bayona_stories
Member
- Apr 19, 2023
- 77
- 124
Mwanaume ameoa mke wake. Wakagombana. Mke wake akamwambia. Na kwa taarifa yako hata hawa watoto sio wa kwako. Wana watoto sita. Mwanaume akaona hizi ni hasira tu.
Ila baada ya muda fulani hili jambo likamuingia moyoni. Likamsumbua sanaaa. Akaona inawezekana ni kweli, maana watu Huongea ukweli wakiwa wamekasirika. Yaani ukitaka kujua mtu anawaza ubaya gani juu yako, wewe mkasirishe, ndo utajua kumbe amewahi hadi kujaribu kukuwekea sumu kwenye chakula na hukujua.
Basi mwanaume akaona kuliko aendelee kuteseka akilini bora aende tu hospitali kufuatilia Aliwachukua watoto wote sita kupimwa DNA zao.
Wakapimwa katika hiyo hospitali kuanzia mtoto wa kwanza mpaka wa mwisho. Ni heri basi angekuta hata watoto wanne au watatu au wawili au hata mmoja ni wa kwake. Watoto wote hawakuwa wa kwake. Hakuwepo hata mmoja Hakuiamini hiyo hospitali akaamua hadi kwenda nje ya nchi hospitali tatu tofauti lakini kote majibu yakawa ni yale yale. Watoto wote sio wa kwake.
Can you imagine?