Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 16,464
- 35,629
Nimepita tena hapa kwenye huu Mgahawa wa Ally Mpemba nimejiuliza maswali mengi sana bila majibu hivi kwa Mgahawa ule tu kila baada ya miezi sita anakufa Mfanyakazi. je huyu Ally Mpemba angekuwa anamiliki Hotel kama Kilimanjaro Hotel, Serena, Sea Cliff au Golden Tulip angekuwa anauwa Wafanyakazi wangapi kwa mwaka? Vijana wenzangu kuna maswali mengi sana ya kujiuliza kuhusu hii pesa, sometimes turidhike na kile tulichojaaliwa na wala tusiishi maisha ya kumuiga mtu fulani kuna watu wanafanya madhambi makubwa sana nyuma ya pazia kwa sababu ya pesa.