Hivi mtu unaweza kusubiri kusimuliwa kama jua litachomoza au litazama? tangu mtoto wa kike anaanza kukimbia kimbia anaanza kuambiwa maneno ya kutongozwa (hey mchumba..!) na anapoanza kuota manyonyo ndio kabisa, na akianza kupata balehe ndiyo inakuwa ugomvi.. haijalishi msichana anakuambia au hakuambii ukweli ni kuwa atatongozwa akienda sokoni, akienda kanisani, akikaa darasani, akipita ofisini n.k
Mtoto wa kiume hivyo hivyo naye atatongoza hata migomba alimradi imekaa kimapenzi mapenzi..
so that given; mwisho wa siku ni uamuzi wa mtu kukataa au kukubali. Mwanamke utatongozwa kila wakati na kila mahali hata ujifanye mkali kama simba; lakini unayo nguvu yakukubali au kukataa. Ukikubali au ukikataa yote yanakuhusu wewe zaidi lakini yana gharama kubwa kwa mwenzio; na mwanamme vile vile.. unaweza ukaamua kumtongoza fulani au kutomtongoza au kukubali kutongozwa na mtu au kutokutongozwa lakini uamuzi wowote una gharama kwako na kwa mwenzio.
Mwisho wa siku (sijui kama ni siku ile ile!) tafuta na upate mtu atakayekupenda na ambaye kwake wanaume/wanawake wengine wote hawafui dafu. Kama unaye ambaye anazidiwa na mtu mwingine basi utajiunga katika ile clabu ya "wale"..