Utajuaje gari iliyofunguliwa na kitengenezwa Engine.

Joasi

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2014
Posts
766
Reaction score
674
Habarini.

Mwezi Huu mwishoni Nataka kutafuta hiace ya Hali Nzuri bila kuagiza starti langu ni gari isiwe imeguswa kwenye Engine, gearbox na vitu vingine.


Naomba kuelewesha Baadhi ya vitu.
(1) utajuaje gari iliyoguswa engine
(2) gearbox
(3)iliyo rudiwa rangi


Nb: nampango nikiipata nimtafute fundi aikague but Kuna changamoto, Wamiliki wengi wanafahamiana na mafundi So NAHITAJI NIPATE UJUZI KUTOKA KWA WADAU.

ASANTE.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tafuta fundi magari na muamini nia yako hiyo na umweleze, baadae tafuta gari yeye mjulishe ili muwe wote wakati analikagua,mfanye nae kama vile mnamiliki pamoja hapo utakuwa umewashinda hao wanotaka kukuuzia.
 
Angalia mfuniko wa cylinder head. Kama umefunguliwa kurudishia lazima ule mfuniko utakuwa umewekwa cylinder gasket mpya pamoja na Silicone ambayo itakuwa inaonekana.
Pia unaweza chukua spana kujaribu kufungua nati za cylinder head. Nati ambayo ilishafunguliwa itafunguka moja kwa moja. Ila kama haijawahi itafunguka kwa kushtuka kama vile unavyofungua soda ya pladtick kwa kukata seal.
 
Changa agiza japan ,utanunua mkweche na kushinda gereji kuliko barabarani.
 
Inategemea unanunua kwa mmiliki yupi.wapo wamiliki wengine wanajali sana gari zao.lakini hizi za sisi waafrika Haya ukiikagua na fundi WA kibongo itakula kwako. nakushauri Agiza kutoka nje tu.
 
Binafsi nakushauri tafuta gari taratibu bila kupewa presha na madalali au wauzaji ambao wanakwambia mimi nimeamua tu kuipaki, cha msingi ukipata gari kuwa serious anza kukagua Body kwanza yaani usiangalie namba sijui D, C, B ila A sikushauri maana kidogo kianzia B kuendelea zina hadhi yake, binafsi mimi nilinunua Hiace Mkononi mwezi wa5 lkn mpk sasa napeta nayo, nakula50 daily bila hofu, tena ingekuwa naendesha mwenyewe ningekuwa naweka hata80 kwa siku, muhimu kagua
1-Body rangi kama haijarudiwa, 2-Mlango kama unafunguka na kufunga vyema
3- Buti kama inafunga bila kuacha uwazi
4- Kagua siti wasikwambie hizo utashona tu
5-Washa gari sikiliza mlio wa injini kwanza na fungua sehemu ya injini angalia mtetemo wa injini na gari kwa ujumla, hakikisha unafungua mfuniko wa Oil huku gari ikiwa silence uone kama oil itamwagika au lah!
6- Test kwa kuendesha huku angalia ulaini wa steering
7- Check gear kama zinaingia kiulaini au mpk uotee na kama kuna mkwaruza wakati wa kubadili gear
8-Sikilizia mlio wa Diff maana nyingine zinavuma kwaajili ya kuisha kwa bearings
NB, tembeza gari ikiwezekana nenda hata kilometa3 hasa njia za mlima na vumbi na ikiwezekana speed, na upande mlima hata na 5 utashusha angalau mpk3 bila abiria kwa mlima mkali na sio2 au1

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu nakushukuru Sana. But pia Nataka kufanya demo ya kuagiza ili kupima mfuko Kama utatosha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu nakushukuru Sana. But pia Nataka kufanya demo ya kuagiza ili kupima mfuko Kama utatosha.

Sent using Jamii Forums mobile app

Habarini tena.

Nimepata wazo LA kuagiza hiace from Japan but Sina uzoefu .



Naomba kujua mchanganua iwapo hiace itakuwa imeingia Tz.

(1) tofauti na taxe payment hapo ni vitu gani vingine nitatakiwa kuvilipia.
(2) na Kama Kuna gharama nyingine tafadhali Naomba kueleweshwa Kwa wazoefu WA kuagiza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Attachments

  • Screenshot_20180822-183347.jpg
    59 KB · Views: 45
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…