Utakwendaje mbinguni wakati unaishi dunia iliyotawaliwa na dhambi?

Utakwendaje mbinguni wakati unaishi dunia iliyotawaliwa na dhambi?

Frumence M Kyauke

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2021
Posts
630
Reaction score
1,262
Ikiwa mbinguni/peponi wanaingia watakatifu! Tujiulize swali hili kuwa mtu atakwendaje mbinguni wakati anaishi dunia iliyojawa na dhambi?

Tunatumia vitu vingi vinavyopatikana kwa njia zisizo sawa kama watu wa imani wanavyodai.

Inawezekana mtu akajihisi anatenda mema na ni mchamungu lakini anatumia condom au anakopa na kukopesha wakati mikopo inasemekana ni haramu?

Vipi mtu anayehisi ni mchamungu lakini akanunua nyama iliyopatikana kwa njia haramu pasipokujua? Vipi mtu anaejihisi ni msafi na akajikuta amenunua shamba lililozulumiwa yaani mhusika aliuawa ndipo akauziwa pasipokujua?

Je, vipi mtu anaejihisi ni mchamungu na akanunua mavazi yaliyopatikana kwa njia haramu?

Mtu atavukaje dhambi zote hizi ikiwa kila suala linalomzunguka linamlambisha dhambi?
 
Dhambi ni pale unapomfanyia mwenzako au jirani yako mabaya tena kwa kukusadia na dhambi nyingine kumkufuru Mungu.
 
Sunghru anasema anaefikiria kuna maisha mazuri baada ya kufa ni mwehu. Maisha ni haya tu, jitahidi tu uishi vizuri, utapotea tu kama mdudu. Wazungu walitudanganya ili tufikirie tu kuhusu mbinguni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom