akabadili mtungi wa gesi,baada ya kumpatia mimi nilirudi ndani kuendelea na zoezi la kuhesabu zile hela,baada ya kumaliza kuzihesabu jumla yake zilikuwa milioni 5,kiukweli nilifurahi sana na nikaona mambo yangu yanazidi kunyooka tu bila kutumia nguvu nyingi.Sasa mpango wangu ulikuwa ni kwamba,nichukue zile hela niongezee na ambazo nilikuwa nimedunduliza benki ili nianze kufanya biashara ya viazi mbatata kutoka Mbeya na niachane na mambo ya kusajili line za simu.
Kwakuwa dhamira yangu ilikuwa kuwa mfanyabiashara mkubwa wa viazi mbatata hivyo nikaona nianze kutengeneza koneksheni ya madalali pale soko la Ilala na Mabibo ili kuweza kulifahamu na kuliteka soko,sasa baada ya kujiridhisha bei ya soko nikaona nichukue kale ka hela kangu nilikokuwa nimedunduliza benki pamoja na ile hela niliyoikuta pale kitandani kisha nikapata milioni 7.

Niliamua kumpigia simu team leader na kumdanganya kwamba naelekea nyumbani kulikuwa na matatizo huku lengo langu ni kuelekea mkoani Mbeya kukusanya viazi mbatata na kuvileta mjini ili nipige pesa,lengo la kumuaga team leader ni asiendelee kuniona mzembe katika kazi ile ya kusajili line ili kuendelea kuweka uaminifu asije kuninyang'anya kodi akampatia mtu mwingine,nilitaka ile kazi niiache mdogo mdogo bila kuondoka kwa dharau maana nilichoamini ni kwamba maisha hubadilika.

Niliianza safari ya kuelekea Mbeya kwenda kukusanya viazi na kuvileta mjini.



Itaendelea .............
Duu hapo unaanza kusanya bila jasho
 
Miaka hiyo, jeuri ya kulinunua gazeti hilo, wengi tulikuwa hatuna! Sasa kuna "aliyekuwa" classmate pale Azimio Primary School Mbeya mjini, baba yake alikuwa ni mfanyabiasha ya usafirishaji (mabasi),basi yeye ananunua magazeti mawili, moja lake, lingine linazunguka darasa zima.
Wakati mwingine, linahamia madarasa mengine! Ile michoro ya akina Kipepe ilikuwa inatuburudisha sana!
Kero, ilikuwa kulisubiri kama miendelezo ya simulizi hizi za UMUGHAKA !
Aisee Ni kweli watoto wa matajiri tu ndio walikuwa nayo hayo,nilikuwa napenda Sana simulizi ya Pablo Escobar Sasa muendelezo ilikuwa inatakiwa kuwa mvumilivu😂.....Haki tumetoka mbali
 
Sehemu ya 18

Nikiwa ndani niliendelea kuwaza juu ya mambo aliyokuwa ameniambia bwana ally mpemba.

Swala la Kwanza ni juu ya kuniachia gari yake aina ya Audi, hapa niliona ni fursa kwasababu ningetumia kuwaringishia maboya kama Chizi Maarifa, na kuwanasa watoto wazuri Kama Antonnia, na To yeye .

Ila swala la kumstiri ndilo lilizidi kuniumiza kichwa??, Nikawaza namstiri wapi, au anadaiwa mikopo ya kausha damu, hivyo anaomba nimlipie🤔🤔

Yajayo yanafurahisha
Aisee,mi kwenye uzuri nitoe sifikii hata a half...em niambie kwanza ...kutunga hadithi umeanza lini
 
Back
Top Bottom