Utamaduni ni uchumi

Utamaduni ni uchumi

kuna wakati huwa natamani turudi miaka ya 75-80 ila tuboreshe kidogo kwa kadri ya mazingira yaliyopo.
hatukuwa na viongozi wengi majambazi ambao wako tayari wagonjwa wafe kwa kukosa dawa huku wao wakitumia raslimali kwa ubinafsi wao lakini wakizilinda wale waliowaibia wasizichukue na wako tayari kuwaua kwa gharama yoyote.
hatukwa matajiri lakini kwa kiasi fulani tulithamini kufanya kazi kama si kuajiriwa basi kwenye kilimo pamoja kilimo kilikuwa cha mateso na hakikututosheleza.
tulitembea muda mrefu kutafuta elimu zaidi ya km 3 wengine llakinipamoja tulifeli lakini tulitoka tunajua kusoma na kuandika achilia upeo na uelewa uikuwa mkubwa. kwa sasa tunafauru lakini mhn!
tuliishi katika mazingira magumu sukari ikipatikana kwenye duka la ushirika la kijiji kwa kila kaya kununua kilo zisizozidi mbili tena unanunua bidhaa mbili sukari pamoja na glass au viberiti visivyoendana pamoja lakini bado hatukuwa na magonjwa.
tuliweza kuchagua viongozi waaminifu kwaajiri ya jamii na walianzia tokea kwenye jamiia zetu za familia ndogondogo kisha wakapanda kwenye matawi bila kutarajia kuhongwa mlo mmoja na kupoteza vyote.
kwa kiasi wanasiasa na wanajamii waliheshimu taaluma za watu pamoja kuwa wenye taaluma hawakulipwa vizuri.
kwa kiasi tulipendana na kuheshimiana kwa watoto kujua wajibu wao na wakubwa kujua wajibu wao.
viko vingi vizuri lakini katika yote haijalishi tumekosea umbali gani inabidi turudi tutafute njia itakayotuvusha ili tuepukane na kutetea ujinga.

 
Back
Top Bottom