Utando mweupe katika miti ya michungwa na mapapai!

leipzig

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2013
Posts
2,766
Reaction score
1,708
Utando huu huenea sehemu zote za shina na hata majani na hivyo kusababisha mmea kudhoofika na hata kufa. Nimejaribu kutumia mbalimbali za mimea bila mafanikio kwa vile dawa zote hizo zinzteleza juu ya utando huu ambao ni vipepeo wadogo sana weupe.
Wana JF nimekuja kwenu na kwa wadau ili kupata wale wenye uzoefu katika kilimo waweze kunishauri ni dawa(pesticide) gani inafaa kukabiliana na waxudu hawa waharibifu wa mazao.
 
Mkuu,

Tunao wataalam wengi hapa wawekee picha wakusaidie kwa uzuri zaidi
 
niliwahi kusoma mahali kuwa mipapai isikae karibu na nyanya kuna hao wadudu. Mie nafikiri tembelea maduka ya dawa kuna dawa ya kupiga kwenye majani. Pia nasikia ukitwanga mbegu za muarobaini, aloe vera na kuloweka kwenye dumu wiki ukinyunyizia wadudu hufa sijajaribu ila ni njia organic kama hutaki kemikali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…