Utakiona cha mtema kuni!, Kama ni hadithi , ilikuwa kwenye kitabu gani? Mtunzi alikuwa nani...na mengineyo....

Sometimes tunatumia msemo: utakiona cha mtema kuni.
Msemo huu ulianzia wapi? Mtemakuni aliona nini?
 
ninavyojua huo msemo una asili ya Wasukuma/Wanyamwezi,,,,,,,,,na hilo neno Mtema linatokana na neno Mtemi, ,,,, na mana halisi ya neno hilo Mtemi ilikuwa ni Mkataji, mkata mashauri, mkata kesi kwa hivyo "utakiona cha mtema kuni" ina maana utakiona cha mkata kuni,,,,,,,,,,,,,,, swali lako nadhani bado halitakuwa limejibiwa sawasawa kwani hata mimi pia nina shauku ya kujua kilichompata mkata kuni
 
Sometimes tunatumia msemo: utakiona cha mtema kuni.
Msemo huu ulianzia wapi? Mtemakuni aliona nini?
Kwa mtazamo wangu ulianzia huko TB/SHY/MZA.. neno la kiuhasama na la kitisho ! kama alivyo nena member kituko.
 
Sometimes tunatumia msemo: utakiona cha mtema kuni.
Msemo huu ulianzia wapi? Mtemakuni aliona nini?
Mtema kuni ndiye aliyeona kilichomng'oa kanga manyoya ya shingoni, alipokuwa msituni akikata kuni. Hadi leo mtema kuni hajisimulia ni nini haswa kilichotokea siku hiyo!
 

Ni thnread ya zamani kidogo ia umenifurahisha ulipo taja wahusika ktk hivyo vitabu.
 
Nashukuru sana ndugu yangu, si haba, iatabidi niende BAKITA pia kujiridhisha.
Hapa inaoneka wengi wetu huwa tuna tumia misemo tusiyojua asili yake!

Japokuwa ni kitambo kirefu, Najua bado upo jamiiforums. Hebu niambie BAKITA WALIKWAMBIJE?
 
Mmmmhhh... Hii ni kweli?
 
Last edited by a moderator:
Duh kweli kusoma kwingi ni kujua mengi,hili neno ukweli nalitumia sana lkn sijui ht sababu wala maana ila nashkuru nimepata maana ht ya mtema kuni,ikiwa na maana ya mkata kuni,big up wana jf
 
Sasa nimegundua kuwa yooote hayo majitabu kutoka ughaibuni ni facade ,ukweli watu wana hamu ya hadthi na visa vyetu asilia!swali tunaanzia wapi kukata kiu hii?
 
Habri za asubuhi wadau!?

Naomba kuelewa chanzo hasa cha hiyo kauli "... cha mtema kuni". Je hiyo ilikuwa ni hekaya au nini hasa?

Na kama ni hekaya kama zilivyo za Abu nuwasi, je Kitabu chake kinaetwaje ili nijue ni nini hasa kilimpata huyu mtema kuni hadi leo huwa tunatishwa kukiona alichokiona mtema kuni.
 
Hahaaa mi mwenyewe huwa natamani kujua huyu mtema kuni alikiona nini hadi imekuwa historia ya miaka yote??
 
Mtema kuni ni mkata kuni. Inahadithiwa kuwa kulikuwa na mtu mmoja aliyekwenda kukata kuni msituni. Wakati wa kukata,alijeruhiwa na kipande cha mti aliokuwa akiukata vibaya sana. Ikasemwa kuwa,kuni zimemrudi mkataji. Yaani,kuni zimelipa kisasi kwa kuwaka hasira.
 
nilishawahi kusimuliwa kisa (hadithi) hiki cha mtema kuni nilipokuwa mdogo lakini kumbukumbu nzuri sina.

Rafiki yangu DEMBA jitahidi kuweka kumbukumbu bhana!! Wanao utawasimulia nini!!
 
Last edited by a moderator:

Asante Petro kwa kunipa mwanga kidogo...
Nadhani hizi ni moja ya hadithi zetu za kiafrica ambazo nyingi hazijawa documented popote na matokeo yake zimeshakufa na kusahaulika!
 
Last edited by a moderator:
Hapo unachanganya mambo kidogo. Msemo mzima ni: utakiona cha mtema kuni kilichomng'oa kanga manyoya ya shingoni.

​Suala zima hapo ni nini haswa kilichomng'oa kanga manyoya ya shingoni? Hicho ndio alichokiona mtema kuni alipokua anakata kuni huko msituni!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…