Utalii wa ndani: Kundi la watalii wa ndani wapatao 500 watembelea hifadhi ya taifa Ruaha

Utalii wa ndani: Kundi la watalii wa ndani wapatao 500 watembelea hifadhi ya taifa Ruaha

IamBrianLeeSnr

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2022
Posts
2,010
Reaction score
4,179
Msafara wa watalii wa ndani wapatao 500 wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendegu wametembelea Hifadhi ya Taifa Ruaha iliyoko mkoani Iringa hivi karibuni kwa lengo la kuhamasisha utalii wa ndani na kuvutia wawekezaji ili wawekeze katika miundombinu ya utalii.

0EEFCDC7-87F0-4DB9-A790-CD030DB4802B.jpeg


Akiwa katika hifadhi hiyo yenye ukubwa wa Kilometa za Mraba 20,226 mkuu wa mkoa huyo amesema, “mtalii anapokuja Hifadhi ya Taifa Ruaha ategemee kuona mandhari nzuri, wanyama wengi wazuri na wa kuvutia wakiwa katika makundi makubwa. Nilikuwa na wasiwasi leo kutomuona Simba lakini imekuwa kama ‘surprise’ mwishoni tumemuona kwa ukaribu zaidi na hizo ndizo sifa za hifadhi hii.”

“Mbali na kuona wanyama kwa ukaribu na wakiwa katika makundi yao ya asili, pia nimefarijika sana kuona watanzania wengi wamejitokeza kuja kutembelea hifadhi. Niwahakikishie tu kuwa kwetu sisi kama mkoa tutakuwa na utalii endelevu na utalii huu wa ndani tulioufanya leo katika ni mwanzo tu” aliongeza Dendegu.

974C92AA-DE13-485C-A62C-C12D13387E4D.jpeg


Ziara ya watanzania hao kutembelea Hifadhi ya Taifa Ruaha imechagizwa kwa kiasi kikubwa na uhamasishaji wa utalii unaoendelea katika Maonesho ya “Utalii Karibu Kusini 2022” yanayoendelea mjini Iringa. Maonesho hayo yaliyoanza Novemba 09 na yanatarajia kutamatika leo Novemba 13, 2022.
 
Aiseee watu wa coaster wamepuga hela hapo
Dah! Weh acha rfk tupige hesabu za chapchap Dar to Iringa hapo mbugani Transport fee kwa coaster bus moja lk8 go and return correct me if am wrong sina experience sana kwenye hili.
 
Dah! Weh acha rfk tupige hesabu za chapchap Dar to Iringa hapo mbugani Transport fee kwa coaster bus moja lk8 go and return correct me if am wrong sina experience sana kwenye hili.
Hapo imekodiwa kwa 1mil maana hailali, na ilikuwa na escort toka Bandarini
 
Back
Top Bottom