Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yeah nafikiri hii 20 ilitakiwa iwe 21..alafu 20 kaiacha sehemu...kuna muunganiko umekosekana ila kwakuwa mtunzi na msimulizi ni master basi tunakausha tu kwakuwa tunapata mafundisho na burudani inshaalah yatosha.Ila umughaka umevuka kwenye 20 kuna muendelezo pale kujua farah ilikuaje kaingia chumban kwa Ally mpemba na Usiku huo ulisema utathibitisha kuwa utamuangalia vyema maya uone kama kuna tofauti
Kima kweli hilo punga linajiona jaanjaa wakati lofa tu.unatafuta mume kwa nguvu
Unazinguasehemu ya 21
Basi bwana,baada yakuona kwa macho yangu Farah alichokifanya,yaani kuingia chumbani kwa kaka yake bila kutumia ufunguo kama malaika,majini na wachawi wafanyavyo nilibaki kinywa wazi huku nikitafakari mimi ni mtu wa aina gani kukubali kuishi mazingira yaliyozungukwa na miujiza kama sio mauza uza
Nikakumbuka vile visa vya wachawi kule kwa baba mdogo headmaster, nikakumbuka kisa cha kuvua kule kambini kwa shemeji yangu ambako walikuwa wakifanya ushirikina wazi wazi nikiwashuhudia,tena nakumbuka kuna siku walimchinja mtoto ziwani huku nkishuhudia eti ili wapate samaki wengi
Nikakumbuka visa vya kipindi kile niko jambazi,jinsi nilivyopelekwa kwa mganga tukalimia meno mimi na msela wangu Mutatiro,nikakumbuka visa nilivyofanyiwa na mjomba Niko
Nikabaki tu nimeinamisha kichwa chini nikijiuliza ni ipi sababu ya mwenyezi mungu kuruhusu umughaka aje Duniani
Nikataka nifungue mlango ili niende kulala kule chumbani kwa Ally lakini nikapata hofu kuu kwa kutokujua aunt Farah atakuwa amepachikamo zana gani mpya nikafikia maamuzi ya kwenda kulala kwenye Audi yangu
Nilipofungua tu mlango wa gari ili nilale du sikuyaamini macho yangu kwa nilichokiona
Niliikuta ila shuka tuliyoitandika kitandani wakati nampelekea moto huyu Dada yake ally ikiwa imetandikwa kwenye siti za nyuma za gari.Nikabaki nimeduwaa tu nisijue kipi cha kufanya maana ndani hakulaliki na kwenye gari hakulaliki.Wakati nikiwa bado kwenye hiyo hali ya kuduwaa mara nikasikia sauti kama ya maya akiniita kwa jina langu la ulisyani(utotoni),mung'osi,mung'osi Maya akawa anaita nikaamua kupiga kimya lakini akawa sasa anaanza kugonga mlango kwa nguvu sana kana kwamba kuna kitu kinamuogopesha kukaa peke yake humo kwenye limjumba la kake yake mjalaana
Nikawa kama nimepatwa na ukichaa wa dakika mbili hivi,nikakimbilia kule mlangoni anakogonga maya tena nikarudi kule kwenye Audi yangu kwa speed ya bombardier (hili zoezi nililifanya mara kumi na mbili).Kiukweli nilikuwa kwenye state of confusion ambayo sijawahi kuwa nayo toka nizaliwe mimi umughaka
Baada ya kuona kelele za maya kugonga mlango ndio zimezidi na sasa alikuwa akilitaja jina langu la utoto kama vile mtu amtajavyo jina la bwana yesu ili amuokoe pindi akunapo na pepo mchafu,nikawa nimepata ujasiri wa ajabu sana,nikaamua niende niufungue tu mlango nimkamate maya na kumfungia huko huko chumbani kwake,halafu niende kule chumbani kwa bro Ally mpemba nikaangalie yule msagane(Farah) aliweka nini kisha nisubirie kitakachotokea maana haiwezekani niwe muoga kiasi hiki wakati nilitahiriwa bila ganzi wala nusu kaputi.Huyo mnyama umughaka nikajivisha ukomandoo na kuanza kuuelekea mlango wa nyumba,wakati nimekaribia kabisa kuufikia mlango nikasikia sauti za makelele ya maya zimekoma na kumekuwa na ukimya wa ajabu sana kana kwamba hakuna kilichotokea nikabaki nimeduwaa nisijue cha kufanya.Nikaamua tu nirudi kule kwenye Audi yangu niwashe AC nilale,kitu msichokijua wapenzi wasomaji licha ya kuwa mpenzi mkubwa wa soka vile vile mimi ni mpenzi mkubwa sana wa AC kiasi kwamba kuna kipindi hata sasa hivi nikiwa naendesha bodaboda huwa nalazimika kwenda dukani kwa Ally na kumlilia aniruhusu niingie kwenye ile Range yake ili japo nipate starehe ya AC hata kwa robo SAA tu jamani
Nikaiendea ile Audi yangu na kuufungua mlango kijasiri kabisa eti nikakuta ile shuka bwana aimo,nikaingia ndani na kuwasha AC kisha mwanaume nikalala huku nikifikiria kesho niende kule kwa kiheli nikamdorishie hili liaudi langu halafu baadae niende kule kwa yule muuza juice ninywe juice ya 20000 ili nione kama atanikubali haraka na mimi nijilie mzigo bwana kwani sh ngapi
Itaendelea
Thanks again 😍. Jana sikuwa onlineMbele kabisaaaa Bantu Lady Pendaelli kitalembwa Lovelovie Saint Anne mafian Cartel Restless Hustler Wigelekelo Doctor G National Anthem moneytalk Joannah Santos06
Masta kaharibu hukuuuuuu kavunja mashartiiuuuu ni anakitombesha hatareeeeee😎😎!
Story inakolea na skepticism kibao ila watu wanajadili ujinga tu. Mpeni moyo mwandishi hata kwakujadili angle tamu za story yake na jinsi inavyo shift unpredictable.
Bro ecko sana Omughakha kazi unapopiga mzee naona utata unaozalisha kwenye story na unahtaji majibu nakuongeza utamu
1. Demu mpya kaflash kwenye story[emoji3]
2. Duka wiki nzima alijafunguliwa wewe uliona lipo wazi hii ni kona pia ya story tumebak skeptical kusubiri what next
3. Farha kaingia ndani kwa kaka ake na uliambiwa asiingie[emoji16][emoji16]what next ....inatupa hamu ya kujua
4. Umeshindwa hakiki kama Maya ndiye Farha
5. Maya kagoma kula ...utamu unazidi kukolea
6. Simu ya mshikaji wako...kamaindi
Tumekaa paleee tunasubiri uhondo...kesho sabato mzee mwenzangu utatushushia 1 moto ili sabato iwe njema.
Bravo
Master hanaga uswahiliiii Leo anashusha kitu!!Mambo bado bila bila hapa tukutane j3
Usijareee Nitakuita mkuuMbna mm hauniiti...
Watu wamekazana kutukana. Story imepangwa vizuri plot twist za hatari hata mtunzi angekua fundi vipi asingeweza kuipanga hiviStory inakolea na skepticism kibao ila watu wanajadili ujinga tu. Mpeni moyo mwandishi hata kwakujadili angle tamu za story yake na jinsi inavyo shift unpredictable.
Bro ecko sana Omughakha kazi unapopiga mzee naona utata unaozalisha kwenye story na unahtaji majibu nakuongeza utamu
1. Demu mpya kaflash kwenye story[emoji3]
2. Duka wiki nzima alijafunguliwa wewe uliona lipo wazi hii ni kona pia ya story tumebak skeptical kusubiri what next
3. Farha kaingia ndani kwa kaka ake na uliambiwa asiingie[emoji16][emoji16]what next ....inatupa hamu ya kujua
4. Umeshindwa hakiki kama Maya ndiye Farha
5. Maya kagoma kula ...utamu unazidi kukolea
6. Simu ya mshikaji wako...kamaindi
Tumekaa paleee tunasubiri uhondo...kesho sabato mzee mwenzangu utatushushia 1 moto ili sabato iwe njema.
Bravo
Watu wamekazana kutukana. Story imepangwa vizuri plot twist za hatari hata mtunzi angekua fundi vipi asingeweza kuipanga hivi
Kama ni ya kutunga. Umughaka is the best
Ujuaji wa kijinga labda pesa zilitakiwa kushikwa na mtu anaemlisha yule mwanamke wa kihindiUjuaji
Ngulyati nulu Nyakabindi, uli mahe bhageshi ?Karibu Simiyu
Ngulyati nulu Nyakabindi, uli mahe bhageshi ?
Sasa hiv hata unitagmasai dada shosti njooo
Yani tunaisubiria kwa hamu episode 22 nahivi Ally mpemba kafuraaa sijui itakuaje!!Jamaani umughaka akiweka 22
Naomba tag