Utani ni mzuri na mtamu lakini angalia unayemtania

Utani ni mzuri na mtamu lakini angalia unayemtania

Utani wenye ukweli ndani lazima ngumi ziruke, Sasa imagine wewe Heriet ulipata ajali sasa ajali imesababisha upoteze uanaume wako alafu anatokea mtani wako anasema "Vp, kwahio mwanangu we Madem ndo basi Tena huku anacheka"
 
huwezi kumtania mlemavu kwa ulemavu wake,
Huo sio utani.

Utani ni kuongea Jambo ambalo inakwepesha ukweli kiasi.
Huwezi kumwita ,
-mtu mrefu ngongoti,
-Au mfupi andunje.
Unatafuta vita

Ndio maana nimetaja watu ambao huwezi watania hapo juu. Au hujasoma andiko langu.

Utani ni ukweli usio na chuki.

Kwa mfano,

Wapate wakitaniwa ni wachoyo/wabahili si ukweli? Au si utani unaokaribia ukweli.

Au Sumbawanga na watu wa Tanga wakitaniwa kuhusu mambo ya Ulozi si ni kweli?

Au Wachaga wakitaniwa wanapenda hela, si nikweli?

Utani bila ukweli unapoteza uhalisia.

Labda pengine wewe hujui maana ya utani.

Ila utani unamipaka yake kulingana na mtu na mtu.

Hao niliowataja hawahusiki kwenye utani.

Wewe Kama ni mfupi ulitaka watu wasikutanie na ufupi wako😀😀
Kama huwezi utani ni Bora ujikalie kimya waachie wazoefu wa mambo hizo
 
Utani wenye ukweli ndani lazima ngumi ziruke, Sasa imagine wewe Heriet ulipata ajali sasa ajali imesababisha upoteze uanaume wako alafu anatokea mtani wako anasema "Vp, kwahio mwanangu we Madem ndo basi Tena huku anacheka"

😀😀😀

Au anakuambia unabahati ungetolewa kafara kabisa ukafanywe MSUKULE huko.

Utani Kama huujui achana nao.
 
Mara nyingi utani unapaswa uwe ni tofauti Sana na uhalisia.
Huo ndy utani.

Lakini utani unakuwa ni ukweli na uhalisia huo sio utani.

Huo ni ugomvi.

Mfano mtu ana bichwa kubwa,,
-umtanie bichwa kama Lori la mkaa,,
huo ni utani kwl?
-Mtu mfupi umuite emoro ,

Huu ni ugomvi.

Mwanaume hana kazi wakati mkewe ndy anatimiza majukumu yote ya nyumbani,Kula ,kulipa ada za watoto shule nk,, uje umwite bushoke ,,

Huu ni utani kwl?
Huu ni ugomvi sio utani.
Actually huo sio utani wala ugomvi bali hizo ni “kejeli” ama “masimango” kwa lugha nyepesi.

Kawaida ya kejeli huamsha hisia za chuki na hasira hasa pale ambapo yale unayoyaibua kama utani huakisi uhalisia wa nyakati ambazo mtu hupitia. Vitu ambavyo viko nje ya uwezo wa mtu kwa wakati husika.

Mfano: Mtu kuwa hana kazi au mchongo wa kumpa hela za kujimudu halafu unaleta habari za kwamba “wanawake zetu tuwape hela bana heshima iwepo sio mtu unakaa unalishwa na shemeji tu.” Hapo muhuni akikutia ngumi atakua hana hatia kwa sababu wewe ndiye umeleta umama. Unajua hana mchongo na wakati yupo vizuri alikuwa anahudumia familia yake vizuri tu.

Wewe upo kazini una mshahara mzuri ndio maana unajiweza. Unaanza kununua bia na kuanza kejeli kuwa asiyeweza kuzungusha round 3 atoke mezani! Huu ni upumbavu tu sio utani na ukipigwa hatuingilii.
 
Mimi siku ukinitania kuwa Samia ni Rais mzuri👇😁😁😁
gGSRK.jpg
 
Utani wenye ukweli ndani lazima ngumi ziruke, Sasa imagine wewe Heriet ulipata ajali sasa ajali imesababisha upoteze uanaume wako alafu anatokea mtani wako anasema "Vp, kwahio mwanangu we Madem ndo basi Tena huku anacheka"
Hahahahahah utani wowote wenye asili ya kejeli lazma upelekee kichapo!

Una amsha hisia za chuki na hasira sababu unaloliongea mtu hana control nalo! Kwa mfano unamtania mtu kuhusu nguvu za kiume ikiwa kweli hana lazma akuzibue tu.
 
Kwani ufupi au mweusi Kama mkaa ni udhaifu??

Au kuwa na kibamia ni udhaifu
Huo utani umelenga kuumiza hisia za mtu!

Hio ni kejeli na kimsingi mtu hana control na urefu au ufupi. Hicho ndio kitafanya upasuke tu hamna namna ingine
 
Jirani yangu alikuwa msela tu hajaoa....akamleta mdogo wake wa kike kuja kumsomesha huku mjini...Sasa tukiwa kazini site, kuna boya lilikuwa na mazoea ya utani sana na jirani yangu....akaropoka "wewe hanithi wewe..mtoto umemleta pale kwako hata kugonga hugongi kubabako....utachapiwa..kama haisimami sema masela tukusaidie"...kilichofuata hapo hakisimuliki.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Epuka kutaniwa na mwendawazimu
 
huwezi kumtania mlemavu kwa ulemavu wake,
Huo sio utani.

Utani ni kuongea Jambo ambalo inakwepesha ukweli kiasi.
Huwezi kumwita ,
-mtu mrefu ngongoti,
-Au mfupi andunje.
Unatafuta vita
Utani unakuwa neutral endapo hauumizi hisia za mtu. Mfano kwa sie vijana wa kitaa tumezoea kuitana majina ya utani utaskia “oya kichaa angu inakuaje” kimsingi mie sio kichaa so hainiumizi kihisia ila najua ni masihara tu ya ujana...

Mwengine anakuja ana complain “We mama nmekupigia simu sana hupokei qooma ww ushakosa hela” kimsingi najijua mie sio mama. Hilo nalipokea kwa kicheko tu tunagonga 5 maisha yanaendelea.
 
Jirani yangu alikuwa msela tu hajaoa....akamleta mdogo wake wa kike kuja kumsomesha huku mjini...Sasa tukiwa kazini site, kuna boya lilikuwa na mazoea ya utani sana na jirani yangu....akaropoka "wewe hanithi wewe..mtoto umemleta pale kwako hata kugonga hugongi kubabako....utachapiwa..kama haisimami sema masela tukusaidie"...kilichofuata hapo hakisimuliki.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
Unamuita mwanaume hanithi😅???
 
Utani unakuwa neutral endapo hauumizi hisia za mtu. Mfano kwa sie vijana wa kitaa tumezoea kuitana majina ya utani utaskia “oya kichaa angu inakuaje” kimsingi mie sio kichaa so hainiumizi kihisia ila najua ni masihara tu ya ujana...

Mwengine anakuja ana complain “We mama nmekupigia simu sana hupokei qooma ww ushakosa hela” kimsingi najijua mie sio mama. Hilo nalipokea kwa kicheko tu tunagonga 5 maisha yanaendelea.
Hapo ni yale yale Yale ,utani ni kitu ambacho hakuna uhalisia [emoji817]%.

Mfano unaweza kumtania mlemavu wa mkono/ mguu,,
-wewe kiguu Mambo vp?
-au wewe kikono vp?

Au mtu mwenye kichwa kibaya,
-Wewe kibichwa mambo vp?

Huu ni ugomvi.
 
Wachawi , maskin na mwenye matatzo ya akili wasitaniwe , basi sisi watanzania wote hatufai kutaniwa[emoji38]
 
Back
Top Bottom