nafkiri ili kukuza utalii wa ndani wizara ya utalii sanaa na utamaduni wangeweza kwenye mtaala wa elimu yetu kuanzia ngazi ya msingi hadi chuo yaani watoto wetu waijue nchi vilivyo kitamaduni pamoja na vivutio vyake tena kwa vitendo kila mwaka kunakuwa na tour ya 2-3 day na hii inakuwa ni lazima.
Kuwe na kauli mbiu ya kuuhamasisha utalii wa ndani ikiambatana na mazingira wezesheshi pamoja na gharama nafuu kwa watanzania kuanzia hoteli mpaka viingilio vya sehemu husika ya vivutio.
fikra wezeshi, Elimu itolewe kwa upana wake kuhusu utalii na faida zake na wananchi waondolewe fikra kuwa utalii ni kwa ajili ya matajiri ama wazungu.
Zawadi, kuwe na bonus pamoja na zawadi kwa ngazi tofauti tofauti kwa watalii wandani watakaofanya documentary nzuri wakati wakifanya utalii wao, hapa wagawe zawadi kwa kuzingatia makundi kama vile wanafunzi, vijana, pamoja na wengine na kumtafuta mshindi wa jumla wa taifa. zawadi zinaweza kuwa kwenda kutalii kituo sehemu yoyote ya tanzania kwa gharama za bodi ya utalii kwa muda flani, pamoja na tuzo zingine.
Likizo, Taasisi za kiserekali na za kibinafsi zijengewe uwezo wa kuwapa likizo wafanyakazi wake kwenda kupumzika sehemu mbali mbali zenye vivutio vya kitalii badala ya kuwapa likizo wakati wa matatizo kama ugonjwa ama shida za kijamii kwa ujumla.
Mwisho lakini si kwa umuhimu ni aina za utalii, watalii wa ndani waeleweshwe na kujuzwa aina za utalii ambazo zitawavutia na kufanya chaguo sahihi. mfano utalii wa kilimo, matibabu, kutembelea mbuga za wanyama, kupanda mlima, kuogelea na kuzamia majini, au utalii wa vyakula vya kiasili pamoja na mambo kale.