Utajuaje kama umeonewa?

supasonic

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2012
Posts
356
Reaction score
309
1. Baada ya kufanya kazi siku 30, unafukuzwa kazi bila mshahara

2. Ukiwa una download kitu kwenye net, inafika 99% alafu inagoma

3. Unaingia na kibomu kwenye pepa halafu unashindwa kuelewa mwandiko wako mwenyewe

4. Unanunua simu Leo tsh elfu sabini halafu kesho zinawekwa kwenye promo zinauzwa elfu thelathini

5. Unamualika Demu mkali kwenye dinner unaagiza samaki alfu mwiba wa samaki unakukaba kooni

6. Unakamata manzi alafu unazama nae getoni halafu unashindwa kusimamisha

7. Unavunja uhusiano na boyfriend Wako halafu siku inayofata ananunua gari aina ya vogue ya shilingi milioni 90

8. Unanunua pafyumu kali lakini kwapa bado linatema

9. Unafanya kazi kwenye kampuni miaka 10 bila kupandishwa cheo na kuongezewa mshahara

10. Unamdanganya mkaba roba kuwa huna simu alafu inaita..

11. Unagombana na mtu barabarani halafu kufika ofisini unapokwenda kuomba kazi unamkuta anakufanyia interview

12. Kama gari lako linatumia muda mwingi gereji kuliko barabarani

13. Kwenye pepa matokeo yanatoka umefeli mathematics na kiswahili pia!!!

14. Unaingia kwenye pepa alafu unasahau jina lako la kwanza

15. Unasajiliwa kama beki kwenye timu ya barani ulaya alafu jaribio la kwanza unapewa kumkaba Lionel Messi

16. Kama mtoto Wako wa pekee anajiunga na JWTZ

17. Kama ukikosea ukaweka super glue machoni badala ya dawa ya macho

18. Kama utapiga picha photoshop lakini bado unaonekana mbaya

19. Kama panya atakula jina lako tu, kwenye Cheti chako muhimu

# Kati ya zote ipi ikitokea unakua umeonewa sana??

Sent using Jamii Forums mobile app
 

namba sita na namba kumi mkuu,dah
 
upo kwenye chumba cha mtihani pembeni yako amekaa kichwa wa darasa halafu msimamizi anamuondoa

hayo maumivu bora uachwe na demu
Msimamizi amesimama pembeni yako halafu unasikia anasema someni maswali vizuri huku muda umebaki kidogo na wewe umekaribia kumaliza mtihani.
 
Unataka kureply ila unakuta kuna MTU kashawahi!![emoji2] [emoji2] [emoji3]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…