Utamu wa mkopo umetumiaje

Utamu wa mkopo umetumiaje

Mkanganyiko kukanganya

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2022
Posts
1,204
Reaction score
5,053
Nilikuwa nikipita karibu na ile bank niliyokopa zaidi ya m18 moyo unaanza kimbia na pumzi nayo nzito😂😂😂😂

Mkopo kwa nia ya biashara, kujenga, gari ikatokea tu ghafla paap pesa huioni imekata bila matarajio inaumaa sana. Kimbembe ukiinua salary slip ukitizama basic na take home roho inaumaa zaidi.

Baadhi ya watumishi wanaenda job tu hakuna namna ila mishahara walishachukua siku nyingi 😂😂😂😂😂

Naona mkopo usianze nao biashara bali ongezea mtaji katika biashara, usikurupuke ukaja tesa familia, pata presha au kufilisiwa.

Mimi ni nani nisikope, Serikali yenyewe inakopa. Wajuvi tupeni uzoefu wa mikopo kutoboa nayo.
 
Asili ya mkopo ni utumwa ndani yake na pia ni ngumu mno kuanzisha biashara kwa pesa ya mkopo na biashara ikaenda sawa sawia

Chukua nyaraka za mali yako yeyote kaweke rehani uchukue mkopo mali iliyowekwa rehani ikinusurika kupigwa mnada mshukuru sana Mwenyezi MUNGU.

Mkopo! mkopo! mkopo! nimekuita mara tatu una nini lakini??[emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my OPPO R11s using JamiiForums mobile app
 
Mimi nataka kukopa bank m12 ninunue gari ndogo inisaidie kwenye pilikapilika zangu maana napata shida kwa kweli miguu mibovu inanisumbua siwez kutembea sana, na sina cash kwa sasa ya kununua gari ,inabidi tu nikope ntabaki na take home ya laki saba baada ya makato.silipi kodi nimeshajenga,nasomesha mtoto mmoja. Mungu tu anisaidie nitimize nia yangu maana nishaamua.
 
Ongeza hela kidogo ugize japo IST, ogopa kununua gari za used bongo kwa mkopo. Ikiwa si bahati yako utajuta. So ushauri wangu huo mkopo uwe japo 14M upate IST uagize from japan hutojutia.
 
Nilikuwa nikipita karibu na ile bank niliyokopa zaidi ya m18 moyo unaanza kimbia na pumzi nayo nzito😂😂😂😂

Mkopo kwa nia ya biashara, kujenga, gari ikatokea tu ghafla paap pesa huioni imekata bila matarajio inaumaa sana. Kimbembe ukiinua salary slip ukitizama basic na take home roho inaumaa zaidi.

Baadhi ya watumishi wanaenda job tu hakuna namna ila mishahara walishachukua siku nyingi 😂😂😂😂😂

Naona mkopo usianze nao biashara bali ongezea mtaji katika biashara, usikurupuke ukaja tesa familia, pata presha au kufilisiwa.

Mimi ni nani nisikope, Serikali yenyewe inakopa. Wajuvi tupeni uzoefu wa mikopo kutoboa nayo.

Bodaboda VS watumishi
 
Ulikosea hesabu ndogo .... Ulipaswa kufanya hivi:

hitaji lako ni 18M

Ungetafuta wewe binafsi asilimia 60% ya pesa yote unayohitaji.

60% ya 18,000,000/= ni 10,800,000

Alafu ndio UKAKOPE 40% iliyobakia. Ambayo ni 7,200,000/=

Ungejipa unafuu katika kuirudisha iyo 7.2M

Sio kweli kwamba kama unge-raise 10.8M ungechelewa sana au ungefia katikati ya safari, mbona Bado upo na mpaka imefika mahali unayachukia majengo ya benki uliyokopa.

UHARAKA wa kuchukua 100% mkopo unaua watu sio tu kuwaaibisha.

Benki wanajua tuna mawenge ndio maana wanatuumiza.

Bora ungeumia miaka 2 hata na zaidi kutafuta milioni 10 na laki 8 alafu ndio UKAKOPE iyo milioni 7.2 usingechukia jengo la benki niamini Mimi.
Screenshot_20230309-200701.jpg
 
""Naona mkopo usianze nao biashara bali ongezea mtaji katika biashara"".

#YNWA
 
Ulikosea hesabu ndogo .... Ulipaswa kufanya hivi:

hitaji lako ni 18M

Ungetafuta wewe binafsi asilimia 60% ya pesa yote unayohitaji.

60% ya 18,000,000/= ni 10,800,000

Alafu ndio UKAKOPE 40% iliyobakia. Ambayo ni 7,200,000/=

Ungejipa unafuu katika kuirudisha iyo 7.2M

Sio kweli kwamba kama unge-raise 10.8M ungechelewa sana au ungefia katikati ya safari, mbona Bado upo na mpaka imefika mahali unayachukia majengo ya benki uliyokopa.

UHARAKA wa kuchukua 100% mkopo unaua watu sio tu kuwaaibisha.

Benki wanajua tuna mawenge ndio maana wanatuumiza.

Bora ungeumia miaka 2 hata na zaidi kutafuta milioni 10 na laki 8 alafu ndio UKAKOPE iyo milioni 7.2 usingechukia jengo la benki niamini Mimi.
View attachment 2543456
Huu ushauri unanifaa sana...nauchukua
 
Chukuaa mkopo kuboresha biashara ulishaianza na ikaonekana ina mzunguko wa kurudisha iyo pesa na faida sio kukopa kwajili ya kuanza biashara utakua chizi mapema

Niliwahi pewa idea na mzee flan kwa yule anaeitaji kukopa aanzishe biashara mfano waitaji kuanzisha biashara ya ml10 basi angalau chukua ml15 toa ml10 nyingine iache kwa acc ambayo itarudisha rejesho angalau miez kadhaa huku hii ml10 ikijizungusha
 
Mimi nataka kukopa bank m12 ninunue gari ndogo inisaidie kwenye pilikapilika zangu maana napata shida kwa kweli miguu mibovu inanisumbua siwez kutembea sana, na sina cash kwa sasa ya kununua gari ,inabidi tu nikope ntabaki na take home ya laki saba baada ya makato.silipi kodi nimeshajenga,nasomesha mtoto mmoja. Mungu tu anisaidie nitimize nia yangu maana nishaamua.
Nakushauri tafuta kianzio kwanza mfano m6, halafu m6 nyingine ndio uchukue mkopo.
 
Unaongea tu, mtumishi kujichanga mpaka apate hyo m6 ni kaz labda awe mkuu wa idara kwasabab anapata stahiki za ukuu wa idara lakin kwa mtumishi wa kawaida ni shughur pev
 
Ndio maana ukikopa hela Amana Bank kwa ajili kununua Howo tractor unalipia 30 parentage
 
Back
Top Bottom