Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani

Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani

hao wanawake wa kikurya we kabila lingine huwawezi,kabla ya kuhamia kwenye nyumba yao mpya huku chanika,baada ya kumaliza kushusha mizigo,uliibuka mzozo mkubwa kati ya mke na mume,zilipigwa si chini ya masaa matatu,sisi tunaangalia tu,kuuliza kisa nini,tunaambiwa hao ni wakulya huo mzozo ni kama brekifasti,lanchi bado,tulichoka sana aisee...
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] breakfast
 
Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani - 10.





Nilishitushwa na sauti ya Steve akiwa ananiita na kunigongea akitaka nimfungulie mlango,nilipochukua simu na kutazama muda ilikuwa imefika saa 4.Niliamka nikaenda kumfungulia jamaa mlango,kiukweli alionekana hayuko kawaida na sikutaka kumpa presha,nilimwambia aingie alale atulize akili.

Namshukuru Mungu kulipokucha,mimi niliwahi kuondoka nikamuacha jamaa akiwa amelala,kabla ya kwenda Kariakoo ilikuwa ni lazima kila msajili line kupitia pale ofisini Buguruni kusikiliza kikao na mambo mapya kisha kuelekea kwenye kituo chake cha kazi,nami ndivyo nilivyofanya!.Nilipofika Kariakoo nilielekea eneo ambalo nilikuwa nikihifadhia vitu vyangu vya kazi na kuja kuanza kupiga kazi.

Sasa wakati nafika pale,lile duka la Ally mpemba lilikuwa bado halijafunguliwa,mi niliweka zangu meza nikaanza kupiga kazi kawa kawaida,kiukweli kwa kipindi kile kulikuwa na wateja wengi mno,yaani ilikuwa ukifungua tu ile saa 2 asubuhi wateja wanaanza.Ilipofika mida ya saa 3 asubuhi,kuna gari aina ya Range Sport nyeusi iliyokuwa na Private Number iliyoandikwa " SALIM " ilisimama pembeni yangu kisha ukafunguliwa mlango akawa ameshuka yule Aunt ndugu yake na Ally Mpemba.

Aunt "Leo umeniwahi"

Mimi "Leo nimekuwahi Aunt,salama lakini"

Aunt "Mie niko salama kabisa sijui wewe huko utokako"

Mimi "Salama kabisa"

Wakati nikiwa naendelea kuzungumza na Aunt ile gari ikawa imeondoka kuelekea Kamata.Yule Aunt pamoja na ndugu yake Ally Mpemba walikuwa wakizungumza kiswahili cha kipwani pwani kama ambavyo wazanzibar wakizungumza!.

Ilipofika mida ya 5 asubuhi,alinipigia simu Steve na akawa ananiambia ya kwamba,yule demu wake wamekubaliana arudi nyumbani na yeye amemsamehe ili mambo mengine yaendelee,mimi kwakuwa nilishamshauri sana kuonekana kama natwanga maji kwenye kinu nilimwambia sawa,hakuna tatizo,sikutaka kabisa kuwashauri kwasababu niliona ni kama nilikuwa napoteza muda.

Mimi "Kwahiyo vitu anarudisha?"

Steve "Ndo naenda kuvichukua kaka"

Mimi "Kwahiyo Leo hujaenda Tandika"

Steve "Leo siendi kaka ngoja kwanza nikamchukue huyu"

Mimi "Poa,kama ukitoka funguo utaniwekea juu ya mlango hapo"

Steve "Leo sina ratiba ya kutoka kaka"

Mimi "Sawa,baadae"

Safari hii niliamua nikae pembeni katika kushuri kwasababu nilichokuja kugundua ni kwamba,mambo yote ya msingi niliyokuwa nikimshauri jamaa kuhusu demu wake,yeye alikuwa akimwambia kila kitu na hivyo mimi kuonekana mchonganishi!,hivyo nikaamua sitokaa tena nimshauri na kama ni kufa yeye afe tu!.

Ilipofika mida ya saa 9 mchana,Ally Mpemba akawa amekuja akiwa ndani ya kanzu nyeupe,alipofika pale nje kabla ya kuingia ndani ya duka lake akawa amenisalimu.

Ally mpemba "Assalam aleykum"

Mimi "Alekom salam"

Ally mpemba "Kwema?"

Mimi "Kwema kaka"

Ally mpemba "Leo wafunga saa ngapi?"

Mimi "Kama kawaida kaka saa 12"

Ally mpemba "Basi utanipa muda wako kidogo Leo sheikh"

Mimi "Sawa kaka"

Sasa mida ya saa 10 alasiri alipokuwa anatoka pale dukani akawa ameniomba kama itawezekana tuondoke wote kuelekea Aggrey.

Mimi "Si hakuna haja ya kutoa vitu vyangu"

Ally mpemba "We viache tu,nishamwambia Farah atakuangalizia usijali"

Niliondoka na Ally kuelekea mtaa wa Aggrey ambako huko nako nilikuta kuna duka kubwa la simu na ndani yake kukiwa na wafanyakazi kama 4 wakisaidiana kuuza,sasa tofauti na kule ni kwamba lile la kule niliko lilikuwa dogo na la pale Aggrey lilikuwa kubwa.

Ally mpemba "Mi huwa nashinda hapa mara zote,nisipokuwa kule basi wanipata hapa"

Mimi "Ok sawa kaka lete maneno"

Ally mpemba "Kuna kazi nataka unisaidie Master"

Mimi "Kazi gani tena kaka?"

Ally Mpemba "Ni kazi ya kawaida tu!"

Aliendelea "Mimi ninahusika pia na mambo ya caterings na nimewaajiri ndugu wa familia na watu wengine lakini ndugu zangu ni watu wa ovyo sana huwa hawapendi kazi za kujishughulisha wao wanapenda kukaa kama hivi unavyowaona"

Ally Mpemba "Sasa kila ninapokutazama nakuona wewe ni mpambanaji mtu wa bara na ndiyo maana nakuita Master"

Aliendelea "Mimi nataka tu unisaidie kitu kimoja na offcouse siyo msaada bali nataka tufanye kazi"

Mimi "Sawa kaka"

Ally Mpemba "Kwani huko Tigo mnalipana shi ngapi?"

Mimi "Kaka kule ninalipwa kwa kamisheni"

Ally Mpemba "Sawa naelewa ni kamisheni lakini malipo yao huwa yapoje?"

Mimi "Inategemea na laini nilizosajili na matumizi ya wateja kwa mwezi husika"

Ally Mpemba "Doo kwahiyo mteja asipotumia laini hulipwi!"

Mimi "Ni mara chache mteja aje kusajili line na asiitumie,sema huwa malipo yanategemea,kuna muda yanapungua na kuna muda yanaongezeka"

Ally Mpemba "Ok sasa mimi nataka unisimamie kwenye mradi wangu hata kwa muda wa mwezi tu Master halafu nikipata mtu muaminifu nitamuweka halafu wewe utaendelea na shughuli zako:

Mimi "Kaka kwanini mimi?"

Allya Mpemba "Mi unajua nilikuwa sikutilii maanani sana,kuna siku Farah akaniambia wewe ni mtu poa sana hata namna unavyo behave,kwa maana nilipokuta umeweka meza yako kando ya duka langu nilimwambia Farah unapaswa utoke pale ila akaniambia wewe ni mtu poa sana"

Aliendelea "Ninachotaka mimi ni kwamba,wafanyakazi wapo ila wewe ukanisimamie tu maana alikuwa anasimamia mama yangu mdogo lakini yuko Unguja anamuuguza me wake!"

Aliendelea "Wewe niambie tu unataka niwe nakulipa shi ngapi?"

Mimi "Kaka unajua sijawa na uzoefu na kazi unayotaka niifanye,hivyo itakuwa ngumu kujua unilipeje kaka"

Ally Mpemba "Sasa fanya hivi,wewe nenda kahifadhi vitu vyako halafu uje twende nyumbani mara moja"

Basi niliondoka zangu kurudi gerezani nikachukua meza,kiti pamoja na mwamvuli nikawa nimerudisha mahali ambapo nilikuwa nahifadhia.Baada ya hapo nikawa nimeondoka hadi Aggrey kisha Ally Mpemba akanichukua kuelekea Msimbazi uelekeo wa kituo cha polisi,tulitembea hadi pale Big Bon ambapo nikaona anatoa funguo wa gari kwenye kanzu yake kisha akabonyeza ile gari ikawaka taa na milango ikafunguka,ilikuwa ni ile ile Range ambayo asubuhi niliona dada yake akiwa anashushwa ambayo ilikuwa na Private Number,sasa kwa mara ya kwanza mwanaume kutoka Kijiji cha Mogabiri huko Ukuryani Tarime nikapanda Range,aisee asikwambie mtu na ndiyo maana kuna watu wako tayari kufanya kila aina ya ovu ili kujipatia fedha wanunue magari,ile ilikuwa ni moja ya gari nzuri kuwahi kupanda katika maisha yangu ya umasikini!.

Tuliondoka lile eneo tukaikamata Morogoro Road kisha safari ikaanza kwa spidi ya wastani,baada ya muda tukawa mbele ya nyumba moja maeneo ya magomeni Mikumi,ile nyumba ilikuwa ya kawaida sana kwa muonekano wa nje ila nilipoingia ndani kiukweli ilikuwa nzuri mno na usingedhani kama muonekano wa nje unasadifu kilichomo ndani!.

Baada ya kupiga honi na kufunguliwa geti gari ikawa imeingia pale uani na kupaki,sasa tulipoteremka kuna vitoto vya kike viwili vya kiarabu(Kipemba) tulivikuta hapo ndani vikawa vinamkimbilia Ally na kumrukia kwa furaha!.

Ally Mpemba " Hawa ni watoto wa Farah "

Mimi "Ooh sawa kaka"

Sasa pale nje nilikuta kuna vyombo vingi sana vya kisasa na majiko makubwa ya Gesi na mkaa,na ndivyo vilikuwa vyombo vilivyokuwa vinatumika kwenye shughuli za catering.

Ally Mpemba "Nimekuleta hapa ili ujionee mwenyewe,na ukishajionea najua utaniambia nikulipe kiasi gani master"

Aliendelea "Sasa wewe kazi yako utakuwa unahakikisha vyombo vyote vinaondoka hadi kwenye events na baada ya hapo utakuwa unahakikisha vyombo vyote vinarudi kama vilivyokuwa,baada ya hapo utakuwa unasimamia ishu ya usafi wa vyombo"

Aliendelea "Kikubwa wewe utakuwa msimamizi"

Baada ya yale maelezo angalau sasa ndipo nikaanza kupata uelewa wa kazi nitakayoenda kuifanya.

Ally Mpemba "Na bahati nzuri ni kwamba,events siyo kila siku,kama kutakuwa hakuna events yeyote wewe utakuwa unaendelea na shughuli zako,mimi nahitaji tu msimazi hadi pale atakaporudi mama mdogo au nitakapompata mtu sahihi,ila nakuomba kwa sasa unisaidie kwenye hili"

Mimi "Sawa kaka nimekuelewa"

Ally Mpemba "Ok sasa niambie niwe nakulipaje!"

Mimi "Wewe nilipe utakavyoona kaka"

Ally Mpemba "Wewe niambie kiasi utakachoona kwako kinafaa maana hii siyo shughuli nyepesi kama unavyodhani!"

Mimi "Tufanye hivi kaka,tukianza kazi ndiyo nitajua,nadhani kwasasa tusubiri kwanza "

Ally mpemba "Ok hakuna tatizo maadamu umeamua hivyo!"

Baada ya mazungumzo yale tuliingia kwenye gari tukawa tumeondoka kuelekea Kariakoo,sasa wakati tunarudi tulipitia njia ya Kigogo na tulipofika pale Karume,jamaa alinipatia elfu 20 ya nauli mi nikashuka kwenye gari yeye akawa ameondoka.Nilienda upande wa pili kupanda gari za Gongo la mboto na kuondoka zangu maskani.



Itaendelea.......
baby zu umeona umughaka alivyo itikia Salam huku? Kaambiwa Assalaam Aleykum kajibu Aleko msalam
 
😅😅😅Wakurya ni wababe sana. Mwanamke wanamweka kwenye daraja la chini, wanamchukulia kama mtoto hivi.

Kuna siku nilikutana na Kijana mmoja wa Kikurya, sasa katika mazungumzo tukafikia kuulizana kama ana mchumba. Akasema Ukuryani hawana msamiati wa mchumba, wana msamiati wa mke tu. Kwamba, kijana akishamwona msichana wa kumwoa basi huwa hakuna habari za uchumba. Ni mahari na ndoa inafuata. Nilishangaa na sikuelewa kwa urahisi. Labda kama wapo Wakurya humu wathibitishe juu ya hili.
Happy Christmas Antonnia
Thank you mkuu Hope uliinjoy to the fullest!!!

Kumbe wana mfumo dume doh!! Hatariii sana hio
 
Back
Top Bottom