Nimejisikia kwa kweli kuongelea hili nimesikia wengi baada ya kuwa na mahusiano na kunogewa huanza kudai watoto utamsikia mtu anasema mpenzi si unizalie katoto jamani ona tumekuwa wapenzi muda sasa Wanawake nao anawaza looo bora nishike mimba nimzalie huyu bwana bila ya kufikiria huyo mtoto atalelewa vipi, na yeye mwenyewe ataishi vipi kesho.
Acheni mawazo mgando nyie kama mumeamua kuwa wapenzi endeleeni tu kugegedana bila kuingiza suala la mtoto inapofikia unahitaji mtoto lazima ujipange unazaa na nani, lini wapi na unataka watoto wangapi kulingana hali yako na kipato chako na akiba uliyojiwekea ya kukutosha wewe na watoto wako.
Utakuta mtu hajajiwekea chochote ana kazi ya kufyatua watoto kila kona halafu uzeeni anataka utunzwe zaidi ya yeye alivyowatunza wanawe hakuna hiyo utajikuta unalia peke yako na utaishi kwa uzee wenye shida hadi kaburini utaishia kutoa laana ambazo hazitawakuta hao watoto kisa wamepata bahati ya kuwa na pesa kidogo lakini eti hawakujali, sana sana hizo laana zitakurudia maana utaonekana mzee kituko.
Biashara ya kuwaza kuzaa tuuu badala ya kuwaza wataishi vipi na wewe mwenyewe kesho utakula nini ishindwe na ilegeee kabisaaa ni dhambi kuzaa watoto usioweza kuwatunza na kuwahudumia hata ukiwa ndani ya ndoa, usizae bila mpangilio panga uzazi kulingana na hali yako pia sio lazima uzae.