Utakiona cha mtema kuni!, Kama ni hadithi , ilikuwa kwenye kitabu gani? Mtunzi alikuwa nani...na mengineyo....

Dah......Kwa hisani ya Google..... C & P
UTAKIONA CHA MTEMA KUNI!" Nimeambiwa msemo huu wahenga waliupata katika kisa kimoja cha zama za kale.
Wanasema kulikuwa na msitu jirani na kijiji, ndani ya msitu kulikuwa na miti mingi sana. Ilitokea kuwa katika msitu ule, kulikuwa na miti inapishana sana kwa uzuri, na kati yao ulikuwepo ule ambao ni mzuri sana!
Mtema kuni (Mtemakuni maana yake ni Mkatakuni) alienda katika msitu ule katika shughuli zake za kila siku za kukata kuni!
Alipofika jirani na ule mti mzuri, huku akiwa na shoka mkononi, ule mti zuri sana ulikuwa jirani na mti mbaya sana!
Katika hali ya kufedhehesha (kwa nyodo na maringo) ule mti mzuri sana ukawa unamcheka na kumdhihaki ule mti mbaya, kwamba hauna mvuto na ndio maana kuanzia mbali kabisa, Mtemakuni amaonyesha kuvutiwa na (yeye) Mti mzuri! Huku Mtemakuni akizidi kuusogelea mti mzuri, mti mbaya sana ukajifariji kwa kumwambia mti mzuri basi subiri "utakiona cha mtema kuni"


Kilichofuata ni kweli, Mtema kuni aliukata na kuucharanga Mti mzuri sana kiasi cha kuugeuza kuni za kumfaa kubeba na kuondoka nazo, huku akiuacha ule mti mbaya salama salmini pale msituni!
Yakawa ni majuto kwa Mti mzuri na furaha kwa Mti mbaya!
Hivo ndio nilivyopokea kisa cha "mtema kuni"



UJUMBE WAKE KWA JAMII
πŸ‘‡πŸ½
mnaodhani mna uzuri wa sura punguzeni maringo na nyodo!
 
Write your reply...ni abunuwasi,alikua anakata kuni huku amekalia tawi analolikata,kilichomkuta sasa....
 
Mtema kuni bwana alisumbua sana,kilichompata mpaka Leo siri yake
 
do! itoshe kusema nimekubali
 
Mtema kuni ni mkata kuni ! Alijifanya mjuaji akapanda mtini kukata tawi kavu juu akiwa amelikalia ! Lo ghafla likakwanyuka akaenda nalo chini na lika mtoboa tumboni na kumuacha na jeraha kubwa !!! Wakati akikata pia kibanzi kilimuingia jichoni ! Maskini mtema kuni ! Just stories but we learn from it....
 
Hii simulizi imetungwa na mtu asiyejua kabisa kilichotokea. Kwa taarifa yako ''mtema kuni'' ndiye aliyepatwa na kisa na si mti. Kwa kifupi hadithi inasema mtema kuni alienda porini na alipokuwa anakata mti kuna kitu kilimtokea, akatupa shoka lake na kuanza kutimua mbio. Kuna baadhi wanasema lilitokea joka kubwa likaanza kumfukuza na wengine wanasema mti ulianza kuzungumza ukimlaani mtema kuni hivyo akakimbia kwa kihoro cha ule muujiza. Miaka ya nyuma wakati gazeti la Uhuru likiwika hasa kwenye safu ya Ushairi hili swali liliwahi kuulizwa na mshairi mmoja gwiji na magwiji wenzake walimjibu. Kuna mshairi mmoja mlemavu asiyeoona akiitwa Andanenga (Sauti ya Kiza) naye alikuwepo kwenye mjadala! Ulikuwa ni mjadala mzuri sana ila sikuweza kufuatilia ili nijue jibu lililokubaliwa na wengi. Ila la msingi ni kuwa mtema kuni ndiye aliyepatwa na masaibu na siyo mti kama simulizi yako inavyosema.
 
hahaA hiyo aya ya mwisho dahh
 
Niliwahi kusikia kisa kama hicho nadhani ndo chenyewe
 
Sijawahi kujuta kujiunga jamii forum

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…