Utalii wa ndani - Mikoa yote uhamasishwe kwa uzuri

Masalu Jacob

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2017
Posts
1,446
Reaction score
1,645
Habari Tanzania !

Hivi hatuwezi tukawa na uhamasishaji wa kujifanyia Utalii wa ndani aidha Wilaya moja kwenda nyingine au Mkoa mmoja kwenda mwingine. Tuboreshe utaratibu kwa kuweka mambo machache kwa kutozana bei ndogo tu ila pawe na masharti kadhaa.

Mfano wa hayo masharti:

1. Lazima ulale nyumba ya wageni;
2. Manunuzi yako yoyote yafanyike eneo husika hupaswi kubeba chakula au kinywaji;
3. Useme unatamani au unapenda kutembelea sehemu gani;
4. Utamlipa mwenyeji kiasi fulani cha pesa kwa huduma ya matembezi na ubebaji wa mizigo.
5. Hupaswi kuwq na usafiri wako binafsi hasa eneo ulilokusudia kulitembelea sharti ufanye kukodi usafiri eneo husika.

Cc
Wizara ya Utalii
Bodi ya Utalii
Bodi ya Filamu Tanzania
Wizara ya Sanaa na Michezo

NB

Mtaongeza mengine Watanzania. Asante.
 
Masalu hujambo? Unaelewa vizur kuhusu kutalii? Je unafahama utalii kadiri unavyokutana na mashart mengi ndivyo unavyozid kupungua?
 
Hii ni aina fulani ya kuufanya Utalii wa ndani uwe wa kitamaduni. Yaani hatutapunguza chochote isipokuwa tunaupa uthamani mkubwa na jamii ikishaupokea hata katika mazingira ya uelewa kuna kuwa na uzuri.
 
nafkiri ili kukuza utalii wa ndani wizara ya utalii sanaa na utamaduni wangeweza kwenye mtaala wa elimu yetu kuanzia ngazi ya msingi hadi chuo yaani watoto wetu waijue nchi vilivyo kitamaduni pamoja na vivutio vyake tena kwa vitendo kila mwaka kunakuwa na tour ya 2-3 day na hii inakuwa ni lazima.

Kuwe na kauli mbiu ya kuuhamasisha utalii wa ndani ikiambatana na mazingira wezesheshi pamoja na gharama nafuu kwa watanzania kuanzia hoteli mpaka viingilio vya sehemu husika ya vivutio.

fikra wezeshi, Elimu itolewe kwa upana wake kuhusu utalii na faida zake na wananchi waondolewe fikra kuwa utalii ni kwa ajili ya matajiri ama wazungu.

Zawadi, kuwe na bonus pamoja na zawadi kwa ngazi tofauti tofauti kwa watalii wandani watakaofanya documentary nzuri wakati wakifanya utalii wao, hapa wagawe zawadi kwa kuzingatia makundi kama vile wanafunzi, vijana, pamoja na wengine na kumtafuta mshindi wa jumla wa taifa. zawadi zinaweza kuwa kwenda kutalii kituo sehemu yoyote ya tanzania kwa gharama za bodi ya utalii kwa muda flani, pamoja na tuzo zingine.

Likizo, Taasisi za kiserekali na za kibinafsi zijengewe uwezo wa kuwapa likizo wafanyakazi wake kwenda kupumzika sehemu mbali mbali zenye vivutio vya kitalii badala ya kuwapa likizo wakati wa matatizo kama ugonjwa ama shida za kijamii kwa ujumla.

Mwisho lakini si kwa umuhimu ni aina za utalii, watalii wa ndani waeleweshwe na kujuzwa aina za utalii ambazo zitawavutia na kufanya chaguo sahihi. mfano utalii wa kilimo, matibabu, kutembelea mbuga za wanyama, kupanda mlima, kuogelea na kuzamia majini, au utalii wa vyakula vya kiasili pamoja na mambo kale.
 
Oooh hii ndugu Mtanzania ni nzuri sana. "Tunaweza tukianza sasa".
 
Back
Top Bottom