Utandawazi umesaidia sana kuingiza kipato katika jamii, smartphone ni mtaji wa maisha

Utandawazi umesaidia sana kuingiza kipato katika jamii, smartphone ni mtaji wa maisha

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Huku kwetu Buzza mpaka Kwamtogole ukiwa na smartphone unajiunga na Instagram unatangaza uwezo wako wa kitu chochote unachoweza kufanya. Shughuli isiyohitaji mtaji mkubwa ni kufanya kazi za ndani. Kufua, kupiga pasi, kusafisha vyombo, usafi wa nyumba, kupika nk.

Si watu wengi wanahitaji wafanya kazi wa ndani wa kuishi nao. Hasa wanaume ma bachelor. Unakuta anaingia Instagram akiona mtu anajitangaza kufua, anawasiliana naye na kufanya biashara.

Hii Sekta inakwamua watu kimaisha, uwezekano wa kupata chakula na nauli za watoto kwenda shule upo. Matajiri wengine wanatoa na chai kabla hujaanza kazi na cha mchana pia. Baada ya kazi unapata elfu 20-30 kutokana na ukubwa wa kazi.

Utandawazi umeleta mapinduzi katika Sekta hii ya ajira.
 
Ni kweli dada. Utandawazi umekuja na fursa pamoja na changamoto zake.

Ki ufupi nimejielimisha sana kupitia mitandao na asilimia kubwa za huduma na majibu ya maswali napata mtandaoni.
 
Back
Top Bottom