Utakubali kumwachia fundi kifaa ambacho amekwambia hakifai tena kupona?

Utakubali kumwachia fundi kifaa ambacho amekwambia hakifai tena kupona?

LA7

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2019
Posts
655
Reaction score
2,369
Kulingana na muda mchache huu nilioingia kwenye sekta ya ufundi Kuna vitu kadhaa nimejifunza

Mfano juzi Kuna mteja aliniletea pasi baada ya kuikagua nikagundua ile pasi yake haifai Tena kupona kwani ilipiga shoti ikaua mpaka hita lakini ile pasi ilikuwa Bado nzuri kwa bodi lake

Baada ya kumwambia mteja kuwa haifai Tena mteja Wala hakuwaza akaniambia Baki nayo tu utatoa spea hapo.

Na mwingine aliniletea tv nch58 ilikuwa inawaka tu mwanga mweupe tatizo lilikuwa kioo baada ya kumwambia mteja ugonjwa wake na jinsi ilivo ngumu na gharama kubwa kuponyesha basi baada ya kumpigia simu yule mteja na kumjulisha akaniambia nibaki nayo tu Kama spea.

Sasa Kuna wateja hata kitu ambacho hakifai kabisa yeye anakwambia urudishie tu akakitupie ndani au awape watoto wachezee na utakuta labda pengine ameshaenda fundi zaidi ya Moja na shida akaambiwa hiyo hiyo

Au unaweza kwa mfano tv nch3 iliyokufa kioo mafundi huwa tunanunua kiasi kisichozidi 40 sasa unakuta mteja anakwambia umpe laki akithaminisha na Bei aliyonunulia dukani ikiwa nzima halafu anakwambia eti si ni kioo tu ndo kibovu.

Je? Wewe huwa unafanyaje fundi akikwambia hicho kifaa chako hakifai Tena kupona.
IMG_20250101_174731_955.jpg
IMG_20250101_174629_293.jpg
IMG_20250101_174651_507.jpg
 
Attachments

  • IMG_20250101_174731_955.jpg
    IMG_20250101_174731_955.jpg
    553.1 KB · Views: 4
Hao wateja wanakuamini ndio maana. Endelea kujenga trust kwenye kazi yako mkuu.

Mi nikiwa kazini watu wakileta gari mfano service, kuna spare wakibadirisha utasikia wanakuambia iyo used baki nayo tu. Na wakati me naweza muuzia mtu akija na gari ambalo kigaa iko iko kimekufa kabisa.

Kikubwa usiharibu trust kwa hao wateja.
 
Hili linategemea na uhusiano kati ya mteja na fundi.

Kuna mafundi ni waaminifu na wastarabu kwa namna ambavyo anakuhudumia ikitokea Jambo kama Hilo inaweza kuacha kifaa atumie kama spare

Lakini Kuna mafundi ni wajeuri na wenye vuburi afu pia waongo waongo hawa ni kina mafundi maiko.

Hawa Huwa siwezi kuwaachia hata msumari uliopinda nabeba
 
Kama naweza mudu kutengeneza sikuachii
Maana yake mkuu mfano tv umenunua milioni 1 halafu ukaambiwa kioo ni laki8 sio kwamba haiwezekani ili ni lazima ushirikishe na ubongo wako kwanza
 
Pengine nanyi mafundi acheni janja janja. Kikibaki kitu used hapo kwako, unakuja kukitumia kwenye matengenezo mengine tena kwa kumuhadaa bosi umemuwekea spare mpya.
Mkuu mbona vitu used ndo mara nyingi huwa imara zaidi mfano wa kioo kilichokkuja na simu au mfano Kuna seapiano bufa ic zikifa ukiweka mpya hazitadumu Ila ukapata zilizokuwa kwenye sakiti nyingine Toka kiwandani ukiweka zitadumu
 
Je? Wewe huwa unafanyaje fundi akikwambia hicho kifaa chako hakifai Tena kupona.
Mimi nilirekebisha radio ambayo mafundi km 8 walisema imekufa mwenye radio mpaka leo ananiona km nina kipaji cha pekee sijaenda kusoma ufundi veta wala sina degree ya electronics na sielewi chochote kilichopo kwenye radio sijui chochote kuhusu umeme ila nilisoma physics form 1 mpaka 4, mafundi wale 8 wote degree holder wakaanza kunizengea mimi nianze kuwapa somo just imagine mtu ana degree huko ya mechanics sijui kasoma chuo gani fundi mchundo anakuja kunizengea mimi ambae ukiniuliza transistors ni nini sijui haya mambo mengine ni akili tu sio kwamba ufundi sijui kufanya nini

Nakumbuka nilipokua mdogo standard 6 I think kuna feni moja ya mzee alipeleka kwa mafundi wakaishindwa wote nikaja mimi siku hio nina shida ya feni mzee ananiambia nenda store kule kuna lifeni limoja mafundi wamelishindwa emu angalia km utaweza kulitumia mimi nikaingia store nikalichukua lile lifeni nikalifumua nikalichokonoa mpaka likazunguka ila nilichoshindwa ni kucontrol speed maana lilikua linatembea speed 1 tu ile ya juu nikiliwasha km una ngiri usikae karibu na hilo feni utamwamsha ngiri, ufundi ni utundu tu
 
Kama gharama ya kutengeneza ni kubwa kulingana na thamani ya kifaa husika na hakuna dhamana yeyote kua kifaa hicho kitafanya kazi kama kilivyokua,unamuachia tu fundi ili achukue spare awatengenezee na wengine wafaidike,

Ni sawa tu na kudonate organ ili mwingine nae apone,

Ni vizuri zaidi kua na fundi mmoja uliyemzowea kuliko kuhama hama,

KIngine,mafundi muwe waaminifu tu,
uaminifu ni moja ya siri kubwa sana katika mafanikio kwenye maisha.
 
  • Thanks
Reactions: LA7
Ishu kubwa ni uaminifu wako na wateja wako, binafsi simuamini fundi maana asilimia kubwa ni janjajanja nyingi hivyo siachi kitu naondoka nacho kitanifaa mbele ya safari kama spea
 
Mimi kwenye gari nina fundi wangu mmoja tu huyo akisema tatizo ni engine au fuse sijui plug basi nakubaliana nae tu. Huyu fundi hata nipeleke gari anatengeneza kwa hela yake yeye atanipigia na kusema bei ya jumla spare+labor. Nikifika nampatia hela yake au namrushia kwenye simu tu.

Zamani nilikuwa na fundi mwengine huyu mwamba nilimuamini sana sababu mtoto wa mtaani. Lakini uhuni alionifanyia nimemtoa kwenye list ya mafundi wangu.

Mimi nina mafundi 3 wawili wakisema tatizo hilohilo basi nasikilizia huyu wa 3 atasemaje akisema jengine narudi kwa wale 2 wa mwanzo.

Kuna fundi alitaka kushusha engine akisema kuna part imetoka kwenye engine. Na gari ndio kwanza mpya, kumpelekea fundi wangu ninae muamini alisema wiring ndio tatizo na kweli alifix hilo tatizo mpaka leo gari ipo poa tu.
 
Sema ufundi ni utundu utundu na kujiongeza, sometimes nawapa mafundi kazi Ili nisipoteze muda ila nikisema niamue kutengeneza mwenyewe natengeneza safi kabisa.
Hamna utundu utundu kaka bali ni kuamua kujifumza na kila kazi unakuja na changamoto yake hata uwe fundi masta lazima ikuumize kichwa
 
Hamna utundu utundu kaka bali ni kuamua kujifumza na kila kazi unakuja na changamoto yake hata uwe fundi masta lazima ikuumize kichwa
Utundu ninaosema si wa watoto, bali ni "curiosity". Nikijua "A" nitataka kujua Hadi "Z". Huwa nacheka ninapomuona fundi akinipigia hesabu zake za uongo na kweli, by the way heshimu kazi za watu.
 
Utundu ninaosema si wa watoto, bali ni "curiosity". Nikijua "A" nitataka kujua Hadi "Z". Huwa nacheka ninapomuona fundi akinipigia hesabu zake za uongo na kweli, by the way heshimu kazi za watu.
Huyo anakupigia hesabu za uongo ww ndo utakuwa shida kawaida ww unayetoa kazi inatakiwa kwanza umwamini fundi halafu ndo akupe gharama za kazi,

Shida Kuna kitu watu wengi hawaeliwi wenyewe hufikiria tu jinsi ya kifaa kilichobadilishwa wanasahau Kuna kujua au kutambua ugonjwa wa kitu ndo kazi kubwa kuliko hata tiba yenyewe,

Ukitaka Mambo yaweza rahisi wewe nenda na kifaa halafu ukifika Anza kumwelekeza chomoa hiki weka hiki toa na kile niweke hiki

Hakika haitazidi 5000 Ila uwe umeshafungua kila kitu.
 
Kulingana na muda mchache huu nilioingia kwenye sekta ya ufundi Kuna vitu kadhaa nimejifunza

Mfano juzi Kuna mteja aliniletea pasi baada ya kuikagua nikagundua ile pasi yake haifai Tena kupona kwani ilipiga shoti ikaua mpaka hita lakini ile pasi ilikuwa Bado nzuri kwa bodi lake

Baada ya kumwambia mteja kuwa haifai Tena mteja Wala hakuwaza akaniambia Baki nayo tu utatoa spea hapo.

Na mwingine aliniletea tv nch58 ilikuwa inawaka tu mwanga mweupe tatizo lilikuwa kioo baada ya kumwambia mteja ugonjwa wake na jinsi ilivo ngumu na gharama kubwa kuponyesha basi baada ya kumpigia simu yule mteja na kumjulisha akaniambia nibaki nayo tu Kama spea.

Sasa Kuna wateja hata kitu ambacho hakifai kabisa yeye anakwambia urudishie tu akakitupie ndani au awape watoto wachezee na utakuta labda pengine ameshaenda fundi zaidi ya Moja na shida akaambiwa hiyo hiyo

Au unaweza kwa mfano tv nch3 iliyokufa kioo mafundi huwa tunanunua kiasi kisichozidi 40 sasa unakuta mteja anakwambia umpe laki akithaminisha na Bei aliyonunulia dukani ikiwa nzima halafu anakwambia eti si ni kioo tu ndo kibovu.

Je? Wewe huwa unafanyaje fundi akikwambia hicho kifaa chako hakifai Tena kupona.View attachment 3190126View attachment 3190127View attachment 3190128
Eeh Me huwa nawaachia, sasa kubebana na matakatakaa ya nini au nami nataka kuja kuwa fundi
 
Ila trust nzuri sana asee,hapa kwangu nina tv kama tano hivi za 50" nimeachiwa mbili zina shida ya taa zingine vioo, ila najua one day yes nitaziamsha.

Kuna mama mmoja mkuu wa idara fulani ofisini aliwahi kunipa laptop yake inashida miaka minne iliyopita kipindi sina vifaa vya kisasa vya kufanyia maintenance, siku naenda kumkabidhi alinishangaa sana kwani alishasahau, toka moyoni akanipa kama zawadi na zingine mbili zilizoitaji ufundi kidogo tu.
 
Back
Top Bottom