USHAURI
Usipende kumfanyia mwenzio jambo ambalo wewe usingependa abadani kufanyiwa.
Kuna muda huwa napitia komenti za watu humu ndani nakuta ni lugha chafu za matusi,dhihaka,dharau na kebehi kwangu au kwa watu wengine.Sasa sielewi ni hii stori tu ndiyo inaleteleza hayo yote au uenda kuna ajenda nyuma ya pazia.
Mimi nilipoamua kuleta simulizi zangu hapa nadhani nia na madhumuni ni kutoa funzo,kuelimika na kuburudisha wenye misongo,hakuna mahali nimewahi kusema nitaleta episode muda gani na saa ngapi!.
Hivi mmewahi kujiuliza swali tu la kawaida ya kwamba kwanini stori nyingine nilikuwa nikiandika mfululizo kila siku episode?,kwanini baadhi yenu muishie kutukana bila kunifata dm na kuniuliza nimepatwa na nini?,au dm ni mbali sana?,au mnadhani matusi ndiyo suluhisho?.
Mbona kuna watu kadhaa wamenifata dm wameniuliza ni kitu gani kimesababisha siweki episode mfululizo nikawajibu wakaridhika?,Ndugu zangu hii platform walioibuni waliumiza vichwa,walipoteza muda na gharama zao wakiwa na lengo la kuwakutanisha watanzania na wasio watanzania kwa wakati mmoja ili kubadilishana mawazo na kuelimika kwa namna moja ama nyingine,ila sisi leo badala ya kueleimika ndipo tunazidi kuwa wajinga na tunachukulia poa kama ilikuwa lazima,mtu anapofanya kitu kizuri apongezwe na anapokosea akosolewe na aulizwe kwanini amefanya hivyo na wala si matusi kwasababu hayatosaidia kitu.
Simulizi zangu zote nimekuwa nikisimulia eidha nikiwa kijiweni au nikitoka kijiweni nikiwa home nimepumzika,sasa huu ni mwezi January na kama mnavyofahamu ni muda wa kilimo,hivyo na mimi sikuwepo na nadhani niliwaambia nitakuwa mkoani Mbeya,na huko nilienda kwa ajili ya mambo mengine lakini kilimo kikiwa ni sehemu moja wapo ya uwekezaji wangu,sasa kama mjuavyo kilimo kinavyotaka umakini na muda,ndiyo maana nilipokuwa nikipata muda naendelea japo kwa episode moja lakini watu bado hawaridhiki wanaendelea kutukana tu!.
Jamani,kama nyie wenzangu mnakazi za maofisini na muda wote mnataka kuperuzi basi hongera kwenu,mimi ni mpambanaji na ndiyo maana mwaka huu nikasema niwekeze angalau na kwenye kilimo na ndiyo muda wa kuandika nilikuwa nakosa,tuache kuwa tunalalamika na kutukana kwasababu haitusaidii bali inashusha heshima na kutufanya kuonekana hatuna uelewa.
Pia nadhani JF kuna "buton" ya IGNORE/BLOCK,ni vema kama unafikiri nakukera,nakuudhi,nakufedhehesha ukabinya hiyo button ili uwe huru usiweze kunifatilia angalau ukawa na amani kuliko kuendelea kuishia kutukana tu bila sababu ya msingi,pia hapa JF sikufata followers au kura za mwandishi bora kama wengi wenu mnavyodhani,nimeanza kuandika huu uzi hata kabla ya hizo kitu na hakuna mahali nimewahi kumuomba mtu au kimlazimisha anipigie kura,ni watu waungwana na wenye mapenzi mema na mimi ndiyo waliona nafaa wakanipigia kura,sihitaji umaarufu hapa kwasababu sipendi kuwa maarufu,sihitaji hata thumni ya mtu kwasababu ninachokipata kinanitosha na naridhika,hivyo niwaombe ambao mnaona nawakera mnaweza kupita kimya kimya bila matusi na mkawaacha wale wanaotaka kuelimika na kuburudika,siyo kwamba wewe hutaki uwalazimishe na wengine wakuunge mkono kwenye ujinga wako.
Umeikuta EPISODE soma,hujaikuta kausha na endelea na mambo yako,sidhani kama utapungukiwa!.
NOW NIPO MJINI,KILA SIKU NITAKUWA NASHUSHA EPISODE HADI ITAKAPOISHA,LABDA NIFE LEO USIKU.
Ni hayo.