Utalii Wazidi kukua Nairobi

Utalii Wazidi kukua Nairobi

Junior Clinton Mr.

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
1,075
Reaction score
1,423
=

THURSDAY, MAY 3, 2018

Hivi ndio Tanzania ilivyonufaika kwa ujio wa ndege kubwa za Airbus..

Airbus A380-800 iliyotua Dar na fursa za utalii

Ndege hiyo iliyokuwa na abiria 475 na wahudumu 27 ilishindwa kutua nchini Mauritius kutokana na hali mbaya ya hewa, hali iliyomfanya rubani wake kucha-gua kutua JNIA Hata hivyo, ndege hiyo iliyotua Aprili 25, saa 7 mchana, iliondoka kesho yake saa 2:15 asubuhi kuendelea na safari yake ya Mauritius.



Ghorofa ya juu ya A380 inachukua urefu wote wa umbo la ndege pamoja na upana wake.

Hiyo inaipa A380-800 eneo la mita za mraba 550 ya lile linalotumiwa na abiria, ikiwa ni asilimia 40 ya ndege inayo-fuatia kwa ukubwa ambayo ni Boeing 747-8 na ina viti vya abiria 525 katika vyumba vitatu.

Ndege hiyo ina uwezo wa kusafiri umbali wa kilomita 15,700 bila kujaza mafuta ikiwa ni ratiba ya pili kwa urefu wa safari duniani hadi kufikia Novemba 2017 na mwendokasi wa kilomita 900 kwa saa. Ndege ya A380-800 ilipotua Tanzania ilikunywa lita 98,000 za mafuta, lakini matanki yake yana uwezo wa kunywa lita 320,000 sawa na malori (tankers) tisa yakiwa yamejaa mafuta.

Hadi Machi 2018, Airbus inayotengeneza ndege hiyo ilikuwa imeshapokea maombi 331 kutoka taasisi na mashirika mbalimbali duniani, lakini imeshauza ndege za aina hiyo 223 ambapo Emirates inaongoza kwa kutuma maombi ikiwa imeshapata ndege 102 kati ya ndege 162 ilizoomba.

Ndani ya ndege

Ndege hiyo ina uwezo wa kubeba abiria 853. Ndani ya ndege hiyo ya kifahari kuna chumba cha starehe (lounge) kilichonakshiwa kwa kuta za shaba na mbao na viti vya sofa vinavyomwezesha mteja kustarehe wakati akipata vinywaji kutoka kwenye kaunta.

Kwa kuwa ni ndege ya safari ndefu, abiria akiamka asubuhi huenda bafuni kuoga na kujiweka sawa kabla ya kwenda kupata kifungua kinywa.

Katika vyumba vya daraja la kwanza abiria anakuwa peke yake akipata huduma zote ikiwamo vyakula na vinywaji huku akiangalia sinema na kama atachoka, anaweza kulaza kiti chake kikageuka kuwa kitanda.

Kwa wanaosafiri daraja la biashara, wanaweza kuendelea na kazi zao ikiwamo kuandika na kutuma barua pepe. Umeme upo wa kutosha kwa ajili ya kuchaji kompyuta mpakato na simu, huku abiria akijihudumia kwa vinywaji vilivyopo kwenye kabati lake pembeni. Vyakula vipo vya kutosha wakati wote wa safari na vinatolewa kulingana na mahitaji ya abiria.

Ukiwa angani si mwisho wa kuwasiliana, huduma ya intaneti isiyo ya waya (wi-fi) inapatikana wakati wote na abiria anaweza kuipata kwenye simu au kompyuta.

Uwezo wa Tanzania

Akizungumza hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Hamza Johari anasema licha ya kutua kwa nadra, JNIA una uwezo wa kuhudumia ndege hizo.

Anasema licha ya dege hilo kutua wakati mgumu ambao ndege nyingi hutua, walimudu kulihudumia na kuitumia kwa fursa za biashara.

“Ilikuja kwenye peak time (muda mgumu) kwa sababu kulikuwa na ndege nyingine zinakuja kama Emirates, Qatar, Ethiopia na nyinginezo. Kulikuwa na abiria zaidi ya 2,000 lakini tuliwasimamia vizuri. Kwenye hilo tukawa tumefanya biashara,” alisema Johari.

Aliongeza: “Baada ya kuondoka asubuhi walitaka kujaza mafuta, ndege ile inakunywa lita 320,000 lakini pale ilikunywa lita 98,000.

Vigezo na Vifaa

huduma muhimu zilizotumiwa na ndege hiyo ikiwamo mashine za ardhini za kuisukuma nyuma kabla haijaruka (pushback) na ngazi za kushuka na kupandia zinazotolewa kwa tozo maalumu, huku akitaja tozo ya kutua na kupaa kuwa Dola 320 mara mbili (zaidi ya Sh1.53 milioni).

Kuhusu vigezo vilivyozingatiwa hadi ndege hiyo ikaja Dar es Salaam, Johari anasema ni kutokana na ubora wa uwanja wa ndege, akisema ndege hiyo inahitaji njia ya kutua yenye urefu wa kilomita tatu na upana mita 60 hadi 75.

“Kulingana na ndege aliyonayo, rubani ataangalia ‘running way capacity’ (uwezo wa uwanja), JNIA una urefu wa kilomita 3.1 umezidi kidogo na upana wa mita 60,” alisema. Alitaja pia ubora wa mitambo ya uongozaji ndege inayomwezesha rubani kutua kwenye mistari maalumu bila kukosea na mifumo ya mawasiliano.

Vilevile, alitaja huduma ya udhibiti wa moto ambayo ipo kwa kiwango kinachotakiwa na ni namba tisa na ndicho kilichopo.

“Rubani pia anazingatia mitambo ya kutoa huduma za ardhini ikiwamo ngazi za kushukia abiria. Je kuna mtambo wa kuwashia? Wakati wa kuondoka kuna mtambo wa kuisukuma ndege nyuma? Anataka kujiridhisha na mtoaji wa mafuta (fuel farm),” anasema.

Kuhusu huduma nyinginezo, anataja hali ya usalama (safety maturity level) akisema kwa sasa imepanda kutoka asilimia 37.8 ya mwaka 2013 katika ukaguzi tuliofanyiwa na Shirika la Usafiri wa Anga Duniani hadi asilimia 64.35 mwaka 2017.

“Aviation security level’ tulipokaguliwa tulipata asilimia 83, hivyo tuko vizuri katika masuala ya usalama,” anasema na kuongeza kuwa hata kwenye operesheni wakiwemo marubani wa ziada pia wanapatikana.

Hata hivyo, anataja changamoto za kutokuwepo kwa mapokezi ya ghorofa katika uwanja huo, hivyo kushindwa kuwapokea abiria moja kwa moja kutoka kwenye ndege kuingia ndani ya jengo la abiria.

“Somo kubwa tulilojifunza ni kwamba tumepata kujiamini zaidi kwamba ndege kubwa tunaweza kuihudumia,” anasema.

Kutokana na kupanda hadhi hiyo, Johari anasema Rais wa Shirika la Usafiri wa Anga Duniani, Dk Bernard Alio atakuja Tanzania kutoa tuzo kwa Rais John Magufuli atakapoalikwa.

Johari pia alithibitisha kuteuliwa mwenyekiti wa Afrika wa Shirika la Kimataifa la Huduma za anga na Uongozaji wa Ndege, (Civil Air Navigation and Organization).

Manufaa mengine kibiashara

Mbali na uuzaji wa mafuta uliofanywa na kampuni ya Puma, Joharia anasema ndege hiyo ilileta neema kwa hoteli za nyota tano na nne za jijini Dar es Salaam ikiwa pamoja na Serena, Golden Tulip, Southern Sun na New Africa.

Baadhi ya wenye hoteli hizo walipoulizwa kwa njia ya simu hawakutaka kuzungumzia wateja wao wala biashara hiyo ya ghafla.

Hata hivyo, gharama ya chumba kwa usiku mmoja katika Hoteli ya Serena ni zaidi ya Sh500,000.

Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (Taa), Joseph Nyahade anasema japo bado hawajapiga hesabu za jumla, lakini ni wazi ujio wa ndege hiyo uliongeza mapato ghafla.

“Ile ni ndege kubwa na ilikuwa na abiria 475 kwa hiyo walikuwa wakihitaji huduma kubwa. Kama ni ngazi tuliwapatia, huduma ya usafi ilifanyika vizuri na zote hizo zinalipiwa. Sisi wenyewe kama mamlaka tulilipwa ada kubwa kulingana na ndege yenyewe, japo kwa sasa bado hatujapiga hesabu za mwisho,” anasema Nyahade.

Anasema mamlaka zote ikiwemo Idara ya Uhamiaji, Mamlaka ya Mapato (TRA) na hoteli zilizopata wageni ziliingiza mapato.

Mikakati ya utalii

Akizungumza na Mwananchi kuhusu ujio wa ndege hizo na fursa za utalii, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii (TTB), Devotha Mdachi anasema kuna mikakati kabambe inafanyika ili kuyashawishi mashirika makubwa ya ndege kutua Tanzania.

“Tunafanya mikakati kwa kushirikiana na viwanja vya ndege na kampuni za utalii ili kujitangaza na kualika watalii. Kwa mfano hii ndege ya Qantas kutoka Australia tumeshikiana na Kilimanjaro Airports Development Company (Kadco) na ndiyo maana wamefika,” anasema.

“Huwa tunahudhuria mikutano ya maonyesho ya utalii na huko ndiko tunakotangaza viwanja vyetu na vivutio vya utalii. Kadco wamechangia kwa kiasi kikubwa kuja kwa ndege za mashirika ya Qatar Airways na Emirates. Kuna wakati shirika la ndege la Israel liliwahi kuleta watalii 600 kwa siku moja, hayo ni mafanikio,” anaongeza Mdachi.
 
Bado sijaelewa utalii unazidi kukua Nairobi au dar es salaam naomba urudie tena kwenye kichwa cha habari
 
hahahahahahaha bado munasheherekea ndege.
 
Back
Top Bottom