Utani mwingine wa Wapemba

Utani mwingine wa Wapemba

Zak Malang

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2008
Posts
5,404
Reaction score
239
Kwenye baraza la kahawa Mpemba mmoja alikua anahadithia jinsi yeye na mke wake walivyosaidiwa lifti ya gari na rafiki yake mmoja jijini hapa.

Alisema: "Wallahi sikujua kama Hamud alikuwa mkarimu hivyo. Tulipotoka tu hospitalini mara tukamuona Hamud huyo anapita na gari lake. Tukampungia mkono, akasimama.

"Baada ya kumuomba sana hatimaye akakubali kutupa lifti. Mke wangu akantia mbele nami akantia nyuma na kisha akawasha gari tukaondoka. Tulimshukuru sana Hamud."
 
Wewe unazipuliza kwelikweli !!!!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom