Utani ni mzuri na mtamu lakini angalia unayemtania

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
UTANI NI MZURI NA MTAMU LAKINI ANGALIA UNAYEMTANIA.

Anaandika Robert Heriel.

Sisi wengine tumezoea matani, tumezoea kutaniwa, kudhihakiwa, kukejeliwa, hata kuzomewa piah. Mtu aliyebobea kwenye matani hayo kwake ni mambo madogo kabisa.

Sisi tuliozoea utani tunamiiko yetu, tunajua mipaka yetu ya matani, tunajua Nani ataniwe hivi na Nani asitaniwe.

DARASANI au vijiweni Sisi kina Taikon tunakuwaga Radhi kutaniwa Sisi ilimradi Wale watu dhaifu wa matani wasibughuziwe.
Ni kawaida kukuta watu Kama Sisi kila siku tukitaniwa na kijiwe kizima au Darasa zima likituzomea na kutushambulia lakini Sisi wala hatuna habari.

Ni kawaida yetu tukiona kununua ugomvi wa matani tukiona mtu Fulani aliyedhaifu akizidiwa kwenye vijiwe, nyumbani, DARASANI au hata maofisini tunapofanya kazi.

Matani ni sehemu ya Sanaa, ni kipaji Kama vilivyovipaji vingine, hivyo sio kila mtu anaweza matani.

Sisi tujuao matani tuna miiko na maadili yetu tunayozingatia. Moja ya miiko na maadili ya wapenda matani ni Kama ifuatavyo;

1. Usimtanie mtu dhaifu
Kwenye Tasnia ya matani watu dhaifu wapo katika makundi Yafuatayo;
a) Mtu mwenye matatizo ya akili na mihemko(kuongozwa na hisia)
Dalili za mtu mwenye matatizo yenye akili ni pamoja na Kuwa na hasira za haraka haraka, mtu anayeongozwa na hisia kuliko akili,
Mtu anayetoa machozi upesi,

b) Mtu mwenye njaa
Mtu mwenye njaa mara nyingi Sisi wazoefu wa matani hatumtanii maana tunajua mtu mwenye njaa anaweza kufanya Jambo ambalo hata yeye mwenyewe hajalitegemea.

c). Mtu mwenye ulemavu.
Ni mwiko kumtania mtu mwenye ulemavu, mara nyingi utaacha yeye akutanie ili iwe ahueni kwake.
Maadili ya matani yanatutaka kumuachia ushindi mlemavu hata Kama unaona unammudu.

d). Mwanamke
Mtu mbobevu na mahiri katika matani akiwa wa jinsia ya kiume ni nadra Sana kumtania mwanamke. Mwanamke Acha akutanie wewe gusagusa sehemu ndogo usipige mashambulizi makali,
Mwanamke ni dhaifu na mara nyingi huongozwa na hisia ndio maana kanuni ya juu kabisa inasema usitaniane na mtu mwenye matatizo ya akili au anayeongozwa na Hisia.

2. Usitaniane na Masikini
Maadili ya kazi yetu pendwa ya matani inatutaka kutowatania watu fukara na Masikini. Hii kwake anaweza kuitafsiri Kama Dharau kwake.
Ukiwatania Masikini wengi wao watakuona unaringa, unawadharau, unamajivuno na usiyetambua thamani Yao.

3. Usimtanie mtu aliyetoka kufilisika.
Ni mwiko kumtania mtu ambaye ametoka kufilisika au hali yake ngumu Sana.
Kwa mfano mtu alikuwa maarufu lakini umaarufu ukaisha na Hana jipya achana Naye

Acha ataniwe na watu chipukizi katika utani.
Mtu aliyekuwa anapesa akafilisika achana Naye.

4. Usimtanie Mkwe wako.
Sisi wabobevu wa matani ni marufuku kumtania Mama Mkwe au Baba Mkwe, hata Kama yeye atataka utani, wewe cheza Kama Babatovu😀😀

5. Usimtanie Mkuu/Boss aliyekuacha mbali Sana.
Usimtanie Boss awapo kazini, usimtanie Rais, jemadari Mkuu, na Wakuu wote, ikiwa wewe hauna Cheo chochote, Acha wao wataniane.

Wewe huna hata laki kwenye Akaunti unaanzaje matani na mtu ambaye anamilioni Mia moja au zaidi kwenye Akaunti.
Huko ni kutafuta lawama.

6. Usimtanie mke/mume WA mtu, Pia na shemeji yako.
Kwa Sisi wabobevu wa matani ni nadra Sana kumtania Shemeji yako, hasa mke WA Kaka au mdogo wako, au rafiki yako.
Huko ni kumtafuta ubaya ndugu yako.

Usitanie wake za watu hata Kama wanajipendekeza.

7. Usimtanie MCHAWI
Usije ukajichanganya ukamtania mchawi, utalogwa mchana kweupe. Hata Kama mnacheza Bao au Drafti. Achana Naye.

8. Usimtanie mhuni aliyevurugwa.

Kufikia hapo sina laziada.

Ni Yule Mtibeli kutoka nyota ya Tibeli yenye mbawa mbili irukayo huku na Huku.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Mara nyingi utani unapaswa uwe ni tofauti Sana na uhalisia.
Huo ndy utani.

Lakini utani unakuwa ni ukweli na uhalisia huo sio utani.

Huo ni ugomvi.

Mfano mtu ana bichwa kubwa,,
-umtanie bichwa kama Lori la mkaa,,
huo ni utani kwl?
-Mtu mfupi umuite emoro ,

Huu ni ugomvi.

Mwanaume hana kazi wakati mkewe ndy anatimiza majukumu yote ya nyumbani,Kula ,kulipa ada za watoto shule nk,, uje umwite bushoke ,,

Huu ni utani kwl?
Huu ni ugomvi sio utani.
 
Utani unaweza kuwa kweli Mkuu.
Utani pia unaweza kuwa uongo.

Utani ni ugomvi Fulani hivi uliorahisishwa watu wasipigane,😀😀😀
 
Mara nyingi utani unapaswa uwe ni tofauti Sana na uhalisia.
Huo ndy utani.

Lakini utani unakuwa ni ukweli na uhalisia huo sio utani.

Huo ni ugomvi.

Mfano mtu ana bichwa kubwa,,
-umtanie bichwa kama Lori la mkaa,,
huo ni utani kwl?
-Mtu mfupi umuite emoro ,

Huu ni ugomvi.

Mwanaume hana kazi wakati mkewe ndy anatimiza majukumu yote ya nyumbani,Kula ,kulipa ada za watoto shule nk,, uje umwite bushoke ,,

Huu ni utani kwl?
Huu ni ugomvi sio utani.
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Kwani ufupi au mweusi Kama mkaa ni udhaifu??

Au kuwa na kibamia ni udhaifu
Sio udhaifu lakini hupaswi kumtania mweusi utani wa weusi wake.
Mfano,,kumwita mtu black People hata Kama ni black na wewe ukiwa ni white huo ni ugomvi..

Utani unapaswa uwe tofauti na mtu alivyo.
 
UTANI NI MZURI NA MTAMU LAKINI ANGALIA UNAYEMTANIA.

Anaandika Robert Heriel.

Sisi wengine tumezoea matani, tumezoea kutaniwa, kudhihakiwa, kukejeliwa, hata kuzomewa piah. Mtu aliyebobea kwenye matani hayo kwake ni mambo madogo kabisa.

Sisi tuliozoea utani tunamiiko yetu, tunajua mipaka yetu ya matani, tunajua Nani ataniwe hivi na Nani asitaniwe.

DARASANI au vijiweni Sisi kina Taikon tunakuwaga Radhi kutaniwa Sisi ilimradi Wale watu dhaifu wa matani wasibughuziwe.
Ni kawaida kukuta watu Kama Sisi kila siku tukitaniwa na kijiwe kizima au Darasa zima likituzomea na kutushambulia lakini Sisi wala hatuna habari.

Ni kawaida yetu tukiona kununua ugomvi wa matani tukiona mtu Fulani aliyedhaifu akizidiwa kwenye vijiwe, nyumbani, DARASANI au hata maofisini tunapofanya kazi.

Matani ni sehemu ya Sanaa, ni kipaji Kama vilivyovipaji vingine, hivyo sio kila mtu anaweza matani.

Sisi tujuao matani tuna miiko na maadili yetu tunayozingatia. Moja ya miiko na maadili ya wapenda matani ni Kama ifuatavyo;

1. Usimtanie mtu dhaifu
Kwenye Tasnia ya matani watu dhaifu wapo katika makundi Yafuatayo;
a) Mtu mwenye matatizo ya akili na mihemko(kuongozwa na hisia)
Dalili za mtu mwenye matatizo yenye akili ni pamoja na Kuwa na hasira za haraka haraka, mtu anayeongozwa na hisia kuliko akili,
Mtu anayetoa machozi upesi,

b) Mtu mwenye njaa
Mtu mwenye njaa mara nyingi Sisi wazoefu wa matani hatumtanii maana tunajua mtu mwenye njaa anaweza kufanya Jambo ambalo hata yeye mwenyewe hajalitegemea.

c). Mtu mwenye ulemavu.
Ni mwiko kumtania mtu mwenye ulemavu, mara nyingi utaacha yeye akutanie ili iwe ahueni kwake.
Maadili ya matani yanatutaka kumuachia ushindi mlemavu hata Kama unaona unammudu.

d). Mwanamke
Mtu mbobevu na mahiri katika matani akiwa wa jinsia ya kiume ni nadra Sana kumtania mwanamke. Mwanamke Acha akutanie wewe gusagusa sehemu ndogo usipige mashambulizi makali,
Mwanamke ni dhaifu na mara nyingi huongozwa na hisia ndio maana kanuni ya juu kabisa inasema usitaniane na mtu mwenye matatizo ya akili au anayeongozwa na Hisia.

2. Usitaniane na Masikini
Maadili ya kazi yetu pendwa ya matani inatutaka kutowatania watu fukara na Masikini. Hii kwake anaweza kuitafsiri Kama Dharau kwake.
Ukiwatania Masikini wengi wao watakuona unaringa, unawadharau, unamajivuno na usiyetambua thamani Yao.

3. Usimtanie mtu aliyetoka kufilisika.
Ni mwiko kumtania mtu ambaye ametoka kufilisika au hali yake ngumu Sana.
Kwa mfano mtu alikuwa maarufu lakini umaarufu ukaisha na Hana jipya achana Naye

Acha ataniwe na watu chipukizi katika utani.
Mtu aliyekuwa anapesa akafilisika achana Naye.

4. Usimtanie Mkwe wako.
Sisi wabobevu wa matani ni marufuku kumtania Mama Mkwe au Baba Mkwe, hata Kama yeye atataka utani, wewe cheza Kama Babatovu😀😀

5. Usimtanie Mkuu/Boss aliyekuacha mbali Sana.
Usimtanie Boss awapo kazini, usimtanie Rais, jemadari Mkuu, na Wakuu wote, ikiwa wewe hauna Cheo chochote, Acha wao wataniane.

Wewe huna hata laki kwenye Akaunti unaanzaje matani na mtu ambaye anamilioni Mia moja au zaidi kwenye Akaunti.
Huko ni kutafuta lawama.

6. Usimtanie mke/mume WA mtu, Pia na shemaji yako.
Kwa Sisi wabobevu wa matani ni nadra Sana kumtania Shemeji yako, hasa mke WA Kaka au mdogo wako, au rafiki yako.
Huko ni kumtafuta ubaya ndugu yako.

Usitanie wake za watu hata Kama wanajipendekeza.

7. Usimtanie MCHAWI
Usije ukajichanganya ukamtania mchawi, utalogwa mchana kweupe. Hata Kama mnacheza Bao au Drafti. Achana Naye.

8. Usimtanie mhuni aliyevurugwa.

Kufikia hapo sina laziada.

Ni Yule Mtibeli kutoka nyota ya Tibeli yenye mbawa mbili irukayo huku na Huku.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Utani ni Ukweli Pasi na Chuki
 
Sio udhaifu lakini hupaswi kumtania mweusi utani wa weusi wake.
Mfano,,kumwita mtu black People hata Kama ni black na wewe ukiwa ni white huo ni ugomvi..

Utani unapaswa uwe tofauti na mtu alivyo.

Huo sio utani Sasa.

Utani lazima Asilimia kubwa iwe ukweli ili ikukere hapo sio Kwa ubaya😀😀
 
Huo sio utani Sasa.

Utani lazima Asilimia kubwa iwe ukweli ili ikukere hapo sio Kwa ubaya[emoji3][emoji3]
huwezi kumtania mlemavu kwa ulemavu wake,
Huo sio utani.

Utani ni kuongea Jambo ambalo inakwepesha ukweli kiasi.
Huwezi kumwita ,
-mtu mrefu ngongoti,
-Au mfupi andunje.
Unatafuta vita
 
Back
Top Bottom