Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani

Sema kitu nimejifunza kwenye hii hadithi ni kuwa makini na watu wapya , connection za watu wapya , marafiki msiofanana kipato na uchumi muda mwingine ni kuwa nao makini sana, mtu analeta mazoea anajifanya anakubali harakati zako kumbe lengo akutumie kwenye issue zake kama Omughaka
 
Mwanamke ni shetani mpaka shetani mwenyewe anamuogopa

Wanawake wakiacha ujinga na umbulula wanaweza kuiteka dunia tena pasipo kutumia mabomu

Pamoja na Umughaka kuwa na tamaa ya kupata utajiri lakini kaamua kupoteza kila kitu kwasababu ya mwanamke mwenye shape lake matata
 
Yeah ni kweli kabisa. Lakini pia kuna somo kwamba kama una siri inayokupa maendeleo/mafanikio usidiriki kumwambia mtu yeyote Hata ajioneshe kuwa mwaminifu kiasi gani maana hawawezi kuitunza hiyo siri kama unavyoweza kuitunza wewe
 
Njoo Pm uniambie maeneo unaona hayapo sawa nikufafanunulie mkuu
nashukuru ndugu, ila sababu zangu binafsi mara nyingi huwa sizisemi adi tujuane na kafahamiana kwelikweli. migogoro pia huanza na maneno.

Kiufupi mimi ni wa kizazi niliyelekewa na wazazi wa aina ilee.

asante sana.
 
We jamaa SALUTE kwako
 
@lubawa njoo huku kaka
 
Mkuu hukusoma vizuri ..... Alisema baada ya kuweka zile mboga alipotoka kwenda kulala alisikia sauti ya ajabu ya mnyama mfano wa nguruwe, na hapo kwenye nguvu hakusema alisukumwa na nguvu za ajabu ila alisema alisukumwa na kiumbe chenye nguvu za ajabu ndo baadaye alikuja kugundua kumbe ni msukule.
 
Hii inaonesha kuwa wewe ndiye jobless unapata wapi muda wa kuandika ma-nsha mareeeeefu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…