Utamwambiaje akuelewe?

Utamwambiaje akuelewe?

sweetdada

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2011
Posts
517
Reaction score
169
Una mpenzi wako wa kiume umekaa nae kwenye mahusiano kwa muda wa miaka mitatu na wakati wote huo mmekuwa mkifanya mapenzi. Imekuja kutokea wewe umeamua kubadili mfumo wa maisha kwa maana ya kwamba umeamua kumrudia Mungu na kuacha ya shetani ila bado unampenda mpenzi wako..na mmeahidiana kuoana.

Je utamwambiaje kuwa wewe hutaki tena ku'do' mpaka pale mtakapooana? atakuelewa kweli?

Nawasalimu wote wanajamvi na nasubiri michango yenu.
 
Sweetdada kuacha ya shetani yapi hayo au unamaanisha kufanya mapenzi kabla haujaoa/haujaolewa??
 
itabidi aone kwa vitendo kama kweli hutaki ku do, sio unasema hutaki wakat faragha unajilengesha...haiji kabisa af hutaeleweka.
 
ni mwenzio find out the right time which u think atakuelewa,use apropriate language i hope kwamba ataelewa though its not that easy
 
Mhh nitamwambia tu Kipenzi unajua miaka 3 ni mingi katika uhusiano kama tabia tumechunguzana vyakutosha sasa unaonaje tufunge ndoa!!!
Kama anakuwa haelewi somo nitajua huyu sio wangu na kuangalia ustaarabu mwingine :love::love::love::love:
 
Sweetdada kuacha ya shetani yapi hayo au unamaanisha kufanya mapenzi kabla haujaoa/haujaolewa??

Ehee hilo ndo nimemaanisha TF...si unajua ukimrudia Mungu inabidi usifanye mapenzi mpaka uoe/uolewe..
 
Ehee hilo ndo nimemaanisha TF...si unajua ukimrudia Mungu inabidi usifanye mapenzi mpaka uoe/uolewe..
Mimi nakubaliana na ushauri alioutoa Maria Roza hapo juu hebu jaribu kuuchukua huo
 
Kama wewe unaweza kwanini udhani yeye hataweza??Anza kwa kumuuliza mnapoelekea..then mshawishi kufanya kilicho sahihi mbele ya muumba wenu.Akileta ubishi mwambie kama anataka aendelee kukufaidi akufanye mke wake au achape mwendo.Kama uko tayari kusimamia imani yako mpya hata kama utampoteza basi mwambie tu plain and simple....maisha haya siyataki tena!
 
Alleluyah!
 
Back
Top Bottom