Utamaduni mpya wa uchumi duniani umeshabadilika, tujiandae kisaikolojia kwenda nao na si kuganda kule kule

Hiyo mikataba Mwarabu anayo ingia huko ulaya ni sawa na Mkataba wa Bongo?
Ni tofauti na pia huko ulaya wanatazama zaidi uwezo wa kazi [substance], huku afrika elimu zetu bado ni ndogo na pia wapambe wa magharibi wanaitumia hali hiyo kama fursa za kupotosha umma juu ya nini haswa kinachotaka kufanyika.
 
Maktomm mbona ni Mzee sana kwa Sasa kama Dubai yote integemea yeye tu it's too risk
 
Kyle Djibouti Walipewa miaka mingapi na kipi kimeleta mgogoro kule?
Sio Djibouti peke yao kuna mataifa mengi walikosea kwenye misingi ya biashara nzima. Naamini kwa kwenda bungeni sisi tumeweka msingi mzuri wa ulinzi wa kisheria.
 
Nadhani nguvu inayoibuka sasa ni BRICS ndio inazipasua vichwa nchi za Magharibi.
40% ya uchumi wa dunia ipo BRICS hapo bado nchi kama Iran,Saudi Arabia,Argentina,Indonesia....hazijaingia rasmi.
 
Ulitaka kusemaje labda kwamba kwakua wana hela sasa tuwape rasilimali zetu wazimiliki bila ukomo?

Middle east hasa saudi na emirate ni mali ya mzungu anaweka civilization hapo ili kuua nguvu ya uislamu,be aware
 
Ufafanuzi gani? Wanasheria waliouandika ni nani?
Hamza Johari CEO wa mamlaka ya anga, Dr Possi mwanasheria wa serikali, Mohamed Said mwanasheria wa wizara n Musa Mbura mwanasheria wa wizara na CEO wa TAA.

Tafuta youtube ile video waliyoongea na wahariri wa vyombo vya habari kuna ufafanuzi wa kina.
 
Ulitaka kusemaje labda kwamba kwakua wana hela sasa tuwape rasilimali zetu wazimiliki bila ukomo?

Middle east hasa saudi na emirate ni mali ya mzungu anaweka civilization hapo ili kuua nguvu ya uislamu,be aware
Ukomo upo kwenye mikataba ya kazi haupo kwenye mkataba uliongia bungeni, IGA haiwezi kuwa na ukomo ni mkataba wa jumla.

Mkuu, waarabu hawana hizi akili zetu za kujifanya tunamjua na kummiliki Mungu, wao wanatazama namna gani wanaweza kufaidika na fursa za kiuchumi.

Wazungu walipiga vita sana kombe la dunia kufanyika Qatar wale jamaa wakawaambia litafanyika hapa kwetu na upuuzi wenu wote muuwache uwanja wa ndege siku ya kuja huku Qatar.

Kuna vita inayoendelea kati ya magharibi na waarabu wanaofanya mapinduzi makubwa ya kiuchumi muda huu.
 
Kwenda zako kule. Unafikiri utamzuga nani akubali dili la kijinga kukabidhi bandari zetu kwa waarabu? Bora tubakie na kasi ndogo ya maendeleo yatakayinufaisha wote huku tuko na uhuru na heshima kuliko kutoa mamlaka yetu kwa waarabu kwa maendeleo ya hao waarabu na mawakala wao nchini.
Kuhusu ulaya usiwasifie. Hao wazungu bure washakua 'hostage' wa mfumo wao mbaya wa kibepari. Kwani huoni wanavyoteseka kutokana na mabepari wa ulaya kuisusua urusi kiuchumi baada ya kuona wameshindwa kuidhibiti kiuchumi nchi hiyo? Ukraine ni kisingizio tu.
 
Pesa Iko Kwa Mwarabu no way out
 
Siasa tupa kule, nchi Dar es salaam inataka kuwa HUB na SSH ameshaamua kufunga vioo, mwekezaji anapokuja anapokelewa tunaongea terms zetu na faster tunasaini mikataba, ujumbe wa Rais kwenye hotuba yake ya mwisho ikulu.

Kuna IGA nyingine mbili zinakwenda kusainiwa ndani ya hii miezi miwili na uwekezaji unaanza kazi mara moja. Nyinyi endeleeni kujidanganya kwa kusema mwarabu hawezi kuchukua bandari yetu.
 
Hao wanasheria wa serikali waliomuumbua rais kwa kumfanya asaini instruments of full powers za Tanzania zinazompa Mbarawa nguvu za kuwakilisha Tanzania na Dubai?

Umeusoma mkataba wewe au unategemea wanasheria wa serikali tu?

Acha ujinga.

Nakwambia hivi, acha ujinga.
 
Mbarawa ni wa kwanza kupewa hiyo authority tangu tupate uhuru?. Huo ujinga ungeuficha wewe kaka Kiranga.

Ni mara ya kwanza kwa rais kukasimu madaraka yake kwa waziri na kisha akasaini mikataba?. yaani unaongea kama vile umezaliwa leo hii mwaka 2023.

Karamagi alisaini mkataba hotelini kule Uingereza akiwa waziri wa nishati, unajua kwamba alifanya hivyo kwa niaba ya Rais Kikwete?.

Na hata marais mara nyingi tu wanawapa mawaziri au makatibu wakuu hizo nguvu za kusaini mikataba na kamera za TV zinarusha live kabisa tukio zima. Rais amekaa katika kiti chake na mawaziri wamekaa katika viti maalum sambamba na wawekezaji wa kigeni wakisaini mikataba.
 
Wewe ngumbaru unaelewa hata nilichoandika?

Unaelewa sijahoji Mbarawa kupewa instruments of full powers kwa niaba ya Tanzania?

Unajua kusoma kwa ufahamu wewe kifulang'unde?

Mkataba umeusoma wewe maamuma?

Haya ndiyo matatizo ya kujibizana na wapumbavu wanaobumbabumba mambo bila hata kujua kusoma kwa ufahamu.

You are an ignoble imbecile.

An insufferable idiot.

A calcified cretin.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…