Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani

Umempopoa[emoji23]
 
Utajiri wa rafiki yangu ulivyonifanya nikamuamini shetani - 20

Hakika nilishangaa sana kwanza inawezekanaje Dada yake Ally Mpemba (Aunt) awe amefanana kila kitu na Zahra/Maya, kwa kua rangi, nywele na ule mchoro pale mkononi isipokua tu Maya alikua na muonekano wa tofauti sana kutokana na yale mazingira ya ajabu aliyokua akiishi. Nikiwa naendelea kutafakari ghafla nikashtushwa na sauti ya Aunt akiwa tayari ndani ya ile Audi A4 ili niende nae kule Magoneni kwa kaka yake Ally Mpemba ili akachukue ile gari nyingine (Range ambayo ilikua mle ndani).

Sasa kama mnakumbuka vizuri moja ya maelezo aliyonipa Ally Mpemba ni kwamba hakuwahi kumleta ndugu yake yeyote pale Magomeni anapoishi lakini kwa kua niliongea nae mimi mwenyewe kwenye simu aliyonipatia dada yake kipindi nimefika pale nyumbani Gongo la mboto ndipo nikaamini na kuondoa wasiwasi nilikua nao kuhusu kufimfikisha dada yake pale nyumbani kwake.

Nakumbuka mida ya saa 11 nikawa nimefika pale nyumbani kwa Ally nikiwa dada yake (Aunt Farah), nikashuka nikaenda kufungua geti alafu nikaingiza gari ndani, Kiukweli kwa wakati huo ukinitazama nilikua ninapendeza sana ukilinginisha na kipindi kile nilipotoka kwa yule binamu yangu Kileri, na kiukweli ukinitazama ungeweza kudhani kua lile gari ninalotembelea ni la kwangu yaani nililonunua kwa pesa yangu, lakini pia kwa muonekano wa nje wa ile nyumba ya Ally Mpemba ni wazi kua ilikua inaendana na hadhi ya ule muonekano wangu.

Basi baada ya kuingia ndani ya ile nyumba (ndani ya fence) Farah hakuonekana kuyashangaa yale mazingira japokua kaka yake alinieleza kua hakuna ndugu yake yeyote aliyewahi kufika hapo, kutokana na zile funguo za gari kua ndani ya nyumba ile ilinilazimu mimi na Aunt Farah kuingie mle ndani, lakini baada ya kufungua mlango wa hapo sebuleni ambapo ndipo mlango mkuu ulipo kuna kitu kikanishangaza.

Hakika nilishangaa sana baada ya kukuta Runinga ikiwa imewashwa na kukuta kile kitambaa cheupe kikiwa pale juu ya ile meza ambayo hua tunaitumia kuweka mboga za majani na yale makabichi makubwa kwaajili ya chakula cha Maya, ile hali kwa kweli nilianza kuogopa ila kutokana nilikua na Aunt Farah nikakausha na kujifanya nina hali ya kawaida ili Aunt Farah asigundue chochote.

Nikamkaribisha Aunt Farah ndani na kumueleza anisubiri pale sebuleni ili nikamfuatie funguo ambayo ilikua mle ndani kwenye chumba cha Ally mpemba, lakini kabla sijakifikia chumbani kuna jambo lingine lilonishangaza zaidi baada ya kukuta chumba cha Maya kikiwa wazi na wakati kwa kumbukumbu zangu nilikifunga ile asubuhi baada ya kumpa shoo nzito yule Maya/Zahra, hakika nilizidi kuogopa lakini nilijikaza na kuamini kila kitu kitakua sawa kwa wakati ule, basi nikausogelea ule mlango wa Maya/Zahra na kuufunga, tofauti na siku zote kile chumba na Maya/Zahra kilikua na marashi yanayonukia sana.

Baada ya kuufunga ule mlango wa Chumba cha Maya nikaingia chumbani kwa Ally Mpemba kwa haraka sana ili nimpatie Aunt Farah zile funguo za ile gari (Range) aliyotaka kuondoka nayo, kama maagizo niliyoyapata kutoka kwa Ally Mpemba, nikafungua droo na kuchukua ile funguo lakini ile nageuka tu, nikakutana uso kwa uso na Aunt Farah ambaye nilimuacha pale sebuleni lakini akiwa katika muonekano mwingine, akiwa kaziachia nywele zake na taulo kama mtu aliyetoka kuoga..

Maswali niliyokua najiuliza je aliingiaje mle ndani mpaka akapata wakati wa kuoga ikiwa funguo nilikua nazo mimi kabla ya kuufungua mlango?


Itaendeleeeea.........
 
Mmmmmmh endeleza umughaka akija akute imeisha
 
TANGAZO

Umughaka alipata Dharura, hakuwa mjini ila sasahivi yupo njiani anarudi DAR na ataendelea na Story kesho. kuweni na Subira msipende kuhukumu Binadamu hatuna Guarantee ya kesho yetu.
Dharura wakati yupo 24/7 online acha undezi wewe endelea kuwa Mnyonge na ukafagie Kaburi huko Chato kwa kiongozi wenu Uchwala...
Tena usilete shobo wengine hatuna nidhamu ya lugha kwa watu kama wewe
 
Kumbe story unayo afu uko kimya? Endelea basi
 
Naam [emoji91]
 
TANGAZO

Umughaka alipata Dharura, hakuwa mjini ila sasahivi yupo njiani anarudi DAR na ataendelea na Story kesho. kuweni na Subira msipende kuhukumu Binadamu hatuna Guarantee ya kesho yetu.
Aandike kwanza akishamaliza ndo aweke sio unaandika ki-episode kimoja afu unasema una dharula,kwani hakujua km huwa Kuna dharula?mbona kutwa anaonekana active humu jf?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…