Utakufa siku si zako...

mapipando

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2015
Posts
2,922
Reaction score
3,559
Wasalam,

Kumekuwa na hii kauli "utakufa siku si zako" ambayo husemwa kwa mtu pengine mwenye tabia ambayo si ya kukubalika katika jamii,mfano wizi,tamaa,uzinzi,sifa za kijinga, nk nk.

Ama "amekufa siku si zake".

Swali la msingi hapa ni kwamba,wewe unaesema fulani kafa/atakufa siku si zake umetoa wapi huo uwezo wa kujua kuwa anapaswa kufa siku gani???

Ukizingatia binadam hatujui siku wala saa ya kufa kwetu,kifo hakichagui mchanga,kijana wala mzee,sasa iweje wewe binadam mwenzangu uanze kusema flan kafa ama atakufa siku si zake???
 
ni kama onyo tu..kukumbusha ulifanyalo si jema na linaweza kukusababishia kifo mapema.
kijana ana uwezo wa kuishi maisha halal ya haki na akaishi hata uzeeni....kaamua kuwa kibaka kadakwa kacharangwa mapanga.hapo si kafa kabla ya siku zake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunarudi pale pale kwamba kama kafa siku si zake una maanisha unazijua siku zake za kuishi,ni sawa na kusema jamaa kachelewa ama kawahi ili hali hujui mda wake wa kufika.
 
vifo vingine vya kujitakia ujue.. unaambiwa mke wa mtu sumu! wewe unasema geto lina maziwa, siku wakikubamba na mke wa mtu wakakuua.

hapo ndio tunarejea kwenye mada. "utakufa siku si zako"
Mkuu kumbuka hakuna aina moja ya kifo,wala hakuna anaejua atakufaje,na kama hujui utakufaje pia hujui mwenzako atakufaje sasa wawezaje mwambia mtu mwingine atakufa siku si zake??
 
Nakubaliana na wewe mkuu.

Tuko pamoja, kama siku haijafika utatwangwa risasi zaidi ya 30 hautakufa, ndege itapata ajali utapona peke yako, jengo litalipuliwa wakati huo unaweza hata ukawa na udhuru usiwepo eneo la tukio.

Lakini kama siku imefika, hata kama umelala utarudi mavumbini tu, utapita eneo lenye taharuki risasi itapinda kona na kukutafuta wewe tu, utapelekwa hospitali bora kuliko zote duniani na mauti itakufika tu.
 
Dhambi ndio huleta kifo kabla ya muda wako.yaani utajikuta ulienda sehemu ambayo sio sahihi na muda ambao sio sahihi ukakumbwa na kifo hivyo usiende na wadhalimu na watenda uovu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dhambi ndio huleta kifo kabla ya muda wako.yaani utajikuta ulienda sehemu ambayo sio sahihi na muda ambao sio sahihi ukakumbwa na kifo hivyo usiende na wadhalimu na watenda uovu

Sent using Jamii Forums mobile app
Dhambi?? yawezekana ikawa ni kweli lakini vipi kuhusu watoto wadogo wapotezao maisha,nao ni dhambi?
 
Kudos mkuu,Tundu Lissu's a vivid example.
 
Tuna maneno ya ajabu sana

Sent from my SM using Tapatalk
 
Huwa wànaangalia Sana vile vifo ambavyo man himself can control,sasa ukishindwa kuji control ili walau usogeze siku za kuishi basi matokeo yake utakufa siku si zako,mfano unaambiwa ili mwili wako uwe na kinga madhubuti ya kujikinga na maradhi fanya mazoezi,badae ukapuuza matokeo yake utakufa siku si zako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…