Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani

Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani

Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani - 27.



Nilifanikiwa kufika Sumbawanga na ilikuwa ni Safari iliyochukua takribani siku siku mbili kwasababu nakumbuka tulipofika Mbeya tulilala pale halafu kesho yake tukaianza tena safari, nilipofika Sumbawanga sikutaka kupoteza muda nilitafuta gari zilizokuwa zinaelekea Namanyere nikawa nimekata tiketi,muda ulipowadia tuliondoka.

Nilifanikiwa kufika kwa yule mtaalamu niliyekuwa nimeelekezwa kwake,alinipokea na nikawa nimeambiwa nisubiri kwanza amalize kuwatibu watu kadhaa niliowakuta pale;Zamu yangu ilipofika aliiniita nikawa nimeingia ndani ambako alikuwa akifanyia shughuli zake za uaguzi.Sasa alinipatia kigoda nikawa nimekalia na akaniambia nitulie nisizungumue jambo lolote,alianza kuhesabu tudude fulani kama tumawe kisha akawa ananiambia.

Mganga "Hadi sasa uko hai inabidi ushukuru Mizimu kukulinda"

Aliendelea "Naangalia namna ulivyotupiwa jini linaloendelea kukutesa na inapaswa ufe,kuna sehemu ulienda ukatengenezwa ndiyo imesaidia"

Aliendelea "Mtu uliyemuamini ndiye kafanya yote haya"

Mganga "Huyu mtu ni nani kwako?"

Mimi "Ni rafiki yangu tu"

Mganga " Kwanini unaishi na rafiki ambaye anakufanyia mambo mabaya namna hii?"

Aliendelea " Huyu mtu ni hatari sana kwako"

Aliendelea "Huyu mtu anafuga jini ambalo ndilo limekuhangaisha na kwakuwa ulikuwa kwenye himaya yake alikuwa anakufanya anavyotaka!"

Aliendelea "Ndiyo maana nasema Uishukuru Mizimu yako kwasababu alikuwa amekutegeshea Jini hilo likuangamize kabisa"

Baada ya kuniambia maneno hayo ndipo sasa akaniambia nizingumze ninachokitaka.

Mimi "Nimekuja unisaidie maana hali yangu si nzuri "

Mganga "Nitakusaidia ondoa shaka ila inabidi kuna vitu ununue niweze kukutengeneza vizuri"

Basi akawa ameniambia nikanunue vitu kadhaa ambavyo vitahusika katika matibabu yangu,mimi nilitoa fedha na vitu hivyo vikaenda kununuliwa na mtu ambaye alimtuma yeye.Baada ya kununuliwa vitu hivyo nilianza matibabu na matibabu yenyewe nakumbuka kuna mengine yalifanyika makaburini akiwa ameniambia ni kuzika mikosi yote na uchawi wote ule wa Ki-Unguja(Chumbe).

Nilikaa kwa yule mtaalamu takribani wiki 2 na baada ya kuwa amekamilisha zoezi la matibabu,kuna dawa kadhaa alinipatia ambazo aliniambia nitazitumia nikapafika Dar es salaam.Niliondoka nikawa nimerudi Dar es salaam na sikutakiwa kabisa kumsogelea Ally Mpemba hata kidogo,nakumbuka maisha yalianza kuwa magumu sana tena kwa upande wangu,kwakuwa nilishazoea kupambana sikutaka kabisa kukaa,fedha ambayo nilikuwa nayo kwa kipindi hicho ndiyo ilinisaidia kwa kipindi chote ambacho sikuwa na kazi,pia ndiyo fedha niliyotumia kumlipia Ada na matumizi mpenzi wangu Rehema wakati wote akiwa chuo cha ualimu.

Kuna kipindi hali ilipokuwa mbaya kiuchumi nilikuwa naenda pale Gongo la mboto kwa washikaji kujipendekeza kwenye magari na hatimaye kuna gari ambalo nililipata nikawa konda mimi na mshikaji wangu mmoja,lile gari lilikuwa likifanya ruti za Gongo la mboto kwenda Mbagala,niliamua kuto mtazama mtu usoni ili niweze kupambana,sasa nakumbuka Steve alikuwa akinishangaa mimi kuwa konda wa daladala ilihali niliacha kazi ambayo angalau ilikuwa kidogo na heshima ya usajili wa line,jamaa yeye aliona ni heri kuwa msajili line kuliko kuwa konda kazi ambayo ilikuwa ikidharaulika na kila mtu!,mimi sikuona taabu yeyote kwasababu nilishaifanya na ambacho nikagundua ni kwamba wakati huo makonda walikuwa wakipiga sana hela,yaani kulaza kwa siku elfu 20 lilikuwa jambo la kawaida kabisa,hiyo elfu 20 ni hela ambayo unabaki nayo baada ya mambo mengine kama msosi n.k

Mimi sikutaka kumuangalia mtu ananipangia nifanye nini,niliangalia kitu ambacho kinanipatia hela nzuri na ambacho nakifanya kwa moyo mmoja,aibu haikuwaga na haipo hadi leo kwenye maisha yangu ya utafutaji!.Kwenye lile gari nakumbula makonda tulikuwa wawili kwasababu lilikuwa gari lililokuwa na milango miwili,hivyo tukawa tunafanya kazi kwa kushirikiana!.

Namshukuru Mungu hata Rehema wangu ni mwanamke ambaye alikuwa hajali wala hachukii kile nilichokuwa nakifanya,tena nakumbuka ni mwanamke ambaye alinitia sana moyo katika kupambana.Alipomaliza chuo akawa ameajiliwa mkoani Morogoro wilaya ya Ifakara ambako ndiko anafanyia kazi hadi leo,baada ya kuwa ameajiliwa na kupangiwa kituo cha kazi akawa ameondoka.
Mimi niliendelea kupambana sana kwenye kazi ya ukonda na nikawa najinyima kiasi kwamba nikapunguza matumizi yasiyokuwa ya lazima.Baada ya kutengeneza kama milioni 2 kwa miezi kadhaa ya kujinyima,nikawa nimenunua tena uwanja maeneo ya kibamba,nililipa hela nusu nikawa napambana kutafuta pesa nyingine ili angalau nilipe yote kile kiwanja nikimiliki,nilipambana sana na hatimaye nikawa nimemaliza kulipia kile kiwanja,sasa kumbe kiwanja chenyewe kilikuwa na mgogoro wa kifamilia.Kiukweli nilihangaika sana na kile kiwanja,ilifika sehemu mtu aliyeniuzia tulifikishana hadi mahakamani,jamaa aliahidi kuwa atakuwa ananipatia hela kidogo kidogo hadi hela niliyompatia itakapokwisha,sasa ulipaji wake ulikuwa wa kusua sua na ikabidi niachane nacho,alinilipaga pesa kama nusu ya kile nilichompatia ikabidi niachane nae.
Rehema aliniambia nitulie niachane nacho na kama ni uwanja tungenunua mwingine,huu mji kiukweli umenitesa sana ndugu zangu.

Namshukuru Mungu baada ya kupata tena fedha kiasi ambazo nilizikusanya kwenye kazi yangu ya ukonda kwa kudunduliza,Rehema akawa ameniongezea fedha nyingine nikawa nimenunua pikipiki yangu na nikaanza rasmi kazi ya bodaboda ambayo ndiyo inaniweka mjini hadi leo.

Rehema alinizalia mtoto wa kike mzuri kama yeye na mwaka huu ifikapo mwezi wa kumi anatimiza umri wa miaka 5.Rehema hadi sasa ni mwanamke wangu ingawa mi naishi Dar es salaam na yeye akiwa kituo cha kazi hapo Ifakara,huwa naenda na yeye pia huwa anakuja Dar es salaam.

Ally Mpemba hadi sasa ninavyoandika hapa yupo na naona jamaa amekuwa mtu mkubwa sana,lile duka la pale gerezani walilifunga na ile fremu sikuhizi naona ina mtu mwenye biashara nyingine,duka lile la Aggrey bado lipo na huwa jamaa anakuwepo pale mara moja moja,ule mgahawa hadi sasa upo na unayo sifa ileile ya kuua wafanyakazi wake.

Jamaa kwasasa sijajua atakuwa anabiashara gani nyingine lakini hizo nilizoziacha bado zinafanya kazi.

Mwaka jana nikiwa kwenye mitikasi yangu Kkoo nilipita pale Aggrey nikawa nimemuona ila yeye hakuniona.Jamaa bado anaendeleza libeneke na kupiga pesa.

Mimi niliamua nichague haya maisha yangu yasiyokuwa na msongo hata kidogo kwasababu naridhika na hichi kidogo nikipatacho.

Kuna uwanja mwaka jana nimenunua kwa kushirikiana na Rehema wangu upo maeneo ya Maili moja,na Mungu akisaidia mwaka huu tunaweza kuanza ujenzi mdogo mdogo.

Kituo changu cha kazi huwa ni Bunju ingawaje pia huwa niko bize wakati fulani,mimi napaki Bunju ila sikai Bunju ndugu zangu.


Maisha si lelemama kama mnavyodhani,kama una nafasi ya kufanya chochote ambacho ni halali wewe fanya ili ukimbilie ndoto zako,usiogope kufanya kwa kuhofia watu watasema nini,wewe kaza moyo fanya,hao wanakucheka leo yawezekana kesho wakaanza kusema weww ni freemason,hivyo wape kisogo na fanya chochote ilimradi kinakuingizia pesa.

Usimuangalie mtu wewe ziangalie fedha,huyo mtu anakucheka kwasababu huna fedha,ukizipata hata kuwa na muda wa kukucheka tena.


MWISHO.
Stori nzuri UMUGHAKA ila point of correction
Ifakara sio wilaya
Wilaya ni kilombero , ambayo makao makuu ya wilaya ya kiloi yapo ifakara mjini.
 
Nimekutana na huyu client amevaa bangili la ki-@umughaka, aisee nilitaka niutumie huu mkono kwa kazi fulani ila nimeahirisha..[emoji23][emoji23][emoji23]

IMG_20230208_103452.jpg
 
Sku hz hapa town kila nikipishana na gari afu nkaona dereva ni mwarabu,,, naona kama nmeonana na ally mpemba

Afu kushoto nkimwona mwanamke kavaa kininja,, najisemea maya yuleee,, THOUGH SIAMINI KAMA KUNA UCHAWI.
 
Nisikuchoshe na usinichoshe, tusichoshane!.

Kwanza kabisa nipende kuwashukuru wote ambao mmeendelea kuwa na mimi bega kwa bega tangia mwanzo wakati naanza kusimulia visa vya maisha yangu ambayo nimeyaishi na kuyapitia kama mwanadamu.

Simulizi yangu ya kwanza kabisa hapa JF imefahamika kama "TULICHOMFANYA YULE MCHAWI HATOKUJA KUSAHAU KAMWE" hii inapatikana kwenye jukwaa hili la Entertainment, simulizi hii iliangazia namna tulivyopata shuruba ya ushirikina wakati ambao nilienda kumsalimia baba yangu mdogo aliyekuwa mwalimu katika shule moja ya sekondari huko mkoani Tabora, kiukweli ni mkasa ambao sitokuja kuusahau kamwe kwasababu ndipo niliamini wachawi wapo na uchawi upo!

Simulizi ya pili ilikuwa ni muendelezo baada ya hiyo ya kwanza, simulizi hii ya pili niliona nianze kusimulia baada ya mimi kwenda shule ya upili(Advance)na wakati nilipomaliza matokeo yangu hayakuwa mazuri hivyo nikatimuliwa na Mzee(Baba)yangu nyumbani nikaingia mtaani kupambana, simulizi hii inafahamika kama "NILIVYONUSURIKA KIFO BAADA YA MZEE KUNITIMUA NYUMBANI" na inapatikana kwenye jukwaa la Habari na Hoja Mchanganyiko.

Sasa leo nimeona niwaletee na niendelee na masimulizi ya maisha yangu ili kuwapa hamasa vijana wenzangu kuweza kupambana na kutokata tamaa mapema! Dhumuni la masimulizi yangu ni kutoa funzo kwa watu na sipo hapa ili kujipatia fedha kwa njia ya ulagahai, mimi binafsi ninajiweza kwasababu ni mpambanaji na sihitaji hata mia mbovu ya walalahoi wenzangu!.

Mimi binafsi ni mfanyabiashara, nimejiajiri kwa kutoa huduma ya usafirishaji wa abiria almaarufu kama Bodaboda, shughuli zangu huwa nazifanyia hapa Bunju, ingawa ki makazi naishi Mbezi Inn ila kikazi nafanyia Bunju. Sasa kama mtakumbuka kwenye simulizi ya mwisho nilisema ya kwamba, baada ya kuwa tumeuza lile duka la vipodozi ambalo tulikuwa tumefungua na rafiki yangu kipenzi Mtatiro (Kwa sasa anaishi nchini Uganda), tuliamua kugawana fedha kila mtu afe na chake, mimi niliamua kurudi zangu Tarime-Sirari, baada ya kukaa kule kuna ndugu yangu(Mtoto wa Baba yangu mkubwa) tuliwasiliana naye akaniambia nije Dar es salaam ili tufanye biashara ya uuzaji wa vyombo vya ndani kwasababu kwa wakati huo ilikuwa na pesa(Kwa maelezo yake).

Niliianza safari ya kuja Dar es salaam, sasa nilipofika Dar es Salaam pale Ubungo(Kipindi stendi bado haijahamia Mbezi), ile nimefika mida ya saa 5 usiku nikampigia simu mwenyeji wangu lakini majibu toka kwenye simu ni kwamba "Namba unayopiga kwasasa haipatikani, jaribu tena baadae", niliendelea kuipiga ile simu lakini majibu yalikuwa ni hayo hayo!.

Kwakuwa nilikuwa nimechoka, niliamua kumsikiliza moja ya watu ambao walikuwa wakinisumbua ili wabebe mzigo wa begi langu ili niwalipe posho, mpaka wakati huo nilikuwa makini sana kujilinda mimi binafsi pamoja na mzigo wangu, kilichofanya nikawa makini kupita kiasi ni stori ambazo mara zote nimekuwa nikizisikia kuhusu Jiji la Dar es Salaam na vioja vyake.

Mimi " Mwanangu vipi!?"

Jamaa " Poa bro"

Mimi "Mbona mnavurugu, shida ni nini?"

Jamaa " Si huyu msenge, nimemwambia wewe ni wakwangu lakini hataki kusikia"

Mimi "Ok mnasemaje"

Jamaa "Bro we nipe begi mi nikubebee, achana na huyu muhuni atakuibia"

Mimi " Sasa wote mnang'ang'ania mzigo, nimpe nani na nimwache nani?"

Mimi "Sa sikia, begi langu nitalibeba mwenyewe, achaneni na mimi"

Baada ya kusikia lafudhi yangu na namna nilivyochukia nadhani waliamua kutii sheria bila shuruti, waliondoka wakiwa wananiangalia kwa uchungu na maumivu makali ya kukosa posho! Kiukweli muda huo nilichokiongea ndicho nilichokuwa nikikimaanisha, kutokana na sifa mbaya za mkoa wa Dar es Salaam nilikuwa nimesema yeyote ambaye angejitia kimbelembele kunikaba au kuniibia, basi siku hiyo ndiyo ingekuwa mwisho wa maisha yake! Jeuri na kiburi cha kikurya vilinitia morali maradufu na niliwaona wale vijana wa pale stendi ni kama wanawake tu wasiokuwa na uwezo wa kunifanya chochote!.

Niliamua kujisogeza mpaka kwenye geti la kutoka nje, nilipotoka nje nilikuwa nikiendelea kushangaa pilika pilika namna zilivyokuwa za kutosha pale stendi, kiukweli sikuwahi kuona mji uliokuwa na pilika nyingi kama Dar es Salaam.

Mwanza nimekaa lakini hakukuwa na harakati za kutosha kama Dar es salaam. Nilichukua simu yangu nikawa nampigia tena mwenyeji wangu lakini simu yake ikawa haipatikani. Nilichukia sana kwasababu nakumbuka nilivyofika Singida alinipigia simu nikamwambia ya kwamba nimefika Singida na akawa amesema ikifika mida ya saa 2 usiku angekuwa amekuja pale stendi ili anisubiri nikifika tuondoke wote.

Kuna jamaa mmoja alikuwa kando ya geti la kutokea nje ya stendi pale Ubungo nilimsogelea nikawa namuuliza kuhusu Guest House yeyote iliyokuwa karibu ili niende nikalale na ikiwezekana asubuhi niendelee kumtafuta jamaa.

Jamaa "Sasa tutafanyaje ndugu!"

Aliendelea "Mwenyeji wako hajatokea?".

Mimi "Nimempigia simu lakini hapatikani!"

Jamaa "Duuuu mbona ni hatari!"

Aliendelea "Sasa sikia, wewe nyooka na hii barabara, unaona kwenye ile njia?"

Mimi "Ndiyo"

Jamaa "Hebu subiri"

Jamaa " Hassaniiiiiii"

Baada ya ya kuita hilo jina muhusika alifika

Jamaa "Hassani hebu nenda kampeleke huyu jamaa pale kwa Asteria, ukifika mwambie jamaa anataka chumba"

Aliendelea "Kaka nenda na jamaa atakupeleka kwenye Lodge ambayo kuna usalama na vyumba vipo vya kutosha, ila utamlipa maana kuna umbali"

Mimi "Hakuna tatizo"

Basi yule jamaa aliyeitwa Hassan akanichukua akanivusha barabara tukaikamata njia ya Ubungo Maziwa kuelekea kwenye hiyo lodge ambayo nimeambiwa kuna usalama na vyumba vya kutosha. Wakati tunakwenda na Bwana Hassan tulikuwa tunapiga stori za hapa na pale huku mikono yangu ikiwa bize imeng'ang'ania begi kwasababu ndilo lililokuwa na hela pamoja na nguo za kubadilisha, kiukweli nilikuwa nimesema endapo yeyote angejipendekeza kunikaba angejuta kuzaliwa.

Baada ya mwendo mrefu kidogo hatimaye tukawa tumefika kwenye Bar moja iliyokuwa inapiga mziki kwa sauti kubwa huku kukiwa na watu wengi.

Hassan " Nisubiri hapa nakuja"

Nilimsubiri Hassan pale nje baada ya kufika kwenye hiyo Bar na baada ya dakika 15 akawa amekuja kunichukua na kuongozana nae kuingia ndani. Tulipofika ndani ambako kulikuwa na kaunta, Hassan alinichukua tena kuelekea Uani ambako nilikuta kuna vyumba vingi ambavyo vilikuwa havipungui 10.

Sasa baada ya kufika pale Uani alikuja mwanamke mmoja mweusi mnene na ndiye aliyekuwa akiitwa Asteria, alimuita Hassan Pembeni wakawa wanaongea, sikufahamu kitu walichokuwa wanazungumza kwa wakati huo. Baada ya yale mazungumzo Hassan alirudi kwangu.

Hassan "Sasa bro,mimi nadhani nikuache wewe upumzike, niangalizie basi ustaarabu"

Mimi "Chumba changu cha kulala ni kipi?"

Hassan "Atakuonyesha Asteria, wala usijali kaka hapa ni nyumbani"

Baada ya maneno ya kutia moyo ya Hassan nikachomoa shilingi elfu 5 nikawa nimempatia kama posho ya kunipeleka hapo Guest.

Hassan "Aaah kaka hela gani hii?"

Mimi "Hela gani kivipi?"

Hasaan "Aaaah Kaka yaani nikutoe kule stendi na nimeacha shughuli zangu halafu unanipatia buku tano? Hebu ongeza ongeza kaka angalau kesho niamkie supu"


Sikutaka mambo mengi na yule Jamaa ikabidi nizame tena mfukoni nikatoa elfu 5 nyingine nikampatia, hivyo kufanya jumla kuwa elfu 10.

Baada ya jamaa kuondoka lile eneo nikamfuata yule demu aliyeitwa Asteria ili aje anionyeshe chumba niingie kulala kwasababu nilikuwa nimechoka.

Asteria "Kaka ina maana Hujaambiwa huu si muda wa kulala?"

Mimi "Si muda wa kulala?"

Mimi "Si muda wa kulala kivipi?"

Asteria "Kaka hapa huwa hatulazi watu ila tunakodisha!"

Aliendelea "Hivi vyumba vinakodishwa kwa dakika na masaa, labda usubiri mpaka saa 9 wateja wakipungua ndipo tutakukodishia ulale"

Kiukweli baada ya ile kauli niliishiwa nguvu ghafla, sasa baada ya kuniambia maneno yale yeye aliondoka akaenda kuendelea na shughuli zake akaniacha pale Uani nikiwa sijui cha kufanya, sasa ndipo nilikuja kugundua ya kwamba, vile vyumba vilikuwa vinatumika kwenye biashara ya short time(Biashara ya Ngono),sasa kumbe ile Bar niliyopelekwa, pale nje kulikuwa na wanawake wanaouza miili yao(Dada Poa) na vile vyumba vilitumika kwa shughuli ya short time.

Itaendelea.

Muendelezo soma Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani

SEHEMU YA 1
SEHEMU YA 2
SEHEMU YA 3
SEHEMU YA 4
SEHEMU YA 5
SEHEMU YA 6
SEHEMU YA 7
SEHEMU YA 8
SEHEMU YA 9
SEHEMU YA 10
SEHEMU YA 11
SEHEMU YA 12
SEHEMU YA 13
SEHEMU YA 14
SEHEMU YA 15
SEHEMU YA 16
SEHEMU YA 17
SEHEMU YA 18
SEHEMU YA 19
SEHEMU YA 20
SEHEMU YA 21
SEHEMU YA 22
SEHEMU YA 23
SEHEMU YA 24
SEHEMU YA 25
,lubawa ukuje
 
Sku hz hapa town kila nikipishana na gari afu nkaona dereva ni mwarabu,,, naona kama nmeonana na ally mpemba

Afu kushoto nkimwona mwanamke kavaa kininja,, najisemea maya yuleee,, THOUGH SIAMINI KAMA KUNA UCHAWI.
Leo mchana nilienda maeneo ya CHINA PLAZA kwa nyuma kuna duka la simu nikaingia kuangalia simu nikamkuta mwenye duka ni Mpemba kichwani ikanijia hii simulizi. Hahahahaa
 
Back
Top Bottom