Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani

Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani

Thanks for the tag best,,,,

Master ana tamaa, maya anampa usiku mzima kwa nn anahangaika na rehema ?

Naona Maya alijua jamaa anachepuka ndo maana alisusa chakula [emoji2][emoji1][emoji2]!

In reality wanasema kuwa kwa mfano ukiingiwa na jini mahaba lina wivu Sana, halipendi ushiriki na mtu mwingine !!!!

Sasa inaonekana yule Babu mganga kampigia ally kuwa ndg yako ameharibu !
Hahahaahahahah..... Master aliyavagaaa walaiii hakujua moves zake zote ziko Ally mpemba anazipata bila master kujuaaa! Au ukute alimpakiza Rey siti ya mbelee lol hapana chezea jeuriiii ya pesaa best!
Ngoja tuonee itavokua!
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Nina sababu ni sikufokei maana kipindi Cha nyuma wenye hela walitumia Mapolisi ili kumkamata Mwenye JamiiForums ili atoe taarifa za Members humu. Kwahiyo nakuambia tu. Nenda Google kaandike kesi ya Maxence Melo usome vizuri

Sent from my SM-J700H using JamiiForums mobile app
Heeeh kumbe!😳😳 ! Asante kwa taarifa mkuu!
 
sehemu ya 21
Basi bwana,baada yakuona kwa macho yangu Farah alichokifanya,yaani kuingia chumbani kwa kaka yake bila kutumia ufunguo kama malaika,majini na wachawi wafanyavyo nilibaki kinywa wazi huku nikitafakari mimi ni mtu wa aina gani kukubali kuishi mazingira yaliyozungukwa na miujiza kama sio mauza uza

Nikakumbuka vile visa vya wachawi kule kwa baba mdogo headmaster, nikakumbuka kisa cha kuvua kule kambini kwa shemeji yangu ambako walikuwa wakifanya ushirikina wazi wazi nikiwashuhudia,tena nakumbuka kuna siku walimchinja mtoto ziwani huku nkishuhudia eti ili wapate samaki wengi

Nikakumbuka visa vya kipindi kile niko jambazi,jinsi nilivyopelekwa kwa mganga tukalimia meno mimi na msela wangu Mutatiro,nikakumbuka visa nilivyofanyiwa na mjomba Niko

Nikabaki tu nimeinamisha kichwa chini nikijiuliza ni ipi sababu ya mwenyezi mungu kuruhusu umughaka aje Duniani

Nikataka nifungue mlango ili niende kulala kule chumbani kwa Ally lakini nikapata hofu kuu kwa kutokujua aunt Farah atakuwa amepachikamo zana gani mpya nikafikia maamuzi ya kwenda kulala kwenye Audi yangu

Nilipofungua tu mlango wa gari ili nilale du sikuyaamini macho yangu kwa nilichokiona

Niliikuta ila shuka tuliyoitandika kitandani wakati nampelekea moto huyu Dada yake ally ikiwa imetandikwa kwenye siti za nyuma za gari.Nikabaki nimeduwaa tu nisijue kipi cha kufanya maana ndani hakulaliki na kwenye gari hakulaliki.Wakati nikiwa bado kwenye hiyo hali ya kuduwaa mara nikasikia sauti kama ya maya akiniita kwa jina langu la ulisyani(utotoni),mung'osi,mung'osi Maya akawa anaita nikaamua kupiga kimya lakini akawa sasa anaanza kugonga mlango kwa nguvu sana kana kwamba kuna kitu kinamuogopesha kukaa peke yake humo kwenye limjumba la kake yake mjalaana

Nikawa kama nimepatwa na ukichaa wa dakika mbili hivi,nikakimbilia kule mlangoni anakogonga maya tena nikarudi kule kwenye Audi yangu kwa speed ya bombardier (hili zoezi nililifanya mara kumi na mbili).Kiukweli nilikuwa kwenye state of confusion ambayo sijawahi kuwa nayo toka nizaliwe mimi umughaka

Baada ya kuona kelele za maya kugonga mlango ndio zimezidi na sasa alikuwa akilitaja jina langu la utoto kama vile mtu amtajavyo jina la bwana yesu ili amuokoe pindi akunapo na pepo mchafu,nikawa nimepata ujasiri wa ajabu sana,nikaamua niende niufungue tu mlango nimkamate maya na kumfungia huko huko chumbani kwake,halafu niende kule chumbani kwa bro Ally mpemba nikaangalie yule msagane(Farah) aliweka nini kisha nisubirie kitakachotokea maana haiwezekani niwe muoga kiasi hiki wakati nilitahiriwa bila ganzi wala nusu kaputi.Huyo mnyama umughaka nikajivisha ukomandoo na kuanza kuuelekea mlango wa nyumba,wakati nimekaribia kabisa kuufikia mlango nikasikia sauti za makelele ya maya zimekoma na kumekuwa na ukimya wa ajabu sana kana kwamba hakuna kilichotokea nikabaki nimeduwaa nisijue cha kufanya.Nikaamua tu nirudi kule kwenye Audi yangu niwashe AC nilale,kitu msichokijua wapenzi wasomaji licha ya kuwa mpenzi mkubwa wa soka vile vile mimi ni mpenzi mkubwa sana wa AC kiasi kwamba kuna kipindi hata sasa hivi nikiwa naendesha bodaboda huwa nalazimika kwenda dukani kwa Ally na kumlilia aniruhusu niingie kwenye ile Range yake ili japo nipate starehe ya AC hata kwa robo SAA tu jamani

Nikaiendea ile Audi yangu na kuufungua mlango kijasiri kabisa eti nikakuta ile shuka bwana aimo,nikaingia ndani na kuwasha AC kisha mwanaume nikalala huku nikifikiria kesho niende kule kwa kiheli nikamdorishie hili liaudi langu halafu baadae niende kule kwa yule muuza juice ninywe juice ya 20000 ili nione kama atanikubali haraka na mimi nijilie mzigo bwana kwani sh ngapi

Itaendelea
Hii nguvu unayoitumia kwenye hadithi za wengine, kwanini usingeitumia kuandika ya kwako ukapost?
 
Mimi ndio maana huu uzi huwa sikanyagi kabisa maana kuna watu wanakera sana. Ninacho fanya huwa na search jina lako kisha naangalia kama umeweka ama laa. Kama umeweka nitasoma kisha napotea na kama hujaweka sitii neno lolote napotea kama sikuwepo vile.
USHAURI



Usipende kumfanyia mwenzio jambo ambalo wewe usingependa abadani kufanyiwa.

Kuna muda huwa napitia komenti za watu humu ndani nakuta ni lugha chafu za matusi,dhihaka,dharau na kebehi kwangu au kwa watu wengine.Sasa sielewi ni hii stori tu ndiyo inaleteleza hayo yote au uenda kuna ajenda nyuma ya pazia.

Mimi nilipoamua kuleta simulizi zangu hapa nadhani nia na madhumuni ni kutoa funzo,kuelimika na kuburudisha wenye misongo,hakuna mahali nimewahi kusema nitaleta episode muda gani na saa ngapi!.

Hivi mmewahi kujiuliza swali tu la kawaida ya kwamba kwanini stori nyingine nilikuwa nikiandika mfululizo kila siku episode?,kwanini baadhi yenu muishie kutukana bila kunifata dm na kuniuliza nimepatwa na nini?,au dm ni mbali sana?,au mnadhani matusi ndiyo suluhisho?.

Mbona kuna watu kadhaa wamenifata dm wameniuliza ni kitu gani kimesababisha siweki episode mfululizo nikawajibu wakaridhika?,Ndugu zangu hii platform walioibuni waliumiza vichwa,walipoteza muda na gharama zao wakiwa na lengo la kuwakutanisha watanzania na wasio watanzania kwa wakati mmoja ili kubadilishana mawazo na kuelimika kwa namna moja ama nyingine,ila sisi leo badala ya kueleimika ndipo tunazidi kuwa wajinga na tunachukulia poa kama ilikuwa lazima,mtu anapofanya kitu kizuri apongezwe na anapokosea akosolewe na aulizwe kwanini amefanya hivyo na wala si matusi kwasababu hayatosaidia kitu.

Simulizi zangu zote nimekuwa nikisimulia eidha nikiwa kijiweni au nikitoka kijiweni nikiwa home nimepumzika,sasa huu ni mwezi January na kama mnavyofahamu ni muda wa kilimo,hivyo na mimi sikuwepo na nadhani niliwaambia nitakuwa mkoani Mbeya,na huko nilienda kwa ajili ya mambo mengine lakini kilimo kikiwa ni sehemu moja wapo ya uwekezaji wangu,sasa kama mjuavyo kilimo kinavyotaka umakini na muda,ndiyo maana nilipokuwa nikipata muda naendelea japo kwa episode moja lakini watu bado hawaridhiki wanaendelea kutukana tu!.

Jamani,kama nyie wenzangu mnakazi za maofisini na muda wote mnataka kuperuzi basi hongera kwenu,mimi ni mpambanaji na ndiyo maana mwaka huu nikasema niwekeze angalau na kwenye kilimo na ndiyo muda wa kuandika nilikuwa nakosa,tuache kuwa tunalalamika na kutukana kwasababu haitusaidii bali inashusha heshima na kutufanya kuonekana hatuna uelewa.

Pia nadhani JF kuna "buton" ya IGNORE/BLOCK,ni vema kama unafikiri nakukera,nakuudhi,nakufedhehesha ukabinya hiyo button ili uwe huru usiweze kunifatilia angalau ukawa na amani kuliko kuendelea kuishia kutukana tu bila sababu ya msingi,pia hapa JF sikufata followers au kura za mwandishi bora kama wengi wenu mnavyodhani,nimeanza kuandika huu uzi hata kabla ya hizo kitu na hakuna mahali nimewahi kumuomba mtu au kimlazimisha anipigie kura,ni watu waungwana na wenye mapenzi mema na mimi ndiyo waliona nafaa wakanipigia kura,sihitaji umaarufu hapa kwasababu sipendi kuwa maarufu,sihitaji hata thumni ya mtu kwasababu ninachokipata kinanitosha na naridhika,hivyo niwaombe ambao mnaona nawakera mnaweza kupita kimya kimya bila matusi na mkawaacha wale wanaotaka kuelimika na kuburudika,siyo kwamba wewe hutaki uwalazimishe na wengine wakuunge mkono kwenye ujinga wako.


Umeikuta EPISODE soma,hujaikuta kausha na endelea na mambo yako,sidhani kama utapungukiwa!.

NOW NIPO MJINI,KILA SIKU NITAKUWA NASHUSHA EPISODE HADI ITAKAPOISHA,LABDA NIFE LEO USIKU.


Ni hayo.
 
Hahahaahahahah..... Master aliyavagaaa walaiii hakujua moves zake zote ziko Ally mpemba anazipata bila master kujuaaa! Au ukute alimpakiza Rey siti ya mbelee lol hapana chezea jeuriiii ya pesaa best!
Ngoja tuonee itavokua!
tatzo rehema ana mzigo wa maana , master kashindwa kujizuia na hivi tupesa tupo, kupendeza kwa Sana !

Namfikiria Rey ana shape Kama lako [emoji41]
 
tatzo rehema ana mzigo wa maana , master kashindwa kujizuia na hivi tupesa tupo, kupendeza kwa Sana !

Namfikiria Rey ana shape Kama lako [emoji41]
Khakhaaaaa!! Kuna wanaume mnapenda mitrakoo nyieee lol!
Weeeee nimfikie Rey hata robo ya robo yake nitrambeee 😎😎!

Hio sehemu ya kumvua Rey nguo na kumtia jiti la mlanzi kama watu hawajajichafua sijuuuiii 😄!
 
Ila umughaka umevuka kwenye 20 kuna muendelezo pale kujua farah ilikuaje kaingia chumban kwa Ally mpemba na Usiku huo ulisema utathibitisha kuwa utamuangalia vyema maya uone kama kuna tofauti
Ameeleza kuwa Farah alilazimisha kuingia ndani na maya alimkagua fresh isipokuwa alama ya mkononi tu maana alimpa mgongo
 
Back
Top Bottom