Utamaduni na uduni wetu

Utamaduni na uduni wetu

princebujonde

Senior Member
Joined
Jan 7, 2013
Posts
198
Reaction score
55
Kwa muda mrefu sasa suala la kuwaelimisha kinadharia na kivitendo vijana wetu hasa mashuleni kuhusu kujua chimbuko lao kama waafrika linazidi kukosa mashiko. Kunaweza kuwa na nadharia nyingi kuanzia mfumo mzima wa uelimishaji fikra hadi ile dhana ya uelimishaji rika. Kujua chimbuko lako ni kujitambua, kujiheshimu na kuelewa misingi na mashiko ya jamii inayo kuzunguka. swali la msingi;je? kwanini mfumo wa taaluma Tanzania umesahau dhana ya utamaduni wa mwafrika? (hapa ondoa hoja ya historical theory), zipo wapi ngoma za asli mashuleni,ngonjera,visasili,nyimbo,sanaa za maonesho nk.Hizo ndio ulkua msingi wa kuamsha hari na morari wakati wa matamko muhimu ya kiserikali na kijamii enzi za azimio la Arusha,Siasa ni kilimo,Azimio la musoma na wakati wa Vita ya Nduli Amini. Hoja kuu hapa ni kuangalia namna tunavoweza kuhuisha (formalizing) dhana ya utamaduni katika mitaala yetu ya elimu hapa nchini. Tuanze sasa kwani bado hatujachelewa.
 
Back
Top Bottom