Utamaduni mpya wa uchumi duniani umeshabadilika, tujiandae kisaikolojia kwenda nao na si kuganda kule kule

Utamaduni mpya wa uchumi duniani umeshabadilika, tujiandae kisaikolojia kwenda nao na si kuganda kule kule

Steven Joel Ntamusano

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2023
Posts
5,203
Reaction score
3,913
Vilabu vikubwa vya Ulaya vinamtangaza Emirates kila kukicha. Mechi inachezwa uwanjani na ukitazama yale mabango ya umeme yanayokatiza pembeni ya mstari wa uwanja huwezi kulikosa bango lenye sura za kinadada wazuri weupe wanaotangaza shirika hilo la ndege.

Kabla mechi hazijaanza au kabla ya matukio makubwa yanayorushwa dunia nzima kwenye viwanja vya mpira vya Ulaya huwa wanajipanga kinadada wazuri warefu na weupe wakiwa na mavazi ya shirika hilo la ndege, ni kwa makusudi ili dunia nzima iweze kujua nini kinaendelea kwenye sekta ya anga.

Mwarabu kaikamata biashara ya ulaya baada ya kupigwa vita nzito kule Marekani akipewa kesi nyingi za uongo ili akate tamaa na kuondoka. Akatua ulaya kwenye bara lenye uendeshaji wa biashara wa haki, ukiwa na kitu chenye kuonekana ni lazima utoboe. Ameendelea mwarabu kunawiri katika uwanja wa biashara wa haki barani humo.

Ulimwengu tunaoishi una utamaduni mpya wa kibiashara na haukwepeki ni kama mvua mwezi wa April hazikwepeki ni lazima zitanyesha sehemu fulani ya dunia. Kwa kimombo inaitwa NEW WORLD ECONOMIC ORDER. Ni hali ambayo inamuongezea uzee Joe Biden kule USA, kila Akitazama takwimu za kibiashara anakuta Marekani inamiliki asilimia 40 tu za Market Shares kwenye masoko yote ya hisa, nani mpinzani wake mpya?, ni mwarabu anayeongozwa na Al Makhtoum kiongozi mkuu wa UAE.

Anamnyima usingizi Mmarekani na kumpunguzia ushawishi wake wote unaozidi kupungua siku baada ya siku. Huu ni mfumo mpya wa dunia mpya na sioni ni kwa namna gani Tanzania itaweza kuepuka ushawishi huu unaovuma kwa kasi. Mwarabu anamiliki sekta zote kubwa za dunia hii na kwa sasa kaingia kwenye misitu, kiasi cha mtu kushangaa inakuwaje misitu ya Dodoma inamilikiwa na mwarabu?. Kakamata kila mahali nyeti duniani.

Kwenye sekta ya usafiri wa majini ndio balaa, anamiliki meli 400 za iliyokuwa P & O Nedlloyd kampuni kubwa ya shipping miaka michache iliyopita, anao ushawishi huko DRC, Congo na kwenye madini ndani ndani ya Afrika. Pia anao umahiri wa kufanya end to end logistics kwa miundo mbinu ya kisasa aliyonayo. Anao umahiri katika biashara ya Bandari kiasi cha kuendesha akiwa ni vigezo vyote vya kuwa INVESTOR PORT yaani anamiliki bandari kule kwao na wakati huo huo anazikodisha kila kona ya dunia hii.

Anao uwezo wa kushusha bei za bidhaa nyingi pale Kariakoo kwa kutenga meli zake 10 zikawa zinahudumia bandari ya Dar pekee, na kupunguza kwa kiasi kikubwa bei za bidhaa mbalimbali. Kitaifa naona ni vigumu kupinga huu upepo wa mwarabu anaokuja nao katika pwani ya afrika mashariki.

Anapachikwa majina mengi na taasisi za kidini kwa kigezo cha asili yake kwani hao wanaojaribu kumchafua ni mawakala wa utamaduni wa magharibi na kwa sasa upo katika hali mbaya tukizingatia kuwa Market Shares za USA zinakwenda zikipungua, magharibi na utamaduni wake anao mtihani wa kupata chanzo cha uhakika cha gas, mfaransa anapambana kila kukicha amuue rais mpya wa Niger ili alinde maslahi mapana ya utamaduni wa magharibi.

Mwafrika na rasilimali zake nyingi anaendelea kufanana na msichana mzuri anayevutia wanaume wenye pesa nyingi, anatazama tu wanavyomuhangaikia kwa mitindo mbalimbali ya kutaka kuuvuta moyo wake.
 
Point,Nimeanza kufwatilia siasa na kudadisi mambo ya kichumi 2014 nikiwa la 6 inaweza ikawa ajabu lakn ndo ukwel.Nina miaka takrban 10 nafwatilia mambo haya
Nikiangalia mkataba wa DPW na ufafanuz kutoka kwa wataalam mbalmbal mkataba ule unatija kubwa kwa taifa letu kama utakuwa implemented in a win win situation mfano mdogo tu mapato yatapanda kutoka trillion 7 mpaka trillion 26.7 in just 10 years!
 
They have got a visionary leader Mr Al Makhtoum who is changing this world at a pace that has never been seen before.
He's just an oil baron, with deep pockets. Nothing more, nothing less. You remove oil from the equation, Arab nation like the UAE is nothing but a ramshackle plutocracy, and a civilizational backwater.
 
Point,Nimeanza kufwatilia siasa na kudadisi mambo ya kichumi 2014 nikiwa la 6 inaweza ikawa ajabu lakn ndo ukwel.Nina miaka takrban 10 nafwatilia mambo haya
Nikiangalia mkataba wa DPW na ufafanuz kutoka kwa wataalam mbalmbal mkataba ule unatija kubwa kwa taifa letu kama utakuwa implemented in a win win situation mfano mdogo tu mapato yatapanda kutoka trillion 7 mpaka trillion 26.7 in just 10 years!
Kuna nguvu mbili zinapigana, ile ya magharibi iliyotawala dunia kwa miaka mingi na hii iliyoibuka hivi sasa huko UAE. Hizi ni nguvu mbili zinazokinzana, wazungu wa magharibi wanaona wivu sana pale bandari moja baada ya nyingine zikizidi kuchukuliwa na mwarabu. Heshima aliyoizoea kuwa nayo inakwenda ikipungua na haipendi kabisa hali hii.

Usishangae maaskofu kubadili msimamo wao kwenye suala la bandari baada ya kuitwa Roma na kupewa maagizo ya kuifanyia roho mbaya DPW. Ni vita mbili nzito zinazoendelea.

Lakini uzoefu wa kazi wa DPW unajieleza wenyewe hauhitaji maelezo mengi ya ziada.
 
He's just an oil baron, with deep pockets. Nothing more, nothing less. You remove oil from the equation, Arab nations like the UAE are nothing but a ramshackle plutocracy, and a civilizational backwater.
Nope, arabs of this current generation are well aware on the issue of finding right people with right CVs. Al Makhtoum has a vision and he knows how to reach his goals with the help of right mindsets.

Let us not forget he is a dictator and on the way to all the vast wealth he did not tolerate criticism. In UAE they have a bad history when it comes to human rights matters, he knows how democracy can be an enemy of economic success when given a place to grow.
 
Back
Top Bottom