Asalamaleko
JF-Expert Member
- May 10, 2015
- 2,699
- 7,726
Tuendelee kuwekana wazi Wazazi walezi na vijana. Miaka michache nyuma ilikuwa kwenda kusoma chuo ni kama "Geti" la mwisho kuingia ktk ajira za serikali. Ilikuwa ukimaliza Certificate Diploma au Degree haizidi miaka 2 unapata ajira serikalini na hata ktk taasisi na makampuni binafsi.
Nakumbuka watu walikuwa wanapata kazi serikalini na kuna baadhi ya kada ilikua unaitwa kazini bila hata kufanya interview, na ilikuwa unaweza kukataa kwenda ukaghairi hadi baada ya mwaka au zaidi na ukafanikiwa kupata tena nafasi ya kazi.
Nakumbuka pia ilikuwa unaweza kupangiwa kituo cha kazi mfano Dodoma vijijini au Kagera huko migombani au Tabora Arusha Dsm Mwanza au Mbeya, lakini ulikuwa na uwezo wa kugoma kwenda ukalazimisha uende mkoa unaotaka wewe au wilaya na ukaleta kila aina ya vurugu lakini utakubaliwa ombi lako huku unachekewa chekewa tu.
Kada ya Ualimu na Afya ndiyo ilikuwa raha zaidi unaweza pangiwa kituo cha kazi ukaenda ku-report kazini unalipwa pesa ya kuripoti na mshahara unaanza kuingia kila mwezi na wakati huohuo unaamua kuaga hata kwa mdomo ofisini kwamba unaenda kubeba mizigo iliyobaki nyumban kwenu au kubeba familia utarudi baada ya siku 14, lakini hurudi miezi hata 3 inapita lakini mshahara unaingia kama kawa.
Nakumbuka ilikuwa baada ya kufanya kazi mwaka unaweza kufanya vurugu kulazimisha upewe ruhusa ya miaka 2 au 3 uende ukaongeze elimu chuo, unafanikiwa kupata hiyo ruhusa au hata usipofanikiwa ulikua unaweza kuondoka tu kwenda chuo lakin mshahara unaendelea kuingia kama kawa.
Nakumbuka kuna watu baada ya kwenda kujiendeleza na kumaliza chuo diploma au degree hawakurudi ktk vituo vyao vya kazi wakaomba kazi mikoa au wilaya nyingine na kuanza kupokea mshahara mpya na wakat huo huo mshahara wa zamani unaingia.
Nakumbuka ilikuwa kwenda kazini ni kwakujisikia unaweza singizia umefiwa hata na mbwa au ng'ombe ukaondoka kazini siku 3 hadi wiki, nakumbuka ilikuwa watu wanaingia kazini muda wanaojisikia wao... Kiukweli nakumbuka mengi jinsi watumish wa umma walivyo ichezea serikal na walivyo chezea kazi zao na mishahara yao.
LAKINI MIAKA YA HIVI KARIBUNI HASA KUANZIA 2015 ajira zimeota mbawa zimepaa juu anapofikia "Mwewe" sasa kupata ajira ni sawa na kuiona pepo, sasa kupata ajira hata ya kuzibua choo ni big deal na inahitaji connection haswa...
Ukweli ni kwamba idadi ya wasomi inaongezeka kwa kasi sana wakat idadi ya nafasi za kazi zinapungua kwa kasi kubwa zaidi.
Ukweli ni kwamba pamoja na serikal kujitahidi kutanua wigo wa ajira kwa kukaribisha private sectors na miradi mbalimbali lakini bado soko la ajira ni dogo.
Ukweli ni kwamba elimu yetu bado inaendelea kutuaminisha maisha ni kusoma na kuajiriwa.
Ukweli ni kwamba kusoma vyuo vya ufundi bado jamii yetu inaona mtu anayesomea vyuo vya fani mbalimbali za kutumia mikono ni kupotea kimaisha wakati ukifumbua 3rd Eye huko ndipo kwenye fursa kwasasa.
Jamii ina amini kuvaa shati na kuchomekea na tai shingoni (white color job) kukaa kwenye kiti cha kuzunguka ofisi nzuri huko ndio kufanikiwa kimaisha na ajira.
WAZAZI WALEZI NA VIJANA mtake msitake, tukubali kwamba habari za kuajiriwa zimeisha zimepotea na zimepitwa na wakati na kufa kabisa.
Hivyo Wazaz tuwaandae watoto wakiwa wadogo wajue wanasoma shule na vyuo ili waje kujiajiri wakubali kusumbua akili zao zifikiri namna gani ya kujikwamua kiuchumi kwa kujiajiri.
Mzazi Mlezi Kijana kama nyumban kuna mradi wa kufuga au kilimo au biashara kubali kutumia fursa hiyo kujua ABC's za namna gani shughuri hiyo inaendeshwa ili kesho na kesho kutwa uweze kufungua mradi wako kwa utaalam zaidi.
Elimu bado iendelee kuwa kipaumbele ktk jamii kwa namna yoyote ile kila familia ione mtoto anapozaliwa ni haki yake kupata elimu. Lakini pia serikal iendelee na juhudi za makusudi kuboresha elimu, turudi kuboresha zaidi ile misingi na sera ya "Self Reliance Education" ya Mwl Nyerere.
Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojoia, pamoja na taasisi zote za kiserikali zinazo deal na elimu ziheshimiwe zipewe uzito na zipewe watu wenye Vision and Mission ya kusimamia elimu.
Viongozi wa kisiasa wasijiamulie juu ya elimu ni vizuri mabadiriko yoyote kuhusu elimu wadau wa elimu na jamii wahusishwe kutoa mawazo na mijadala iwe wazi.
Vijana msipokubaliana na uhalisia mkakaa nyumban mkingoja kuajiriwa mtakufa kwa stress madawa ya kulevya na kujiingiza ktk ngono za jinsia moja ili upate pesa za mserereko ambazo mwsho wake ni mauti.
Serikal na Mashirika binafsi ni wakati sasa kuwamotisha watanzania wote wanaochukua hatua ya kujiajiri maana ni fursa ya kufungua ajira nyingi na kukua kiuchumi.
Mheshimiwa Mtanzania, naomba kuwasilisha.