Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani - 07.
Kwakuwa Mwakisaka ndiye aliyekuwa mwenyeji wangu sikuwa na hofu kabisa kwasababu ni mtu ambaye tulifanya nae kazi kwa muda mfupi na alikiwa mtu mwema,baada ya kufika kivukoni(feri)tulikata tiketi za kivuko na tukawa tumefanikiwa kuvuka ng'ambo ya pili,baada ya kufika upande wa pili yaani Kigambo,jamaa aliniambia inapaswa tupande gari zilizokuwa zinaelekea Kibada kwa kuwa ndiyo njia yenyewe hiyo.
Tulifanikiwa kufika hapo kwenye mradi mkubwa kabisa uliofahamika kama DEGE ECO VILLAGE,kiukweli nilikuwa nashangaa sana namna ambavyo watu wanatumia fedha,ule mradi ndugu zangu ulikuwa mkubwa mno,na kwa waliobahatika kufika huko au wanaotokea huko watakubaliana nami.
Hatukutaka kupoteza muda kabisa ilibidi Mwakisaka aniambie tuulizie namna ya kupata kibarua kwasababu tulikuta watu wakiwa wanachakalika kinoma.Kuna jamaa tulimfuata tukaanza kumuulizia namna ya kupata kibarua siku hiyo.
Jamaa "Hapa kwetu yupo foreman ambaye ndiye msimamizi wetu,ukienda kule mbele pia wanae foreman wao"
Mwakisaka "Foreman wenu yuko wapi tujaribu kuongea nae?"
Jamaa "Nadhani atakuwa anazungukia maeneo anayosimamia,subirini tu hapa atakuja"
Tulisogea kando tukawa tunaendelea kuushangaa ule mradi wakati huo tunamsubiri mtu tuliyeambiwa ndiye foreman wa hapo tulipofikia.Baada ya muda wa nusu saa jamaa mmoja mweusi aliyekuwa mnene na kitambi cha kutosha akawa amekuja na ndipo yule jamaa alitukonyeza ya kwamba jamaa ndiye foreman wa lile eneo.Tulimfuata na kumjulia hali jamaa kisha Mwakisaka akaanzisha maongezi nae.
Mwakisaka "Kaka tunatafuta kazi ya kibarua "
Foreman "Aliyewaambia hapa tunaajili vibarua nani?"
Mwakisaka "Hakuna mtu aliyetuambia kaka tumekuja kuona kama tutapata"
Foreman "Hapa hatuajiri kwa sasa,siku tukiajiri vibarua mtapata taarifa"
Baada ya yale majibu ya kukatisha tamaa Mwakisaka aliamua akae kimya kisha jamaa akaanza kuondoka kuzunguka nyuma ya yale majengo yaliyokuwa mbele yetu.Sasa yule jamaa aliyekuwa kibarua pale akawa amemuita Mwakisaka akamwambia bila pesa ni ngumu sana kupata kibarua kwasababu hata wao walihonga ndipo kupata kibarua,jamaa akasema twende tukaongee nae kikubwa.Nilimwambia Mwakisaka hiyo kazi ya kuongea na jamaa aniachie mimi,akikataa basi tungerudi zetu kwa Mushi kule kivule kuendelea na ufyatuaji wa tofali.
Niliamua kuzunguka ule upande alokuwa amekwenda yule foreman na bahati nzuri nilimuona akiwa anaingia kwenye jengo moja,nilitembea kwa haraka ili kumuwahi kabla hajafika kwa watu wengi ikawa shida kuzungumza nae.
Mimi "Kaka kakaa"
Foreman "mmmh nambie"
Mimi "Kaka tusaidie ndugu yangu na kama ni chochote tutakupatia"
Foreman "Wewe si ndo upo na yule mwenzio nimewaambia hamna kazi!"
Mimi "Kaka tusaidie ndugu yangu!"
Foreman "Nyie mnatokea wapi?"
Mimi "Wote tunatokea kivule"
Foreman "Kivule?,sasa kivule hadi kuja kufanya kazi huku hamuoni tutasumbuana?"
Aliendelea "Ni bora hata mngekuwa hapa maeneo ya jirani"
Mimi "Tutaweka kambi maeneo haya kaka wala hilo lisikupe taabu"
Foreman "Hapa jirani haturuhusu watu kukaa kwasababu za kiusalama"
Mimi "Sijamaanisha hapa kwenye mradi kaka,tuta tafuta eneo maeneo ya jirani tutaweka kambi"
Foreman "Tukubaliane,mtanipa elfu tano tano kila siku kwa muda wa wiki moja"
Aliendelea "Na iwe siri,ikiwa vinginevyo mi nitawaruka na kuwageuka"
Mimi "Hakuna tazizo kaka"
Foreman "Kamuite mwenzio mje niwakabidhi huku juu!"
Niliondoka kumfuata Mwakisaka na kumueleza kila kitu jamaa alichosema na jamaa akaniambia hakuna tatizo;Tuliondoka kumfuata yule foreman ambaye alituchukua mpaka kwa jamaa wengine akamuacha hapo Mwakisaka kisha akaniambia tena nifuatane nae,mimi pia akawa amenipeleka kwenye kikosi kingine.
Tukaanza kuifanya kazi ya kibarua rasmi na kwa siku tukawa tunapewa elfu 15,ishu ya kula pamoja na maji ya kunywa ilikuwa ni juu ya yako wewe kibarua uzuri ni kwamba,kwenye kundi ambalo mimi nilikuwepo walikuwa wamejitolea kuchanga fedha na kununua vyakula kisha kuna mtu walikuwa wanamlipa anakuja kuwapikia,hivyo na mimi baada ya kuingia kwenye kundi la wale jamaa niliamua kuchangia elfu 10 kwa kila wiki kwa ajili ya huo mpango.
Miongoni mwa wale jamaa pia walikuwa wametengeneza matenti ya maturubai kuishi hapo maeneo ya jirani,niliamua kichangia fedha na mimi ili kukaa hapo,sasa bahati nzuri ni kwamba wikiendi tulikuwaga tunapumzika na hiyo niliitumia kwenda kufata virago vyangu kwa kaka Kileri na kurudi kambini,sikutaka kabisa kuhangaika na mambo ya jiji la Dar es salaam,fokasi yangu ilikuwa ni kwenye kufanya kazi na kutunza malipo yangu kwenye simu.
Nilipopambana ndani ya miezi mitano kwenye ule mradi nilipata kiasi kisichopungua Tsh milioni 1.3,sasa nilimuomba Mwakisaka aniambie ni eneo gani ni zuri kwa kupanga chumba na angalau linakuwa na maisha nafuu kwa hapa Dar es salaam.
Mwakisaka "Mwanangu mimi nakaa Gongo la mboto na nikuzuri sana"
Mimi "Kwahiyo kipindi kile ulikuwa unatoka Gongo la Mboto mpaka Kwa Mushi?"
Mwakisaka " Nilikuwa nakaa kulekule kivule kwa ndugu yangu mmoja"
Aliendelea "Kama unataka chumba we sema nimpigie simu jamaa mmoja pale kitaa akutafutie chumba"
Mimi "Nahitaji kaka"
Mwakisaka "Basi ngoja nitamcheki mshikaji"
Kweli,baada ya Mwakisaka kuwasiliana na jamaa yake na kumjulisha nilikuwa nahitaji chumba jamaa alianza kutafuta na akasema endapo angepata basi angetujulisha.
Baada ya siku tatu yule jamaa aliyepewa kazi na Mwakisaka ya kutafuta chumba akawa amesema nyumba imepatikana maeneo ya mwisho wa lami lakini ni vyumba viwili ambavyo malipo ilikuwa ni elfu 45 kwa kila chumba na ilipaswa kulipwa kwa miezi 6.
Mwakisaka "Jamaa anasema nyumba imepatikana Gongo la mboto mwisho wa lami"
Mimi "Mwisho wa lami ni maeneo ya wapi?"
Mwakisaka "Hapo hapo Gongo la mboto sema ni mbele kidogo"
Mimi "Sawa,na wewe ndiyo unaishi huko?"
Mwakisaka "Hapana,mimi naishi Mzambarauni"
Mwakisaka "Ila jamaa anasema amepata chumba na sebule kwa elfu 45 kwa kila kimoja na inalipwa miezi 6,vp?"
Mimi "Sawa,hakuna tazizo"
Mwakisaka "Ngoja nimwambie amwambie mwenye nyumba atulie kesho kutwa tukakicheki"
Mwakisaka aliwasiliana na yule jamaa akawa amemwambia amwambie mwenye nyumba jumapili tungeenda kukitazama ikiwezekana nilipie kabisa.
Namshukuru Mungu baada ya kwenda kuingalia ile nyumba niliipenda na nikawa nimelipia miezi sita,hela iliyobaki nikanunua godoro na mashuka nikawa nimeyaweka na mimi kufunga chumba kisha kurudi Kigamboni kuendelea na kibarua.
Kila nilipokuwa ninapata hela nilikuwa nikinunua kitu kimoja baada ya kingine na kuweka ndani na hatimaye vyumba vikawa na muonekano mzuri,kiukweli pamoja na mateso ya kushinda juani niliyokuwa nayapitia kule kigamboni lakini nilihakikisha najinyima kiasi kwamba hadi malengo yangu yatimie.
Ule mradi wa Dege kuna muda ukawa umesimama kidogo hivyo kwa muda ule nikaenda kukaa kwangu nilikokuwa nimepanga,sasa pale nilipokuwa naishi kulikuwa na geti na tulikuwa wapangaji kadhaa na kila mtu alikuwa na ishu zake.
Sasa kuna jamaa mmoja alikuwa akiitwa Steve yeye tulitokea kushibana sana na tukawa marafiki,jamaa alikuwa akifanya kazi kampuni ya Tigo kama msajili line za simu,kwakuwa ule mradi ulikuwa umesimama kwa muda usiojulikana,jamaa aliniambia kama vipi aniunganishe na timu leader wake anipatie kodi ya kusajili line za simu nami nianze kuwa msajili laini.Jamaa aliniambia ni kazi ambayo ilikuwa na pesa sana ila watu walikuwa wakiichukulia poa.
Steve "Ngoja kesho nitamueleza team leader kama vipi akupe kodi ili uanze kufanya kazi"
Mimi "Kazi inafanyikaje kaka"
Steve "Kazi ni nyepesi sana kaka utaelekezwa namna ya kuifanya"
Kwakuwa kwa muda huo sikuwa na kazi baada ya kusimama kwa mradi,niliona jamaa atakuwa amenisaidia sana ili kuweza kujinasua na ukata ambao ulikuwa ukininyemelea baada kuwa nakula hela nilizokuwa nimezitunza bila kuzizalisha.
Itaendelea.........
Muendelezo Soma
Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani