Kwenye baraza la kahawa Mpemba mmoja alikua anahadithia jinsi yeye na mke wake walivyosaidiwa lifti ya gari na rafiki yake mmoja jijini hapa.
Alisema: "Wallahi sikujua kama Hamud alikuwa mkarimu hivyo. Tulipotoka tu hospitalini mara tukamuona Hamud huyo anapita na gari lake. Tukampungia mkono, akasimama.
"Baada ya kumuomba sana hatimaye akakubali kutupa lifti. Mke wangu akantia mbele nami akantia nyuma na kisha akawasha gari tukaondoka. Tulimshukuru sana Hamud."