Utambulisho wa ushabiki

Trebla84

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2011
Posts
510
Reaction score
637
Ingependeza Kama tungetambuana kwa ushabiki wa timu tunazoshabikia ili hata ukitoa wazo tujue kabisa hapa Simba au Yanga ,,,Liverpool au Arsenal. Trebla hapa Tanzania Shabiki wa Simba,,,Ulaya nipo Arsenal the gunners washika bunduki wa London ingawa sasa bunduki hazina Risasi. Je ww ni Shabiki wa timu Zipi?
 
yaani kuwa shabiki wa simba au man-u ni sawa na kuwa mwana CCM, kuna kitu muhimu umepungukiwa????*** eheeee mfano mzurii ni i yule mpiga domo wa mikia ( shabiki wa simba+ManU) yule yuko sawa kweli yule??,
 
Simba chama langu. Ulaya nimefunga ndoa na Arsenal tunavumiliana kwenye hiki kipindi cha mpito, tupo pamoja kwenye shida na raha, kipindi cha uzima na maradhi mpaka pale kifo kitakapotutenganisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
yaani kuwa shabiki wa simba au man-u ni sawa na kuwa mwana CCM, kuna kitu muhimu umepungukiwa????*** eheeee mfano mzurii ni i yule mpiga domo wa mikia ( shabiki wa simba+ManU) yule yuko sawa kweli yule??,
Wewe timu gani
 
Huu utaratibu wa watanzania wengi kushabikia timu mbili tu (yanga na simba) ndio unarudisha nyuma soka letu, sijui nani aliuanzisha? Naanzisha kampeni ya shabikia timu iliyokaribu na wewe. Kwa kuanza na kampeni Mimi nishabiki wa Mbeya city, ulaya red devil.
 
Ukiachana na siasa za usimba na uyanga, timu za mikoani zipo vizuri kwenye kulisakata kabumbu kuliko hizi timu za kariakoo, wanachozidiwa ni uwekezaji na upendeleo wa viongozi wa soka (TFF +bodi ya ligi) na waamuzi tu. Laiti kama kungekuwa na usawa na haki, sidhani kama hizi timu za kariakoo zingekuwa zinapokezana ubingwa peke yao tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na ni kwa sababu viongozi na waamuzi either ni yanga au simba na ukija kwa mashabiki either yanga au simba na ndio maana suala la waamuzi kuboronga linajadiliwa ikitokea kwa mechi za simba au yanga ila ikitokea kwenye mechi ya ndanda na lipuli inakua sio habari. Hapo ndipo mchawi wa soka letu alipo.
 
Ni kweli zikicheza timu zenye mashabiki wachache hakuna ufuatiliaji unaofanyika,,,
 
MANCHESTER UNITED.

Timu moja tu, nina historia nayo mpaka kuwa shabiki wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…