GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Chukulia wewe ni mfanyabiashara mwenye mafanikio makubwa kwenye biashara yako na hivyo unafahamika kwa watu wengi. Siku moja unapigiwa simu na namba ngeni, na baada ya kuipokea, aliyepiga anajitambulisha kuwa anaitwa Makini.
Baada ya utambulisho, Makini anaanza kujieleza kilichomfanya akupigie. Anakuambia kuwa miezi kadhaa iliyopita aliianzisha biashara kama yako, lakini tokea aianzishe, amekuwa akiambulia hasara tupu. Kwa kuwa anaamini kuwa hasara anayoipata inatokana na makosa anayoyafanya, anakuomba akutafute ili umshauri kwa lengo la kurekebisha makosa.
Makini anakueleza na eneo biashara yake ilipo, na anakupa uhuru uamue kama akufuate ofisini kwako au eneo utakakomwelekeza au asubiri mpaka siku utakayopata nafasi ya kumfuata ofisini kwake.
Utakubali kuwa mshauri wake?
Kumbuka:
1. Hamjawahi kuonana na Makini!
2. Hamfahamiani na Makini, na hata namba zako za simu kapewa na wafanyakazi wako.
Nini utakuwa mwitikio wako?