Utamaduni wa kutibu badala ya kuzuia unatugharimu sana kimaendeleo

Utamaduni wa kutibu badala ya kuzuia unatugharimu sana kimaendeleo

Bulesi

Platinum Member
Joined
May 14, 2008
Posts
14,275
Reaction score
13,929
Tumezoea sana kungojea mambo yaharibike ndipo tunaanza kushuhurikia matatizo yaliyojitokeza. Hivi karibuni tumeshuhudia operetion kabambe ikiendeshwa nchi nzima ya kuwahamisha wamachinga kwa gharama kubwa kutoka sehemu zisizokuwa rsmi na kuwapeleka sehemu tunazodhani zitakuwa rasmi kwao. Gharama hizi za kuwahamisha ni gharama ambazo zingeweza kuepukika kama sheria zingefuatwa toka pale walipoanza kuweka biashara zao sehemu ambazo sio rasmi.

Matatizo kama haya pia yako sehemu watu wanapovamia na kujenga nyumba sehemu bila kufuata sheria, mamlaka husika badala ya kutekeleza sheria za kuzuia ujenzi wowote ule holela huwaacha watu wanajenga nyumba au vibanda kwa gharama kubwa bila kuwathibiti halafu baadae wakati makazi yamekuwa makubwa ndipo mamlaka zinazinduka na kwenda kuwavunjia nyumba zao wahusika kwa gharama kubwa kwao na kwa wahusika.

Hivi karibuni huko sehemu za Goba kuna nyumba ya ghorofa ilianguka na kuleta hasara kubwa kwa Maisha ya watu. Kabla ya ajali hiyo kutokea wananchi walitoa tahadhari kwa viongozi wa serikali juu ya obovu wa jengo hilo na kwamba lingeweza kuanguka na kulete madhara; lakini wahusika hawakuchukua hatua mpaka pale ghorofa lile lilipoporomoka ndio wahusika akiwemo mkuu wa wilaya ndio wakaonekana kwenda kuokoa watu waliofukiwa!! Kama hatua ya kumzuia mjenzi zingechukuliwa mapema wananchi walipolalamika hasara iliyotoke ingeepukika!!!

Hivi sasa sehemu za Mbezi beach njia ya kwenda EFM radio kuna mwananchi mmoja ameanzisha karakana yake ya kuchomele vitanda, mageti na nyumba za mabati!! Hatari iliyopo mahala pale ni kwamba kazi zake hizo anazifanyia chini ya nguzo ya umeme ambao unaweza kuleta hitilafu na kudhuru watu wengi sehemu ile. Kwavile sehemu yenyewe iko babarani tena kwenye kona viongozi wengi wanapita pale na kuona ajari inayotengenezwa pale, lakini hakuna jitihada za kuepusha ajali zinazochukuliwa kumuhamisha muhusika kabla ya janga kufika. Hata watu waTANESCO nao hawashituki!!!

Prevention is always better than cure and is less costly! Tubadili utamaduni wetu kwa maendeleo ya nchi.
 
Hakika...

Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Always we focus on problems instead of the source.
 
Back
Top Bottom