Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani

Mke au demu ni ngumu sana kumwambia akae siti ya nyuma kwanza huwa hawakubali, angalau msela anaweza kukubali ,njia peke ya kumweka mwanamke siti ya nyuma gari ikiwa tupu ni kuondoa kabisa siti ya mbele tafuta spana uifungue hiyo siti
 
sehemu ya 23:

Basi bana baada ya kununua zile chupi niliamua niende tu nyumbani kwangu Gongo la mboto maana kipozeo changu Rehema ndio hivyo tena anakwenda kuliwa kichwa na majini ya Ally Mpemba.

Niliamua kupanda daladala maana sikuwa na ujasiri wa kwenda kule magomeni kwa Ally kuchukua ile audi ukizingatia hata chumba cha lile limsukule la kiarabu kilikuwa kiko wazi hivyo niliota itakuwa hatari sana kurudi pale bila kwanza kumaliza hili swala

Nilipokuwa njiani kwenda Gongo la Mboto nilipokea simu moja kwa moja kutoka kwa bro Ally akiniuliza mbona nimekawia sana kumpatia Rehema huo mzigo maana eti Maya hataweza kula mpaka kwanza awe ameinywa damu ya Rehema

Du! Nikabaki nimeduwaa nisijue cha kufanya,halafu kumbe wakati ninaongea na Ally nilikuwa nimeweka loudspeaker hivyo mazungumzo yote abiria wenzangu walikuwa wanayasikia live kabisa bila chenga.Hata sijui kwa nini niliweka loudspeaker au labda kwa sababu nilikuwa nishazoea kujiachia kwenye lile liAudi la kaka Ally muarabu wa Pemba

Basi baada ya kumaliza kuzungumza na Ally,gari zima walikuwa wamenitolea macho mimi huku wakionekana kuwa na wasiwasi sana na Mimi,tena walikuwa wakinongonezana nongonezana kwa sauti za taratibu sana ambazo ilikuwa vigumu kuzisikia lakini nilihisi neno makafara,Freemason na ushirikina yalikuwa yakitajwa tajwa kwenye minongono yao

Basi bwana,kulingana maelezo ya bro Ally kuwa damu ya Rehema inahitajika haraka sana ili Maya aweze kurudi katika hali yake ya kawaida niliamua nikifika nyumbani nioge fasta kisha niwahi nyumbani kwa Rehema nimkabidhi hii michupi yake ili mambo yarudi kama yalivyokuwa maana umaskini sio kitu kizuri aisee,yani siku mbili tu za kukosa usafiri wangu nimepoteza zaidi ya kilo 8 na usheee.

Nilipofika nyumbani nilienda moja kwa moja kufungua mlango wa nyumbani yangu ila nilipatwa na mshangao wa mwaka sana kwa yale niliyokuwa nikiyaona

Nilikuta zile kabechi na mimboga mingine ya majani ninayomuwekea Maya pale sebuleni kwa maya ikiwa imemwagwa kwenye meza yangu ya hapa sebuleni

Kiukweli sikujua hii mimboga imefikaje fikaje hapa ila kabla hata sijajua nifanye nini simu kutoka kwa bro Ally ikawa imeingia.Kama kawaida yake akaongea kwa lafudhi ya kipemba akisema"aisee masta hizo kabechi hapo sebuleni kwako ndio chakula chako cha siku nzima na usithubutu kula chakula kingine chochote kabla ya Rehema hajatwaliwa maana tutampoteza maya "

Sekunde kumi tu baada ya Ally kukata simu nikawa nimepokea simu kutoka namba ngeni ya Tigo,kabla hata ya mpigaji hajajitambulisha kwangu akawa anaongea mfululizo kuwa Rehema amekutwa akiwa amejinyonga chumbani kwake na kaacha barua akisema chanzo no mimi UMUGHAKA hivyo nahitajika kituo cha polisi haraka

Punde tu baada ya simu hii kukatika ikaingia simu nyingine ambayo mpogaji kabla hajasema chochote alijitambulisha kwamba anaitwa maya ama Farah ananiomba nifike nyumbani kwake ndani ya nusu SAA

Nilijikita nimeganda kama sanamu nisijue kipi cha kufanya ila kabla hata sijaamua chochote simu kutoka kwa Ally ikawa tena imeingia


Itaendelea.........


Majobless kujeni sasa akina Allency na wenzako
 
🚮
 
Acha mambp yako basi. Unatuchanganya na muendelezo wako ambao hatahauna ule utamu wa umughaka
 
wewe ni rainbow mbwa ww
 
safi sana kazi iendelee mkuu wapinzani wametuchelewesha sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…