Utamshauri mtu usiyemfahamu?

Utamshauri mtu usiyemfahamu?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Chukulia wewe ni mfanyabiashara mwenye mafanikio makubwa kwenye biashara yako na hivyo unafahamika kwa watu wengi. Siku moja unapigiwa simu na namba ngeni, na baada ya kuipokea, aliyepiga anajitambulisha kuwa anaitwa Makini.

Baada ya utambulisho, Makini anaanza kujieleza kilichomfanya akupigie. Anakuambia kuwa miezi kadhaa iliyopita aliianzisha biashara kama yako, lakini tokea aianzishe, amekuwa akiambulia hasara tupu. Kwa kuwa anaamini kuwa hasara anayoipata inatokana na makosa anayoyafanya, anakuomba akutafute ili umshauri kwa lengo la kurekebisha makosa.

Makini anakueleza na eneo biashara yake ilipo, na anakupa uhuru uamue kama akufuate ofisini kwako au eneo utakakomwelekeza au asubiri mpaka siku utakayopata nafasi ya kumfuata ofisini kwake.

Utakubali kuwa mshauri wake?

Kumbuka:
1. Hamjawahi kuonana na Makini!
2. Hamfahamiani na Makini, na hata namba zako za simu kapewa na wafanyakazi wako.

Nini utakuwa mwitikio wako?
 
Makini hayupo makini na kazi yake, ushauri wowote ni uso kwa uso.
Amaekupigia simu kuomba miadi na wewe. Anataka muonane ili akusimulie mikasa yote ya biashara yake ili kwa jicho la uzoefu wako, umshauri cha kufanya. Kumbuka anafanya biashara kama yako na wewe umefanikiwa sana kwenye hiyo biashara. Utakubali kukutana naye japo hamfahamiani?
 
Watu waliofanikiwa wanajulikana na wengi sana, kwahy kutokumjua ni kitu cha kawaida
 
Chukulia wewe ni mfanyabiashara mwenye mafanikio makubwa kwenye biashara yako na hivyo unafahamika kwa watu wengi. Siku moja unapigiwa simu na namba ngeni, na baada ya kuipokea, aliyepiga anajitambulisha kuwa anaitwa Makini.

Baada ya utambulisho, Makini anaanza kujieleza kilichomfanya akupigie. Anakuambia kuwa miezi kadhaa iliyopita aliianzisha biashara kama yako, lakini tokea aianzishe, amekuwa akiambulia hasara tupu. Kwa kuwa anaamini kuwa hasara anayoipata inatokana na makosa anayoyafanya, anakuomba akutafute ili umshauri kwa lengo la kurekebisha makosa.

Makini anakueleza na eneo biashara yake ilipo, na anakupa uhuru uamue kama akufuate ofisini kwako au eneo utakakomwelekeza au asubiri mpaka siku utakayopata nafasi ya kumfuata ofisini kwake.

Utakubali kuwa mshauri wake?

Kumbuka:
1. Hamjawahi kuonana na Makini!
2. Hamfahamiani na Makini, na hata namba zako za simu kapewa na wafanyakazi wako.

Nini utakuwa mwitikio wako?
Aje makini ofisini!
 
Namwacha aje, ntamsikiliza anieleze namna alivyoanza na anavyofanya. Nitaona cha kumshauri.

Nilipokuwa chuo nilikua napigiwa na wanafunzi wenzangu wakihitaji msaada wa QM (Quantitative methods) na Probability kwenye courses, wengine hata siwajui na wako desperate kinyama. Niliwasaidia.
 
Mfanyabiasha yeyote makini hatokutana naye na tena hatotamka wazi wazi kuwa hatomuona...
 
Kabisaa!! Kwanza abadilishe jina hilo la makini
Hilo ni jina la kutungwa tu, lakini tukio ni la kweli. Limetokea hivi karibuni.

Bwana mmoja aliianzisha biashara fulani katika mkoa fulani mwishoni mwa mwaka Jana. Lakini mpaka miezi ya hivi karibuni, biashara yake ilikuwa bado inasuasua wakati za wenzake walionzisha kipindi kimoja zikishamiri.

Baada ya kutafakari kwa kina, alibaini kuwa kuna mambo bado hayajui. Ndipo akafikia uamuzi wa kumtafutia mtu mzoefu kwenye hiyo biashara ili amwombe awe mentor wake.

Katika kuwatafuta washauri, ndipo jina la mama mmoja lilipojikita kwenye fikra zake. Aliamini kuwa huyo mama anaweza kuwa msaada sana kwake kwa sababu zifuatazo:
1. Amefanikiwa sana kwenye hiyo biashara kiasi cha kuwa na matawi katika mikoa kadhaa

2. Ni mama mtu mzima hivyo anaamini ataweza kumshauri kwa hekima, ingawa yeye mwenyewe hajawahi kumwona huyo mama. Amepata taarifa zake kupitia wafanyakazi wake na wafanyabiashara wenzake

3. Ana uzoefu wa miaka mingi kwenye hiyo biashara.

Baada ya kufanikiwa kupata namba zake, alijitambulisha na kueleza shida yake. Kwa jinsi alivyojibiwa, bila shaka hatokaa amtafute tena kwa jambo hilo.

Mama alimwuliza:
1. Kwa nini ampigie yeye wakati hawafahamiani?
2. Kwa nini amtafute yeye anayeishi mkoa mwingine wakati kwenye mkoa wake kuna watu wanaofanya biashara kama yake?
3. Kwa nini aliianzisha biashara bila kujiandaa?
4. Atajuaje kama siyo katumwa kumchunguza?
5. Alipataje namba zake?
Maswali yalikuwa mfululizo, hakupewa nafasi ya kuyajibu.

Na alipokuwa anataka kuyajbu hayo maswali, mama alimwambia hawezi kumshauri mtu asiyemfahamu kisha akakata simu.
 
Personally ntamshauri the general things ambazo sio siri bali ni general knowledge.
Kila mtu ana angle yake kwenye business ambayo hata mtu akiiga vipi bado hataweza kuwa efficient kiivyo.
Lakini kuna vitu general ambavyo sio dhambi ukimshirikisha mtu.
Mimi ilishanitokea many times na hua nawashauri bila jam, though kila biashara ina siri zake na hizo huez kutoa bali ni jukumu lake kuzitafuta
Huez kumtafunia kila kitu lakn sidhani kama n kosa kumuonyesha njia
 
Back
Top Bottom