Old story
JF-Expert Member
- Jul 21, 2018
- 2,264
- 2,152
Hizi ni stry za wazee wetu ila nao hawajui kisa ni nn hapa moja kwa moja ni kurithishana tu
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
wanasema utakipata cha mtema kuni hapo iaonyesha victim alikuwa mtema kuniDah......Kwa hisani ya Google..... C & P
UTAKIONA CHA MTEMA KUNI!" Nimeambiwa msemo huu wahenga waliupata katika kisa kimoja cha zama za kale.
Wanasema kulikuwa na msitu jirani na kijiji, ndani ya msitu kulikuwa na miti mingi sana. Ilitokea kuwa katika msitu ule, kulikuwa na miti inapishana sana kwa uzuri, na kati yao ulikuwepo ule ambao ni mzuri sana!
Mtema kuni (Mtemakuni maana yake ni Mkatakuni) alienda katika msitu ule katika shughuli zake za kila siku za kukata kuni!
Alipofika jirani na ule mti mzuri, huku akiwa na shoka mkononi, ule mti zuri sana ulikuwa jirani na mti mbaya sana!
Katika hali ya kufedhehesha (kwa nyodo na maringo) ule mti mzuri sana ukawa unamcheka na kumdhihaki ule mti mbaya, kwamba hauna mvuto na ndio maana kuanzia mbali kabisa, Mtemakuni amaonyesha kuvutiwa na (yeye) Mti mzuri! Huku Mtemakuni akizidi kuusogelea mti mzuri, mti mbaya sana ukajifariji kwa kumwambia mti mzuri basi subiri "utakiona cha mtema kuni"
Kilichofuata ni kweli, Mtema kuni aliukata na kuucharanga Mti mzuri sana kiasi cha kuugeuza kuni za kumfaa kubeba na kuondoka nazo, huku akiuacha ule mti mbaya salama salmini pale msituni!
Yakawa ni majuto kwa Mti mzuri na furaha kwa Mti mbaya!
Hivo ndio nilivyopokea kisa cha "mtema kuni"
UJUMBE WAKE KWA JAMII
👇🏽![]()
mnaodhani mna uzuri wa sura punguzeni maringo na nyodo!
Siku hizi umekuwa unashirikisha ubongo kuleta uzi wako umeacha zile takataka ulizotoka nazo fbAman iwe nanyi wapendwa
Ni siku nyingi sana huwa nasikia kisa cha mtema kuni
Je mtema kuni ni nani?
Je aliwahi kuwepo au tu ni story za kutunga?
Kitu gan kilimpata huyu mtema kuni?
Kwa kifupi naomba kujua kisa na mkasa mzima wa mtema
Maana huwa naona mtu ukifanya kosa unaambiwa utakiona cha mtema kuni hivyo bas naomba kujua mkasa huu
Nawasilisha
London boy
Sent using Jamii Forums mobile app
Amri Sudi mzee wa 'Nyege ni kunyegezana'Hii simulizi imetungwa na mtu asiyejua kabisa kilichotokea. Kwa taarifa yako ''mtema kuni'' ndiye aliyepatwa na kisa na si mti. Kwa kifupi hadithi inasema mtema kuni alienda porini na alipokuwa anakata mti kuna kitu kilimtokea, akatupa shoka lake na kuanza kutimua mbio. Kuna baadhi wanasema lilitokea joka kubwa likaanza kumfukuza na wengine wanasema mti ulianza kuzungumza ukimlaani mtema kuni hivyo akakimbia kwa kihoro cha ule muujiza. Miaka ya nyuma wakati gazeti la Uhuru likiwika hasa kwenye safu ya Ushairi hili swali liliwahi kuulizwa na mshairi mmoja gwiji na magwiji wenzake walimjibu. Kuna mshairi mmoja mlemavu asiyeoona akiitwa Andanenga (Sauti ya Kiza) naye alikuwepo kwenye mjadala! Ulikuwa ni mjadala mzuri sana ila sikuweza kufuatilia ili nijue jibu lililokubaliwa na wengi. Ila la msingi ni kuwa mtema kuni ndiye aliyepatwa na masaibu na siyo mti kama simulizi yako inavyosema.
Ni nini kilimpata?Mtema kuni si mtu mzuri kwani hakuwa na bahati. Alipenda sana kukata miti hovyo. Siku moja alipokuwa akitembea kando ya mto, akaona mti mzuri sana. Kama kawaida hakuwa akiacha shoka. Akapanda juu ya mti ili aanze kukata matawi taratibu. Alipokuwa juu ya mti ghafla akaona joka kubwa likikenua ulimi, hajakaa sawa akaona nyuki wakiwa kwenye mzinga. Wakati anawaza kushuka, Hamadi! Akaona chini kuna simba amelala anamsubiri[emoji23][emoji4] akataka arukee mtoni, akakutana na mamba amefungua mdomo tayari kwa kitoweo. Sema alichokiona ndio kilibaki historia hadi leo
Jr[emoji769]
😀 😀 😀 😀
Ni nini kilimpata?