Ndagullachrles
JF-Expert Member
- Jun 20, 2023
- 256
- 259
Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi ni moja ya Hifadhi tano zilizopo mikoa ya kanda ya Kaskazini ambazo ni Tarangire ,Manyara,Arusha na Kilimanjaro .
Hifadhi hii ya mkomazi inaunganisha mikoa ya Kilimanjaro na Tanga ikiwa na ukubwa wa Kilometa za mraba 3245 ikiwa umbali wa Kilometa 112 kutoka Moshi mjini.
Mwaka 2008 Mkomazi ilitangazwa rasmi kuwa hifadhi ya Taifa na Sasa ni miongoni mwa hifadhi 21 zilizopo chini ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania(Tanapa).
Kivutio kikubwa katika Hifadhi ya Taifa mkomazi kwa Sasa ni utalii wa Faru weusi ambao ulianzishwa mwaka 2021 ukiwa ni moja ya mkakati wa kuongeza idadi ya Faru weusi ambao ni moja ya wanyama waliopo kwenye hatari ya kutoweka.
Kuanzishwa kwa utalii huu wa Faru kumeongeza idadi ya watalii wanaotembelea hifadhi hiyo kutoka watalii 3,000 mwaka 2021 hadi watalii 10,000 kwa mwaka kwa Sasa.
Kamishna msaidizi wa uhifadhi na mkuu wa Hifadhi ya Mkomazi, Eva Mallya anasema utalii wa Faru umekuwa moja ya vivutio vikubwa katika hifadhi hiyo .
Miundombinu rafiki ikiwamo viwanja viwili vya Ndege vya Kisima na Mkomazi vilivyojengwa kutokana na fedha za UVICO19 vimekuwa kichocheo kikubwa cha kufikika kirahisi kwa hifadhi hiyo .
Swala Twiga,Tembo,Twiga,Simba,Chui na Nyati ni moja ya wanyama wanaopatikana ndani ya hifadhi hiyo na wanaonekana kirahisi kwa wageni
Ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi mgeni anakuwa na machaguo mengi ya aina ya utalii anaotaka kufanya ikiwamo utalii wa mchana ,utalii wa usiku na utalii wa kutembea kwa miguu .
Uwapo Tanga mjini mgeni anatumia Kilometa 100 kuifikia hifadhi ya mkomazi kwani kilomete 60 ni lami na km 40 ni Moramu iliyotengenezwa kwa kiwango bora kuweza kupitika muda wote .
Utalii wa Faru weusi
Huu ni utalii ambao umeanza kulipa na kivutio cha kipekee kwa Sasa ni Faru kisima ,huyu ni Faru yatima ambaye mama yake akifariki na kumwacha akiwa na umri mdogo .
Ndani ya utalii wa Faru upo utalii wa kuasili Faru hasa Faru yatima kama Faru kisima kwa mgeni kugharamia gharama za Faru kuishi
Filam ya The Royal Tour na Amazing Tanzania
Mkuu wa Hifadhi ya Mkomazi ,Kamishina Msaidizi wa Uhifadhi ,Eva Mallya anasema filamu hizo chini ya Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan zimekuwa kichocheo kikubwa sana cha kuutangaza utalii wa Tanzania na vivutio vyake ikiwamo hifadhi ya mkomazi .
Anasema kuanzishwa kwa Tamasha la Utalii wilaya ya Same ,Same Utalii Fastival kumechochea kuwepo na mwamko mkubwa katika kuvutia watalii katika hifadhi ya mkomazi .
"Nichukue fursa hii kumpongeza sana mkuu wa mkoa wa kilimajaro ,Nurdin Babu kwa kutuletea timu hii ya waandishi wa habari katika hifadhi ya mkomazi ,tunaamini kupitia kwenu mkomazi inakwenda kuitangaza mkomazi kitaifa na kimataifa ",anasema mhifadhi Mallya.