Utakuwa unakatiwa simu mara nyingi, usipozingatia haya unapopiga simu kwa wateja (kwenye sales)

Utakuwa unakatiwa simu mara nyingi, usipozingatia haya unapopiga simu kwa wateja (kwenye sales)

Maka99

Member
Joined
Aug 9, 2024
Posts
7
Reaction score
6
Imekuwa kawaida kwa watu wa call center

Kutoka taasisi mbali mbali kupiga simu kwa wateja

Hasa pale taasisi inapoamua kufanya sales kupitia kupiga simu.

Tunajua sales is a game of number sio?

How many calls you make per day, give you reflections to your sales volume.

Kama hujui haya mambo, basi somo la sale linakuhusu.

Tuendelee, sasa inapotokea taasisi ikapanga kupiga simu, kwa ajili ya kampeni yoyote iwe bidhaa mpya, au elimu fulani kwa wateja.

Kuna changamoto kubwa ya wale wanaopiga simu kukatiwa simu zao na wateja, kabla hata hajamaliza kuongea.

Hii changamoto hutokea kwa sababu huzingatii mambo yafuatayo-:

1. MUDA/TIME
Hiki ndio kitu cha kwanza kuzingatia ukitaka kufanya sales kwa kupiga simu, lazima uje na projections za je simu itapokelewa? Ikipokelewa tutazungumza?. Sasa wewe unapiga simu sa 8 mchana wakati unajua hapo ni muda wa chakula cha mchana.

2. KEY WORDS.
Hapa ni ile sentensi unayotakiwa kuanza nayo. Lazima uje na sentensi ambayo ni "powerful" kumfanya mteja avutike kukusiliza, pia sentensi hiyo inatakiwa kuwa kwenye mfumo wa "story telling"
A: Napiga simu kutoka kampuni X, tunajishugulisha na bima 😡
B: Tunambua usalama wako unalindwa na sisi, na tumekupigia simu hii kukukumbusha kwamba......

3. TONE/VOICE( SAUTI)
Trust me, moja ya kitu kitakachofanya uuze zaidi kwenye calls, ni sauti yako. Sauti itamfanya mteja aendelee kukusikiliza au aache. Zingatia utulivu, matamshi, kusikika, na kutobana sauti.

4. JITAMBULISHE
Ni muhimu ili mteja ajue anazungumza na nani. Anza kujitambulisha kwa jina, cheo, na taasisi unayofanya kazi.

5. PRESENTATION/WASILISHA
Unataka kuzungumza nini? Kuna offer? Ni elimu tu? Ni taarifa? Ni taahadhari? Kama ni offer basi usiache taarifa yoyote kuhusu offer hiyo, ili kupunguza maswali kwa mteja.

6. OMBA RUHUSA YA KUZUNGUMZA NAE.
Kuna kampuni watu wake wa sales wanahitaji elimu sana aisee, yani mtu anapiga simu moja kwa moja anaanza kuzungumza, "napiga simu kutoka kampuni X, tuna kifurushi kipya cha nini na nini, ukilipia leo unapata bonus.." hujui mteja ana mood gani, yupo eneo gani, au ana msiba ..🚨

7. MPE NAFASI YA KUULIZA MASWALI
Ikitaka kuwa good salesman, lazima uwe na closing words kali sana.

Sales, customer care, service management & digital marketing consultant

CONTACT 0757996880
 
Back
Top Bottom