Utamu wa mapenzi sio kuzaa

Utamu wa mapenzi sio kuzaa

majoto

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2013
Posts
2,595
Reaction score
4,775
Nimejisikia kwa kweli kuongelea hili nimesikia wengi baada ya kuwa na mahusiano na kunogewa huanza kudai watoto utamsikia mtu anasema mpenzi si unizalie katoto jamani ona tumekuwa wapenzi muda sasa Wanawake nao anawaza looo bora nishike mimba nimzalie huyu bwana bila ya kufikiria huyo mtoto atalelewa vipi, na yeye mwenyewe ataishi vipi kesho.

Acheni mawazo mgando nyie kama mumeamua kuwa wapenzi endeleeni tu kugegedana bila kuingiza suala la mtoto inapofikia unahitaji mtoto lazima ujipange unazaa na nani, lini wapi na unataka watoto wangapi kulingana hali yako na kipato chako na akiba uliyojiwekea ya kukutosha wewe na watoto wako.

Utakuta mtu hajajiwekea chochote ana kazi ya kufyatua watoto kila kona halafu uzeeni anataka utunzwe zaidi ya yeye alivyowatunza wanawe hakuna hiyo utajikuta unalia peke yako na utaishi kwa uzee wenye shida hadi kaburini utaishia kutoa laana ambazo hazitawakuta hao watoto kisa wamepata bahati ya kuwa na pesa kidogo lakini eti hawakujali, sana sana hizo laana zitakurudia maana utaonekana mzee kituko.

Biashara ya kuwaza kuzaa tuuu badala ya kuwaza wataishi vipi na wewe mwenyewe kesho utakula nini ishindwe na ilegeee kabisaaa ni dhambi kuzaa watoto usioweza kuwatunza na kuwahudumia hata ukiwa ndani ya ndoa, usizae bila mpangilio panga uzazi kulingana na hali yako pia sio lazima uzae.
 
Ndugu ujumbe wako mujarabu sana lakini kama vile unamsimanga mama alokuzaa vile! Ni jukumu letu hasa sisi wanaume kuhakikisha watoto wetu tunawatimizia mahitaji yao yote ya msingi hususan elimu
 
Ndugu ujumbe wako mujarabu sana lakini kama vile unamsimanga mama alokuzaa vile! Ni jukumu letu hasa sisi wanaume kuhakikisha watoto wetu tunawatimizia mahitaji yao yote ya msingi hususan elimu

Namshukuru Mungu wazazi wangu walijipanga tumezaliwa wawili tu ila huwa naona huruma sana kwa waliozaliwa wengi bila mpangilio, na pale wazazi wanapolalamika eti hawatunzwi hali ya maisha ya sasa hata mie ungesema nimtunze mzazi kwa 100% ni mtihani.
 
Yote tisa, kumi mimi nataka katoto sijui kuna mdada yuko tayari tupate mtoto!?


Kuna vingine hutokea pale usipotarajia lakini tunatakiwa kushukuru
 
Namshukuru Mungu wazazi wangu walijipanga. Tumezaliwa wawili tu. Ila huwa naona huruma sana kwa waliozaliwa wengi bila mpangilio, na pale wazazi wanapolalamika eti hawatunzwi. Hali ya maisha ya sasa hata mie ungesema nimtunze mzazi kwa 100% ni mtihani.
upo sahihi
 
sahihi usemalo,mi yamenishinda.unabeba,unalea,unazaa...mwanaume anachokusaidia ni kutupia picha ya mtoto FB like father like a son.mxuuuw

Pole inatupasa kabla ya kubeba tuwe tumejipanga tofauti na hivyo kwa kweli ni mtihani tena hasa kwa hawa wanaume wa leo wana tabia ya kuomba kuzaliwa watoto wakati hawako tayari kutunza watoto usibebe tena hadi uwe na mipango inayoeleweka.
 
Yote tisa, kumi mimi nataka katoto sijui kuna mdada yuko tayar tupate mtoto!?


Kuna vingine hutokea pale usipotarajia lakini tunatakiwa kushukuru

Unasemaje ?pate mtoto bila kujipanga eti vinatokea pale usipotarajia wakati unamwanga mbegu ulitegemea zisiote? acha hizoooo
 
Pole. Inatupasa kabla ya kubeba tuwe tumejipanga. Tofauti na hivyo kwa kweli ni mtihani tena hasa kwa hawa wanaume wa leo wana tabia ya kuomba kuzaliwa watoto wakati hawako tayari kutunza watoto. Usibebe tena hadi uwe na mipango inayoeleweka.
nimekoma,huyo mmoja ametosha
 
nimekoma,huyo mmoja ametosha

Panga mikakati ya huyo mmoja mambo yakiwa mazuri unaongeza, kama vipi mbona anakutosha tu usijisahau kujiwekea mipango yako uzeeni.
 
sahihi usemalo,mi yamenishinda.unabeba,unalea,unazaa...mwanaume anachokusaidia ni kutupia picha ya mtoto FB like father like a son.mxuuuw
[emoji1] [emoji1] [emoji1] huyo anaharibu maana halisi ya baba. Baba ni majukumu sio kujichoresha facebook.
 
nimekoma,huyo mmoja ametosha
Shukuru Mungu kakupa hata huyo mmoja, kuna wadada umri umeenda hawana mtoto wanahaha usiku na mchana kutafuta watoto hawawapati na duniani hakuna mtihani mzito kama mwanamke kutokuwa na mtoto hadi anazeeka. Uzazi wa mpango ni muhimu sana hata hivyo
 
Nimejisikia kwa kweli kuongelea hili. Nimesikia wengi baada ya kuwa na mahusiano na kunogewa huanza kudai watoto. Utamsikia mtu anasema Mpenzi si unizalie katoto jamani... ona tumekuwa wapenzi muda sasa! Wanawake nao anawaza looo bora nishike mimba nimzalie huyu Bwana bila ya kufikiria huyo mtoto atalelewa vipi, na yeye mwenyewe ataishi vipi kesho!!!

Acheni mawazo mgando. Nyie kama mumeamua kuwa wapenzi endeleeni tu kugegedana bila kuingiza suala la mtoto. Inapofikia unahitaji mtoto lazima ujipange unazaa na nani, lini wapi na unataka watoto wangapi kulingana hali yako na kipato chako na akiba uliyojiwekea ya kukutosha wewe na watoto wako.

Utakuta mtu hajajiwekea chochote ana kazi ya kufyatua watoto kila kona halafu uzeeni anataka utunzwe zaidi ya yeye alivyowatunza wanawe. Hakuna hiyo ... utajikuta unalia peke yako na utaishi kwa uzee wenye shida hadi kaburini. Utaishia kutoa laana ambazo hazitawakuta hao watoto kisa wamepata bahati ya kuwa na pesa kidogo lakini eti hawakujali, sana sana hizo laana zitakurudia maana utaonekana mzee kituko.

Biashara ya kuwaza kuzaa tuuu badala ya kuwaza wataishi vipi na wewe mwenyewe kesho utakula nini ishindwe na ilegeee kabisaaa. Ni dhambi kuzaa watoto usioweza kuwatunza na kuwahudumia. Hata ukiwa ndani ya ndoa, usizae bila mpangilio. Panga uzazi kulingana na hali yako.... pia sio lazima uzae.
Nalo neno
 
Shamba bora ni lile lenye kutoa mazao mengi, shida yenu mmeathiliwa na tamaduni za kikafiri(Kizungu), eti uzazi wa mpango!!.
 
Unasemaje ?pate mtoto bila kujipanga eti vinatokea pale usipotarajia wakati unamwanga mbegu ulitegemea zisiote? acha hizoooo
Bahati mbaya ipo mkuu. Maisha si kukariri ni uhalisia.
 
Back
Top Bottom