Utakubali kumwachia fundi kifaa ambacho amekwambia hakifai tena kupona?

Utakubali kumwachia fundi kifaa ambacho amekwambia hakifai tena kupona?

Mafundi wa bongo utawajua ni pale wanapobonda bonda kifaa ili kukichomoa. Angalia fundi anavyochomoa beling utatamani aache.
Mafundi wa bongo ni wahatibifu.
UFUNDI SIO UTUNDU NI UJUZI NA UTAFITI. Utundu ni kufanya kitu bila kujua unachofanya. Achenii habari ya utundu someni na fanyeni tafiti kutatua matatizo.
Acheni kutengeneza vitu kwa kuharibu
 
Huyo anakupigia hesabu za uongo ww ndo utakuwa shida kawaida ww unayetoa kazi inatakiwa kwanza umwamini fundi halafu ndo akupe gharama za kazi,

Shida Kuna kitu watu wengi hawaeliwi wenyewe hufikiria tu jinsi ya kifaa kilichobadilishwa wanasahau Kuna kujua au kutambua ugonjwa wa kitu ndo kazi kubwa kuliko hata tiba yenyewe,

Ukitaka Mambo yaweza rahisi wewe nenda na kifaa halafu ukifika Anza kumwelekeza chomoa hiki weka hiki toa na kile niweke hiki

Hakika haitazidi 5000 Ila uwe umeshafungua kila kitu.
Inawezekana wewe ni fundi lakini huwajui mafundi wengi wa hapa TZ jinsi walivyo, wengi wao si waaminifu na hupenda sana pesa. Si uungwana kuelekezana kusimamiana kama wahindi kwenye kazi ya mtu ambayo ameifanya Kwa muda na ndo inalisha familia yake. Mimi ninachokifanya kama fundi simjui vizuri, namuambia hichi kitu kimekufa kitu Fulani badilisha niwekee kipya na blah blah za hapa na pale Ili asihisi kama namfundisha kazi, basi muda mchache tu mambo yamefaa, halafu hesabu haiwi ndefu, nachukua naondoka. Hata Kwa mafundi ujenzi pia ni muhimu kujua au basi uwe na idea Ili mshauriane jinsi ya kufanya lakini usimfundishe kazi.
 
Back
Top Bottom