Nafanya kazi ya boda boda muda sasa.. Miezi 2 iliopita nilihama kijiwe maeneo ya sinza nikahamia magomeni
Ebana hiki kijiwe kina abiria balaa yani hukai muda wote uko bizee, Sasa kuna abiria wangu mmoja ni mama mtu mzima huwaga naendaga kumchukua kwake nampeleka kwenye biashara zake kiukweli analipa vizuri sehemu ya buku 1 anakupa buku 5 halafu hata chenji hataki
Juzi amenitumia meseji anataka niwe nae kimapenzi na ameniahidi ataninunulia boda boda yangu, sasa Nimepagawaaa nikifiria hii boda boda ni ya mtu nafanya kupeleka hesabu na ndoto yangu kumiliki boda boda yangu
Ushauri wakuuu